Kwanini waende Sweden kula Pasaka na kuacha watoto 3?

Sasa wakati anamtesa mama Yake domo .. Mwanaume hata humu wapo wanaotesa wake zako huku watoto wanaona usijidanganye eti wakikua watakuwa on your side ile chuki huwa haiishi kirahisi rahisi
 
Mzee anaonekana Bishoo hawa ndio wale wakizipata mtakoma" Ila sijui nn huyu mzee alifanya kibaya sana mpaka inakua ngumu kusamehewa na mke na mtt wake dah
 
c6dfc__baba2Bdia.jpg


Wakati mwanaye staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na mwanaye Tiffah wakiteketeza kiasi cha fedha kinachokadiriwa kufikia shilingi Mil.100 barani Ulaya walikokwenda kula bata, baba mzazi wa msanii huyo, Abdul Juma anadaiwa kushinda njaa kutokana na ugumu wa maisha, twende na Risasi Jumamosi.

Baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mzee Abdul Juma.
Diamond na familia yake hiyo sambamba na madansa wake, waliondoka nchini mwishoni mwa wiki iliyopita kwenda Frankfurt, Ujerumani ambapo pamoja na kufanya ziara ya kimuziki katika nchi tofauti balani Ulaya, staa huyo aliitumia ziara hiyo kuponda raha.

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ pamoja na mtoto wao Tiffah wakila ‘bata’ Ulaya.

TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kililiambia gazeti hili mapema wiki hii kuwa, baba Diamond kwa sasa ana maisha magumu na mara nyingi amekuwa akishinda njaa huku baadhi ya majirani wakimpa msaada hali inayowasababisha kushangaa baada ya kusoma kwenye magazeti kwamba mwanaye huyo anatumbua fedha kibao na familia yake, ndugu na marafiki huku mzazi wake huyo akiteseka.



“Jamani baba Diamond anateseka! Muoneeni huruma. Alikuja kwangu kuniomba elfu moja lakini bahati mbaya na mimi sikuwa nayo. Mara nyingi amekuwa akishinda njaa. Mbaya zaidi anasumbuliwa na ugonjwa wa miguu na hana mtu wa kumpeleka hospitali. Njooni mumuone yupo hapa kwake anatia huruma,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:


“Kiukweli baba Diamond anasikitisha sana. Tunashindwa kujua tatizo liko wapi kati yake na mwanaye, maana kuna wakati huwa anamsaidia lakini wakati mwingine anampotezea.”
MAPAPARAZI WAMUIBUKIA
Baada ya kuzipata habari hizo, mapaparazi wetu walifika nyumbani kwa baba Diamond, Magomeni ya Kagera jijini Dar na kumkuta nje ya nyumba yake akiwa ameshika tamaa huku akionesha hali ya kunyong’onyea kama mtu aliyekata tamaa ya maisha.

HALI YAKE NI MBAYA
Akizungumza na gazeti hili baada ya salamu, baba Diamond alieleza kwamba bado hali yake ya miguu ni mbaya kwani anatembea kwa kuburuza laiti angekuwa kama zamani angeweza kufanya shughuli ndogondogo za kujipatia kipato angalau apate fedha kwa ajili ya kula hasa katika kipindi hiki ambacho hana msaada.

“Niko hapa bado mambo siyo mazuri, miguu inanisumbua kama unavyoona. Nasikia mwanangu (Diamond) ana ziara nje ya nchi na juzi niliona mmeandika ameteketeza milioni 100 na familia yake, namsubiri akirudi huko naamini atanisaidia angalau fedha hata ya kwenda kwenye matibabu na kula kama ataamua maana alishawahi kuniahidi, hali yangu siyo shwari nabangaiza tu hapa,” alisema baba Diamond.

DIAMOND ASEMAJE?
Alipotafutwa Diamond aliyeko Ujerumani kwa sasa ili aweze kuzungumzia suala hilo alisema hana cha kuzungumza kwa sasa.
“No comment kwa sasa, subirini nikirudi tutaliongea hilo kwa kirefu,” alisema Diamond.

ALIOKWENDA NAO ULAYA
Katika gazeti lenye udugu wa damu na hili, Ijumaa Wikienda la Jumatatu iliyopita, ukurasa wake wa mbele lilikuwa na kichwa kisemacho; DIAMOND
ATEKETEZA SH. MIL 100 ULAYA.

