Kwanini wachezaji wa siku hizi wa kibongo hawana nick names

Observer2010

Senior Member
Oct 29, 2010
195
44
Nikiwa kati ya wafuatiliaji wazuri wa soka la kibongo, nashangaa sana kuona wachezaji wa siku hizi hawapewi majina ya kuwaonesha uwezo wao, ukiondoa John Boko aka Adebayo, sijaona wachezaji wengine wakipewa majina yanayowakaa vema. Katika soka letu la kibongo hadi mwishoni mwa miaka ya 90, kulikuwa kuna wachezaji wana Nick names zinazowakaa kiasi kwamba unaweza kudhani ni jina lake.
Hizi ni miongoni mwa nick nazozikumbuka.
Iddi Pazi “Father”
Mohamed Mwameja “Tanzania One”
Said Mwamba “Kizota”
Salum Kabunda “Ninja”
Hamis Thobias Gaga “Gagarinho”
Makumbi Juma “Homa ya jiji”
Said Mrisho “Zicco wa Kilosa”
Abdalah Kibadeni “King Mputa”
Samli Ayoub “Beki Mtaarabu”
Razak Yusuph “Careca”
Ally Yusuph “Tigana”
Mao Mkami “Ball dancer”
Malota Soma “Ball Juggler”
Nteze John “Rungu”
Zamoyoni Mogella “Golden Boy”
Sanifu lazaro “Tingisha”
Said Sued “Scud”
John Makelele “Zig Zag”
Method Mogella “Fundi”

Hizi ni baadhi tu kati ya nyingi sana ninazozikumbuka. So wadau, kwanini siku hizi hakuna Nick Names kwa wachezaji wetu ? Au ndio tushachoka kabisa hili chandimu letu lenye kila namna na vituko kila kukicha ?
 
kuna yule mchezaji wa PAMBA yamwanza walikuwa wanamwita mbu ana miguu myembamba lkn aki shield mpira huchukuii baba jina lake limenitoka. PAMBA WISH INGEKUWEPO LEO WADAU ILE ILIKUWA TIMU.
 
nicknames ni tuzo anayovalishwa mchezaji husika kwa kuthamini na kuukubali uchezaji wake na kiwango chake kikifananishwa na nick name aliyopewa.wachezaji wengi hivi sasa hawana performace inayofikia mizania ya comparison na magwiji mbalimbali na kandanda..sasa kuwatunuku tu itakuwa kudhalilisha sifa za hizo nicknames
 
1-Mussa Hassan(MGOSI)
2-Seif Mohamed(KIJIKO)
3-Amri Said(STAM)
4-Kelvin Yundan(VIDIC)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom