Kwanini wake zetu mtoto akikosea anaambiwa "subiri baba yako aje nitamwambia", kama si uchonganishi ni nini sasa?

kwenda21

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
3,422
3,391
Kuna kitabia fulani hivi cha hawa wake zetu wanacho. Utakuta Mtoto kakosea baada ya kumuadhibu utasikia subiri baba yako arudi utakoma. Sasa hii si kugombanisha baba na watoto?

Halafu we ukiwa unatoaga pesa ya matumizi yeye ndo anaenda kununua na kupikia familia; kama ni mahitaji mengine wewe ndo unatoa hela na yeye anaenda kununua na kupatia familia yako, yaani watoto. Kwa hiyo watoto wanamuona yeye mwema na anawajali.

Ila wewe unaonekana kama mtoa adhabu tu, huna umuhimu wowote. Ndiyo maana Mtoto ukiwa unamchapa analia "mama yangu weeeee" na si "baba yangu weeeeee" Jamani, kifupi ni kwamba tukiwa tunatoa pesa za matumizi tuhakikishe na watoto wanaona kwa njia yoyote ile la sivyo shauri yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku hizi sio kihivyo sana.

Kwanza wake hawatuheshimu kwa vile tumelingana kipato na wakati mwingine Mke anachakarika kuliko Baba.

Zamani hizo hiyo ilikuwa ni heshima. Sasa hivi hata watoto wanajua Mama anamzidi Baba Mishe.

Piga kazi.
 
Ila nakumbuka Juzi uliaga. Nashangaa bado upo!!??!🐶🐶
 
Mkuu inamaana hujui sisi wanaume ndo mawaziri wakuu wa vipigo. Tena nafikiri hata huyo mke anaesema hivyo huenda anajua kipigo chako kuwa Ni Cha mbwa Koko😂😂
 
Back
Top Bottom