Katika habari hiyo, Diamond aliandikwa kusafiri na ‘ujumbe’ mrefu wa idadi ya watu 14 ambao wote walikuwa chini yake kwa malazi na chakula. Watu hao ni Zari, mama yake mzazi, Tiffah (mwanaye), Romy Jons (DJ wake), Kifesi (mpigapicha), Salam (meneja), mke wa meneja wake mwingine Batu Tale, madansa wanne na dada mmoja ambaye ni ndugu wa Zari. Hao walikwea pipa na kufikia Frankfurt, Ujerumani.

BABA DIAMOND AMEFIKAJE HAPA?
Baba Diamond anadaiwa akiwa angali kijana, alitengana na mama Diamond akiwa na mtoto huyo mdogo kwa miaka mingi bila kumpa huduma zozote kitu ambacho kimemsukuma Diamond kuwa na chuki na ashindwe kumpa matunzo mzazi wake huyo baada ya kupata mafanikio.
Hata hivyo, mara kadhaa Diamond amekuwa akimsaidia fedha baba yake huyo lakini si kwa asilimia mia moja kama anavyomtunza mama yake ambaye anaonekana kula raha hususan kipindi hiki ambacho bwana mdogo huyo kutoka Tandale, maisha yamemnyookea.


Aisee ni fundisho tosha kwa wanaume na wanawake wote wanaotelekeza watoto. Acha wengine wajifunze wajue impacts za kutelekeza familia
 
Hayo ndo mabadilikoooooooo.... alikula bata wakati Mondi na Mamake wanapiga miayo. now zamu yake wacha apige miayo huku Mondi Maza wake wanakula bata batazzzzz....
 
Sasa wakati anamtesa mama Yake domo .. Mwanaume hata humu wapo wanaotesa wake zako huku watoto wanaona usijidanganye eti wakikua watakuwa on your side ile chuki huwa haiishi kirahisi rahisi
Unauhakika kuwa alimtesa? mambo ya ndani kama huyajui we kaa kimya tu ni siri nzito. Wanaume wengi wanakifua cha kutunza siri huoni wakiwajaza sumu watoto wao.
 
huyu mzee aliuza nyumba yao ya urithi kariakoo milioni 200 yote akala bata huku diamond na mama ake wakiteseka acha ale jeuri yake malipo ni hapa hapa duniani
Wanaume huwa tunajisahau sana,

Ila naweza nisimlaumu sana huyo dingi, wanawake aina na Mama Mondi na Mama Wema huwezi kukaa nao hata miaka miwili anaoneka anamdomo mchafu sana...
 
huyu mzee aliuza nyumba yao ya urithi kariakoo milioni 200 yote akala bata huku diamond na mama ake wakiteseka acha ale jeuri yake malipo ni hapa hapa duniani
Sio hiyo tu pia aliuza nyumba aliyoijenga Pugu karibu na Tazara kuelekea kwa Mh. Pinda na fedha hizo kuzitumia kuponda maisha bila kumjali mama Diamond na mwanaye.
 
Ikitokea kafariki ghafla huyu Mzee Diamond atajilaumu sana na wengi wenu humu mtamgeuka....My advice kijana mwenzetu asahau yote na akumbuke huyo ni Mzee wake yalopita si ndwele kuna asilipe ubaya kwa ubaya na kwa kipindi chote alichomkaushia Mzee kashaisoma namba vya kutosha.
 
sometimes mama zetu wanatulisha sumu za hatari aisee uwezi kujua mama na baba walikosana nini wanawake viroporopo sana usikute alimtamkia kua huyu mtoto si wako na baba kwa uchungu akasusa,, Imefikia wakati sasa domo amsamehe mzazi wake mzee anaweza kufa anamlilia hasa anashuhudia hizi anasa wakati yeye anashinda njaa au anaweza fanya kitu cha hatari sana ili wakose wote "KUNA KUSAMEHE BAADA YA KUKOSEWA"
 
Kumbuka mdingi alipiga m200 na kulia bata zote, diamond na mama yake wakat wanateseka
 
Vyo vyote itakavyo kua Mzazi atabakia kua mzazi,yeye kama mtoto atimize majukumu yake kwa mungu na mzazi wake
mwenyezi mungu atamlipa kwa maovu yake...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom