Kwanini wadada mko hivi?

The Garang

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
2,325
4,138
Kwa mara nyingine tena, tunarudi kwenye jukwaa letu pendwa la MMU, Mbarikiwe nyote mnaofanya hii platform ichangamke kwa experiences mnazojumuika nasi humu, tunajifunza na kuyaepuka makosa yaliokwisha fanywa. Wadada Wadada Wadada !!!! ubavu wetu nyie kwanini mko bivi.

Nimekuwa mpenzi wa kusoma riwaya, vitabu mbalimbali viwe ni vya mahusiano kama kina Joseph Shaluwa, E Shigongo na baadhi ha vitabu vya kiingereza nk, pia ni mfatiliaji WA mambo mbalimbali ya kisayansi, teknolojia, Historia za nchi mbalimbali pamoja na viongozi.

kutokana na tabia ya kupenda kusoma vitabu imenifanya niwe na uelewa mpana wa mambo na kuweza kuchangia mazungumzo mbalimbali ma mijadala mbalimbali pale inaponibidi. Hali hiyo imenifanya niwe na marafiki wengi wa kike ambao mara nyingi tumekuwa tukipeana ideas mbalimbali za kimaisha pamoja na kuwasimulia baadhi ya hadithi na experiences nazokutana nazo kwenye hivyo vitabu lakini piaa ninazokumbana nazo humu JF.

Shida kubwa nayokutana nayo ni kuwa mara nyingi katika midahalo hiyo Wanawake wamekuwa ni wapokeaji tu kutoka kwangu, kwa lugha nyepesi natafutwa halafu naambiwa nisimulie story zako. Swali langu, ni kwanini wanawake mko passive sana kwenye mazungumzo sio wote lakini asilimia kubwa, mdada anaweza kukutafuta halafu anataka we ndo uendelee kumchatisha.

Nimeona mahusiano mengi ya mkaka na mdada yapo exploitative in nature, wadada wako kimaslahi zaidi. Kuna jamaa yangu hapa ni kipanga darasani basi kila siku tunashinda tunadeki ruum na kufua mashuka ili wao wakija kudiscuss wasituone wachafu na hakuna siku wameomba hata watusaidie kudeki wala kufagia ruum. Mdada ataumizwa huko na bf wake atakuja kwako umliwaze na umpe attention sawa na anayopaswa kupewa gf wako na akishapatana na bf wake anakusahau tena

Kwenye magrup ya darasan, hamchangii mada hata zinazowahusu nyie, huwa nashindwa elewa shida kubwa ni nini kwamba hamna lolote mnaloweza kulifanya pasipo mwanamme ku initiate. Kwenye ndoa the same, mwanamme asipoomba show ndo basi ntolee hiyo. Ukikutana na mdada mnajuana, usipomshobokea kumsalimia ndiyo mnapishana kama hamjuani kabisa.

Na kwanini mtegemee wanamme katika chattings zenu hali ya kuwa wewe ndo ume initiate convo lakini ushindwe kuelezea. Yaani mambo , ukijibu powaa vipi , unajibiwa saf

#Wadada badirikeni, kama unapenda kupewa story nawe uwe na cha kuchangia next days ili tuzidi faaana na kupeana experiences mbalimbali.

Naomba hii post, itolewe nakala ngumu na kuwekwa kila ofisi ya umma.
 
Mimi ni mkaka ila kama simwelewi mtu, sina conversation na mtu ambae haeleweki...hata nikichepuka na mdada ambae hana sifa za wife material sina mazungumzo nae ajipendekeze kunitafuta kama hataki ndo imetoka hivyo no contacts
 
Sasa kijana yaaan mwanamke sio mke,mpenzi,demu,la Aziz wako unataka aje akufulie ili iweje?
 
Ukiona hivyo
1. Hakuelewi

2. Una ongea sana (much know)

3. Hana interest na mazungumzo

4.Yupo hivyo(introverts)

Mtu huyo huyo unaweza mkuta na mtu mwingine wanafanya majadiliano vyema tu
 
Ukiona hivyo
1. Hakuelewi

2. Una ongea sana (much know)

3. Hana interest na mazungumzo

4.Yupo hivyo(introverts)

Mtu huyo huyo unaweza mkuta na mtu mwingine wanafanya majadiliano vyema tu
inawezekana kwa kiasi Fulani kuna ukweli, lakini kama hauko interested kwanini utake nikupe story ambazo we huzielewi, kwanini usije na mada yako mie ndo nichangie
 
Sasa kijana yaaan mwanamke sio mke,mpenzi,demu,la Aziz wako unataka aje akufulie ili iweje?
huwa wanalala na kulala kabisaa, na michezo yao mingi mingi tu, pia kiungwana kama wao wanatumia room yetu kwa mijadala yao ndo washindwe hata kusema Leo ngoja tuwasaidie kufagia hata ruum.

mda mwingine wanatawala room hadi wenyeji mnashindwa kulala maana vitanda viko viwili nawao wa3 ,wakijigawa hapo mwingine huku huyu huku
 
Mimi ni mkaka ila kama simwelewi mtu,sina conversation na mtu ambae haeleweki...hata nikichepuka na mdada ambae hana sifa za wife material sina mazungumzo nae ajipendekeze kunitafuta kama hataki ndo imetoka hivyo no contacts
hujawai ambiwa ,Fulani mbona umenisusa lakini sio kuwa kweli umemsusa ila unakuta we ndo actor mkuu wa convo yenu so unaona bora nisimtaute kuliko umtafute mtu asioneshe response nzuri.
 
Vitabu vinafundisha inavyotakiwa iwe ...lakini kuna jinsi hali halisi ilivyo,hapo ndio kazi ilipo.
 
Hauja kutana na Miss mzumbe wewe.! Sio mjuaji wala sio wa kujidai ila yule dada anaongea with fact hadi nikamwambia wewe dada mmeo itabidi awe na akili sana na awe na exposer kubwa sana ya vitu vingi zaidi ya hapo atahisi unamuonea na unataka umpande kichwani
 

Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom