kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,298
- 12,600
Sisi tusiojua kitu tulidhani kuwa Mzee Kingunge aliharibu CV yake kwa kukihama CCM na kujiunga na UKAWA, lakini haikuonyesha hivyo wakati wa kifo na mazishi yake. Karibu viongozi wooote wakuu waliopo na waliopita walikuwepo kwenye mazishi ya Mzee Kingunge. Mimi binafsi nimejifunza kuwa ukweli unalipa, hivyo Mzee Kingunge alikuwa sahihi ALL the time, hata waliomkosoa walifanya hivyo ama kutimiza tu wajibu wao au hawakumuelewa. Kifo cha Mzee Kingunge kimeonyesha ukweli na kimeliunganisha taifa kisiasa, na ni matumaini yangu kuwa tutaona mabadiliko makubwa ya kimtizamo kama taifa. Taifa kwanza siasa baadae, tushiriki wote kwenye kazi kulijenga au kulibomoa taifa kwakuwa sisi wote tuna maslahi makubwa kwa taifa kusimama.
Je, wewe umejifunza nini kwenye masiko ya Mzee Ngombale?
Je, wewe umejifunza nini kwenye masiko ya Mzee Ngombale?