Kwanini wabunge hawakushirikiana walipofukuzwa wanafunzi wa St. Joseph ila kwa wa UDOM wapo pamoja?

RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2016
4,335
10,558
Tungeomba wabunge watolee ufafanuzi hilo swali hapo juu.Maana mazingira na utaratibu uliotumika kuwafukuza wanafunzi wa vyuo tajwa hapo juu unafana.

Lakini wabunge wamelipa suala la UDOM uzito wa hali ya juu kuliko wanafunzi wa St Joseph waliotimuliwa,sababu ni nini?.

Je wanafunzi wa St Joseph hawakuonewa ila isipokuwa wa UDOM?

Je wanafunzi wa St Joseph hawana haki yakutetewa na wawakilishi wao waliopo bungeni kuliko wa Udom?

Mwisho nawaunga mkono wabunge kwa kushirikiana katika suala hili,lakini ningeomba pia watoe ufafanuzi juu ya double stand yao.
 
Mkuu huyu mama anaanza kushughulikiwa baada ya kuvuka mstari uliopigwa marufuku, kwani ni mara ya kwanza ktk Nchi hii kufukuzwa wanafunzi. Lkn mwisho wa Siku haya yote ni kutoka na na watu kuweka siasa hata kwenye mambo serious.
Mkuu jazilizia nyama,utafahamishe ni mstari upi aliovuka?.
 
kwakweli ni bora hivyo hivyo kuwa wabunge hawakuwatetea wanafunzi wa st.Joseph, aisee wameletwa hapa SUA hao wanfunzi ambao walitolewaga st. Joseph yaani ni vihiyo vya nguvu. Kwakweli hata SUA wameshaliona hilo kwasasa wanasubiri kuwapiga disco..!
 
Wakati huo halikuwepo tishio la Vyeti Feki!
Usiwe na mawazo ya kipumbavu suala la vyeti feki haliwahusu wabunge mtu kama Nassari aliyeleta hoja ana elimu nzuri, elimu ya mbunge ni kujua kusoma na kuandika.
 
Hapo tatizo sio chuo ujue kuongezeka kwa idadi ya vyuo kunashusha viwango maana miaka ya leo ukipata div 3 unaenda kusomea udaktari
 
wale wa UDOM wamepelekwa na serikali yenyewe na ile kozi haikuwepo imeanzishwa na serikali na kuzinduliwa na rais wa awamu ya nne
 
Muache kufukiri kwa kutumia mfumo wa majitaka. Wabunge hawajataka kujadili kwanini wameondolewa chuoni bali NAMNA walivyoondolewa chuoni. Yaani ulitaka watu wajadili UPUUZI kutetea watu division four zisizo na sifa hata ya kusomea astashahada wasome shahada? Bila shaka na wewe ni mmoja wa wahanga wa St. Joseph tukiangalia na kiwango cha ufikiri wako.
 
Wa UDOM walipelekwa na serekali yenyewe baada ya kuona upungufu wa waalim wa sayansi so kuwashawishi wanafunzi waliofaulu vizur waombe na ili kuwashawishi kabidi iwapatie mkopo 100% na uhakika wa ajira pindi wakimaliza na moja ya vigezo ni ufaulu mzuri wa masomo ya sayansi.

Sio kweli kuwa form 4 anasoma dip ya miaka 2 Bali ni miaka 3, wakati aliyemaliza form 6 anasoma kwa miaka 3. Vigezo vya udahili viliwekwa na serekali hivyo wanafunzi kudahiliwa so wanafunzi hawana makosa
 
Mkuu huyu mama anaanza kushughulikiwa baada ya kuvuka mstari uliopigwa marufuku, kwani ni mara ya kwanza ktk Nchi hii kufukuzwa wanafunzi. Lkn mwisho wa Siku haya yote ni kutoka na na watu kuweka siasa hata kwenye mambo serious.
Hakuna wanafunzi walio fukuzwa si wa St joseph wala UDOM! Wa St joseph chuo chao kilishindwa kutimiza masharti kwa hiyo wote wameamishiwa vyuo vingine tena hapa tunaongelea Arusha campus!

Pia swala la UDOM wanafunzi wameambiwa warudi nyumbani mpaka watakapo tangaziwa! Mlitaka wake chuoni kufanya nini ikiwa Walimu wamegoma?

Swala la St Joseph Arusha Campus na UDOM ni vitu viwili tofauti!
Tungeomba wabunge watolee ufafanuzi hilo swali hapo juu.Maana mazingira na utaratibu uliotumika kuwafukuza wanafunzi wa vyuo tajwa hapo juu unafana.

Lakini wabunge wamelipa suala la UDOM uzito wa hali ya juu kuliko wanafunzi wa St Joseph waliotimuliwa,sababu ni nini?.

Je wanafunzi wa St Joseph hawakuonewa ila isipokuwa wa UDOM?

Je wanafunzi wa St Joseph hawana haki yakutetewa na wawakilishi wao waliopo bungeni kuliko wa Udom?

Mwisho nawaunga mkono wabunge kwa kushirikiana katika suala hili,lakini ningeomba pia watoe ufafanuzi juu ya double stand yao.
 
Hili swali ni kuntu ngoja niwangojee wataalam wa mambo ya mtambuka waweze kulidadavua kiunagaubaga
 
Back
Top Bottom