Kwanini wachumba, wapenzi au marafiki hukukimbia?

Kwanini wachumba, wapenzi au marafiki hukukimbia?

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,199
Reaction score
7,564
Amenikimbia, hapokei simu tena, hanipigii, hajibu sms, anadai yuko busy kila saa, haji tena, hana time na mimi;Haya maneno yamekuwa yakijitokeza repeatedely humu.

Huwa siandikagi kwenye jukwaa hili lakini ngoja leo niandike kidogo.

Kwa saikolojia ya binadamu, watu huja kwako kwa sababu kuna thamani 'value' flani unatoa na sio vinginevyo.

Hakuna mtu anayevutiwa kuwa karibu na mtu asiyetoa thamani yoyote amma anatoa thamani ya chini sana ukilinganisha na wengine wanaopatikana kwenye eneo husika.

Thamani yaweza kuwa mali au hali. Kuna watu wanakujia kama wachumba, wapenzi au marafiki kwa kuwa unapesa, au kwa kuwa una akili sana, au busara sana, au ushauri mzuri, au unachekesha, au unaongea sana na.k. zote hizo ni thamani.

Sasa limeibuka wimbi la watu ambao hawako tayari kutoa thamani yoyote, yet wanataka wawe na wachumba, wapenzi au marafiki, wakikimbiwa wanalialia kumbe tatizo hawajui hii kanuni.

Kwa mfano, ukiitwa mahali wewe huna nauli mpaka utumiwe hata kama nauli 500 (haijalishi unaitiwa nini), ukifika huwezi kulipia hata soda ya 500, ukiambiwa ule, unaagiza vyakula vya 20,000/ alipe aliyekuita. Kwenye mazungumzo huna cha maana unachoongea, zaidi ya kuitikia mmmh, mmmh, na.k, huna ushauri wala mada ya msingi unaanzishaga, kuondoka huna nauli always. baada ya kufahamiana siku mbili zilizopita, tayari bibi yako kafa, kodi ya nyumba imeisha, shangazi anaumwa, baba kaanguka kwenye mti na yote hayo wewe huna la kufanya. Ukipigiwa simu huongei la maana hata siku moja, mara nyingi unalalamika tu jinsi usivyoweza hili amma lile au usivyokuwa na hii ama kile na.k. kifupi hutoi thamani yoyote kwa upande wa pili. Ukikimbiwa unashangaa shida ni nini.

Conclusion.

Watu wanapenda kuwa karibu na wewe kwa kufuata thamani 'value' unayotoa. Kwa hiyo the more unatoa thamani the more watu watavutika kuwa karibu na wewe na the less unatoa thamani the more watu watakukimbia. Aidha, ukitoa thamani duni sana na wakatokea wanaotoa thamani kukuzidi miongoni mwa sample zilizopo, lazima upigwe chini na wenzako wa win. Hiyo ni kanuni standard ya ulimwengu, wala sio kwamba unaonewa.

N.b katika mazingira flani, factor hii inaweza ikawa na matokeo tofauti kwa sababu ya factor nyingine nyingine
 
value yao chura
Value ni value mkuu. Kwa hiyo itategemea value yako iko wapi. La msingi tu ujue kama iko chini sana, wakitokea wanaofanya vizuri zaidi kwenye eneo hilo, lazima upigwe chini na hiyo ni haki wala sio dhuluma. Ndio maana inashauriwa kuwekeza kwenye character kwa sababu ni manageable
 
Amenikimbia, hapokei simu tena, hanipigii, hajibu sms, anadai yuko busy kila saa, haji tena, hana time na mimi;Haya maneno yamekuwa yakijitokeza repeatedely humu.
Mbona kuna wengine wanakimbia alafu baadaye wanajigonga, kutaka kurud nyuma. Hao tusemeje, au saman kaona baada kuondoka.
 
Mbona Kuna wengine wanakimbia alafu baadaye wanajigonga, kutaka kurud nyuma. Hao tusemeje, au saman kaona baada kuondoka.
Value aliyoifuata katikati ilitoweka, kupungua au alikutana na mwenye value zaidi kwenye eneo hiyo hilo. Kuhusu kurudi, inawezekana value yako iliyokuwa imeungua au kupotea imerudi, au value iliyokuwa imekuzidi ambayo aliifuata imepungua au kuondoka.

Kwa mfano, value yako ilikuwa pesa, katikati kuafulia au akakutana na mwenye pesa zaidi (ataondoka), baadae ukipata pesa tena ( value sababishi) au alikoenda pesa ikipotea atarudi kukubembeleza ( maana value ulimbombo imerudi.
 
Teh mkishafahamiana siku mbili tu mara mjomba kameza shoka

Anyway nashukuru sana mkuu nimejifunza kitu muhimu sana hapa
 
Teh mkishafahamiana siku mbili tu mara mjomba kameza shoka

Anyway nashukuru sana mkuu nimejifunza kitu muhimu sana hap
Ni shida sana mkuu. Yaani unafahamiana na mtu, ndani ya mwezi unajuta kumfahamu. Halafu ukikimbia analeta uzi.


Halafu katika kukimbia kuna wanakimbia kimya kimya. Hawa ndio wengi. Tatizo lao hawatoi fursa kwa wahanga kujirekebisha.

Kundi la pili linawachana wahanga laivu ( hawa ni wachache). Licha ya kundi hili kuchukua hata inayolenga kuwasaidia wahanga kubadilika, mara nyingi wahanga hugeuka mbogo, kununa na.k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom