Kwanini waende Sweden kula Pasaka na kuacha watoto 3?

DIAMOND na Baba yake hawana tatizo wanaelewana na huwa anamsaidia sana tu,japo hana ukaribu wa kivile wa Baba na mwana na maongezi yao zaidi ni ya simu si ya kuonana na hata kama ni pesa ni kwa kumtumia kwa njia ya simu si ya ana kwa ana.Haya mengine ni maneno ya magazeti ya udaku ili yauze tu ( labda mzee aseme kwamba hajamuona mwanae laivu muda mrefu ataeleweka.)
 
Ndio akome hii ni dedication kwa mababa wote jina waliojua kuweka mimba tu kisha kukimbia mtt na mamake!yaani mi nafurahi sn diamond anavyomshit babake ni km babake alivyowashit mond na mamake enzi hizo.ndio akome akome akome
 
Ndio akome hii ni dedication kwa mababa wote jina waliojua kuweka mimba tu kisha kukimbia mtt na mamake!yaani mi nafurahi sn diamond anavyomshit babake ni km babake alivyowashit mond na mamake enzi hizo.ndio akome akome akome
Safi sana. Sitasahau baba mwanangu alivyonitia mimba na kunikimbia. Aliniambia kaitoe nina mwanamke wangu nataka kumuoa, we hukujua utapata mimba? Nilipambana nikalea nikasomesha sasa yuko UK for masters maisha safi. Jamaa kajileta anataka mwanae amuombe msamaha! Ni mengi nashindwa kusimulia. Ila mwanangu ameajiriwa NGO ya kimataifa salary nono na benefit nyingine. Ana fiancee wanapendana soonest wataoana. Baba anataka atambuliwe sasa.
 
eti mwana imeakaaje hapa unaenda kula bata za mamilioni kwa obama wakati huku nyuma umemuacha mshua anapiga miayo ya njaa?
Unafikiri kuwa Baba Ni kuchomekea kibamia chako mahali halafu unakimbia bila kujali wala kumwandalia huyo mtt maisha yake ya baadae. Hao mnaopiga domo jiulizeni Ni nn yy kamsaidia huyo mtt mpaka hapo alipofika???
Mtu kukuzaa siyo sababu ya ww kubeba ujinga wake, huyo Baba keanza Ni kijana sana, badala ya kukaa kupiga domo saa zote kama mwanamke au shoga anyanyue jembe akalime
 
Unafikiri kuwa Baba Ni kuchomekea kibamia chako mahali halafu unakimbia bila kujali wala kumwandalia huyo mtt maisha yake ya baadae. Hao mnaopiga domo jiulizeni Ni nn yy kamsaidia huyo mtt mpaka hapo alipofika???
Mtu kukuzaa siyo sababu ya ww kubeba ujinga wake, huyo Baba keanza Ni kijana sana, badala ya kukaa kupiga domo saa zote kama mwanamke au shoga anyanyue jembe akalime
Kuwa baba ni majukumu hata biblia inasema utakula kwa jasho,unatia mimba unakimbia majukumu,mzee boya kweli anajizalilisha tu
 
Hee toba!!! Najuta ku like coment ya kwanza, nimefanya kosa kubwa. Sikujua kwamba mshua aliikataa mimba na kuukwepa wajibu wake, anatuaibisha, anapaswa kupigwa kitanzi.
 
Sio jukumu la mtoto kuhakikisha baba anakula ila ni jukumu la mzazi kuhakikisha mtoto anakula na anamjengea mazingira mazuri ya maisha ya baadae.
 
Kama Dingi alikaa pembeni akamuachia Mama amuwakilishe kwenye malezi basi atulie tu Mama anaendelea kumuwakilisha wakati huu wa mavuno.

Na akipewa good time wengine hawatajifunza kutoka kwake.
 
Na sidhani kama Chibu anakula bata, la hasha bali anachofanya ni sehemu ya kazi zake zinazomuingizia hizo pesa Dingi na wengine wanazozimezea mate.

Kwa mfano hivi mnavyohangaika kuafuatilia amepita wapi...amefika wapi....amevaa nini n.k, ni pesa zinaingia hivoo...so Dingi akauke tu....afuatilie kwenye mitandao kama sisi.
 
Safi sana. Sitasahau baba mwanangu alivyonitia mimba na kunikimbia. Aliniambia kaitoe nina mwanamke wangu nataka kumuona, we hukujua utapata mimba? Nilipambana nikalea nikasomesha sasa yuko UK for masters maisha safi. Jamaa kajileta anataka mwanae amuombe msamaha! Ni mengi nashindwa kusimulia. Ila mwanangu ameajiriwa NGO ya kimataifa salary nono na benefit nyingine. Ana fiancee wanapendana soonest wataoana. Baba anataka atambuliwe sasa.
Yaani hyo ndio fundisho kwa mababa wote hewa yaani hadi raha na hapo hakuna cha kumsamehe wala nini yaani tena ndio unamuombea maisha magumu hadi atembee peku uyo Baba mwehu
 
huyu diamond lazima atakuwa amelaaniwa na wazazi wake.

Wewe unadhani laana inakuja kwa urahisi hivyo, unajua laana inafanya kazi uzuri once upande mmoja utakuwa umeonewa na ukawa na manung'uniko ya dhati juu ya upande wa pili.

Sasa kama Mond ajafanya lolote baya mpaka sasa hiyo laana Mungu anaisainije sasa? Maana Mungu anaangalia kama kuna upande umetenda kosa lolote then anaachilia laana. That's why laana ni two way traffic inaweza kuwa kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto au kwa watoto kwenda kwa wazazi ikichagizwa na catalyst ya uovu katika moja ya pande hzo mbili.

