Kwanini wakuu wote walikwenda kumzika Mzee Kingunge?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,296
2,000
Sisi tusiojua kitu tulidhani kuwa Mzee Kingunge aliharibu CV yake kwa kukihama CCM na kujiunga na UKAWA, lakini haikuonyesha hivyo wakati wa kifo na mazishi yake. Karibu viongozi wooote wakuu waliopo na waliopita walikuwepo kwenye mazishi ya Mzee Kingunge. Mimi binafsi nimejifunza kuwa ukweli unalipa, hivyo Mzee Kingunge alikuwa sahihi ALL the time, hata waliomkosoa walifanya hivyo ama kutimiza tu wajibu wao au hawakumuelewa. Kifo cha Mzee Kingunge kimeonyesha ukweli na kimeliunganisha taifa kisiasa, na ni matumaini yangu kuwa tutaona mabadiliko makubwa ya kimtizamo kama taifa. Taifa kwanza siasa baadae, tushiriki wote kwenye kazi kulijenga au kulibomoa taifa kwakuwa sisi wote tuna maslahi makubwa kwa taifa kusimama.

Je, wewe umejifunza nini kwenye masiko ya Mzee Ngombale?
 

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
4,374
2,000
Nafikiri hilo ndilo jambo jema, wote kwenda kumzika na hivyo hiyo siyo habari. Swali au habari ingekua kama wakuu wote wasingeenda. Suala la Hayati Kingunge kuachana na CCM haliondoi ukweli kwamba mchango wake katika siasa za Tanzania haviwezi kupuuzwa.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
48,905
2,000
Sikubahatika kumuuliza Kingunge, kwanini nchi yetu inamwabudu mungu Mwenge?
 

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
5,496
2,000
Ccm wenyewe wanajua kingunge alikuwa sahihi jpm hafai hata kuwa diwani
 
Top Bottom