Ndio maana unaweza kukuta kuna baadhi ya familia mzazi kalambwa laana na watoto na inamtafuna vizuri maana watoto wana dhamiri ya dhati na walionewa hivyo laana yao inapewa kibali na Mungu.

My stand; dogo Mond legeza mwili endelea na maisha yako mpe bata mama mpaka akiri kwa kwamba Mungu anabariki vya hatari..dua la kuku halimpati mwewe.
 
c6dfc__baba2Bdia.jpg


Wakati mwanaye staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na mwanaye Tiffah wakiteketeza kiasi cha fedha kinachokadiriwa kufikia shilingi Mil.100 barani Ulaya walikokwenda kula bata, baba mzazi wa msanii huyo, Abdul Juma anadaiwa kushinda njaa kutokana na ugumu wa maisha, twende na Risasi Jumamosi.

Baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mzee Abdul Juma.
Diamond na familia yake hiyo sambamba na madansa wake, waliondoka nchini mwishoni mwa wiki iliyopita kwenda Frankfurt, Ujerumani ambapo pamoja na kufanya ziara ya kimuziki katika nchi tofauti balani Ulaya, staa huyo aliitumia ziara hiyo kuponda raha.

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ pamoja na mtoto wao Tiffah wakila ‘bata’ Ulaya.

TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kililiambia gazeti hili mapema wiki hii kuwa, baba Diamond kwa sasa ana maisha magumu na mara nyingi amekuwa akishinda njaa huku baadhi ya majirani wakimpa msaada hali inayowasababisha kushangaa baada ya kusoma kwenye magazeti kwamba mwanaye huyo anatumbua fedha kibao na familia yake, ndugu na marafiki huku mzazi wake huyo akiteseka.



“Jamani baba Diamond anateseka! Muoneeni huruma. Alikuja kwangu kuniomba elfu moja lakini bahati mbaya na mimi sikuwa nayo. Mara nyingi amekuwa akishinda njaa. Mbaya zaidi anasumbuliwa na ugonjwa wa miguu na hana mtu wa kumpeleka hospitali. Njooni mumuone yupo hapa kwake anatia huruma,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:


“Kiukweli baba Diamond anasikitisha sana. Tunashindwa kujua tatizo liko wapi kati yake na mwanaye, maana kuna wakati huwa anamsaidia lakini wakati mwingine anampotezea.”
MAPAPARAZI WAMUIBUKIA
Baada ya kuzipata habari hizo, mapaparazi wetu walifika nyumbani kwa baba Diamond, Magomeni ya Kagera jijini Dar na kumkuta nje ya nyumba yake akiwa ameshika tamaa huku akionesha hali ya kunyong’onyea kama mtu aliyekata tamaa ya maisha.

HALI YAKE NI MBAYA
Akizungumza na gazeti hili baada ya salamu, baba Diamond alieleza kwamba bado hali yake ya miguu ni mbaya kwani anatembea kwa kuburuza laiti angekuwa kama zamani angeweza kufanya shughuli ndogondogo za kujipatia kipato angalau apate fedha kwa ajili ya kula hasa katika kipindi hiki ambacho hana msaada.

“Niko hapa bado mambo siyo mazuri, miguu inanisumbua kama unavyoona. Nasikia mwanangu (Diamond) ana ziara nje ya nchi na juzi niliona mmeandika ameteketeza milioni 100 na familia yake, namsubiri akirudi huko naamini atanisaidia angalau fedha hata ya kwenda kwenye matibabu na kula kama ataamua maana alishawahi kuniahidi, hali yangu siyo shwari nabangaiza tu hapa,” alisema baba Diamond.

DIAMOND ASEMAJE?
Alipotafutwa Diamond aliyeko Ujerumani kwa sasa ili aweze kuzungumzia suala hilo alisema hana cha kuzungumza kwa sasa.
“No comment kwa sasa, subirini nikirudi tutaliongea hilo kwa kirefu,” alisema Diamond.

ALIOKWENDA NAO ULAYA
Katika gazeti lenye udugu wa damu na hili, Ijumaa Wikienda la Jumatatu iliyopita, ukurasa wake wa mbele lilikuwa na kichwa kisemacho; DIAMOND
ATEKETEZA SH. MIL 100 ULAYA.

Katika habari hiyo, Diamond aliandikwa kusafiri na ‘ujumbe’ mrefu wa idadi ya watu 14 ambao wote walikuwa chini yake kwa malazi na chakula. Watu hao ni Zari, mama yake mzazi, Tiffah (mwanaye), Romy Jons (DJ wake), Kifesi (mpigapicha), Salam (meneja), mke wa meneja wake mwingine Batu Tale, madansa wanne na dada mmoja ambaye ni ndugu wa Zari. Hao walikwea pipa na kufikia Frankfurt, Ujerumani.

BABA DIAMOND AMEFIKAJE HAPA?
Baba Diamond anadaiwa akiwa angali kijana, alitengana na mama Diamond akiwa na mtoto huyo mdogo kwa miaka mingi bila kumpa huduma zozote kitu ambacho kimemsukuma Diamond kuwa na chuki na ashindwe kumpa matunzo mzazi wake huyo baada ya kupata mafanikio.
Hata hivyo, mara kadhaa Diamond amekuwa akimsaidia fedha baba yake huyo lakini si kwa asilimia mia moja kama anavyomtunza mama yake ambaye anaonekana kula raha hususan kipindi hiki ambacho bwana mdogo huyo kutoka Tandale, maisha yamemnyookea.


 

Similar Discussions

Back
Top Bottom