Kwanini waafrika hatuna desturi za kujiudhuru au kukataa teuzi?

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
615
Katika nchi za Afrika ni nadra sana kuona kiongozi anajiudhuru hasa pale inapotokea tatizo katika eneo lake la kiuwajibikaji. Viongozi au watu waliopewa dhamana fulani hawana desturi ya kuwajibika wengi husingizia kuwa hilo jambo au tatizo limefanywa na mtu wa chini. Halikadharika katika nchi nyingi za Afrika watu wengi hawana desturi ya kukataa teuzi hata pale ambapo wanaelewa fika kuwa hawana uwezo au wana mgongano wa kimaslahi au kwa kufanya hivyo watadhoofisha taaluma zao.

Hii ni tofauti kabisa na nchi za Ulaya ambapo ni jambo la kawaida kabisa kuona mtu akiwajibika hatakama hakuna ushaidi wa moja kwa moja kama amehusika kwenye jambo fulani. Aidha ni jambo la kawaida mtu kukataaa uteuzi. Hivi karibuni tumesikia viongozi walioteuliwa na Rais wa Marekani wa kikataa nyadhfa kubwa kabisa ambazo zingewaletea heshma pamoja na maslahi makubwa.

Wanataaluma wa kweli ifike sehemu wakatae baadhi ya teuzi ili umahiri walio nao usije ukapotea kwenye nafasi za kisiasa, ambapo anguko la kisiasa linapotokea mtu hupoteza vyote, kwani ukisha kubali kuingia kwenye teuzi za kisiasa na kwa bahati mbaya ukawajibishwa ni ngumu sana kurudi kufanya mambo ya kitaaluma kwa kujiamini kwani anguko linalotokana na siasa lina athari kubwa sana kiasi cha kupoteza kuaminiwa utakapo jaribu kurudi kwenye mambo ya kitaluma.
 
Ni kweli ni vigumu sana kwa viongozi wa Africa kufanya hivyo because uchu wa madaraka upo kwa sana
 
Alivojiuzuru david Cameron baada ya kura ya brexit ndio imeonesha wazungu hawana mchezo kwenye siasa. Sera zako zikishindwa unakaa pembeni kwasababu Viongozi wapo wengi tu sio wewe peke yako. Ila huku Africa unakuta nchi ina njaa, elimu mbovu, ajira hamna lakini Viongozi anakaa madarakani miaka 20 na hataki kusikia habari za kujiuzuru na hata akishindwa uchaguzi inabidi atolewe kwa nguvu kama yule raisi wa Gambia. Mi nafikiri ni kwasababu sisi tunawatukuza sana Viongozi wetu hadi wanajiona wao ni kama mungu.
 
Sababu kuu ni njaa na dhiki, anafikiria baada ya kujiuzulu atapata wapi ugali kulisha familia.

Waziri wa katiba na sheria ni mwalimu wa sheria, mbali ya kuziishi hizo sheria pia kawafundisha wanafunzi wake.
Leo anaulizwa vipi mbona bwana yule anaenda kinyume anasema aliona vyema azuie ili watu wafanye kazi,

Somo; woga unafiki na njaa
 
Rangi nyeusi= kiza kinene kwenye ubongo ,haijalishi mtu kapata elimu au la!
Wachache mno ndo wamekombolewa fikra zao.Hivi kama mtu kila akipanda jukwaani kazi yake ni kujisifia na kurudia kunena yaleyale hivi mtu huyo ana akili kweli?
 
Umaskini wa nchi. Unapelekea kutokuwa na biashara/ajira mbadala. Mtu akifikiri akiiacha hiyo nafasi ndio basi tena. Elimu aliyonayo haina fursa za kuifanyia kazi.
 
Viongozi wengi wana vyeti feki. Siasa ndio mahala salama pa kujifichia!
 
Vipi, huu Uzi wako kwani unauhusiano wowote na uteuzi wa hivi punde barani afrika, nchini Tanzania?
 
Katika nchi za Afrika ni nadra sana kuona kiongozi anajiudhuru hasa pale inapotokea tatizo katika eneo lake la kiuwajibikaji. Viongozi au watu waliopewa dhamana fulani hawana desturi ya kuwajibika wengi husingizia kuwa hilo jambo au tatizo limefanywa na mtu wa chini. Halikadharika katika nchi nyingi za Afrika watu wengi hawana desturi ya kukataa teuzi hata pale ambapo wanaelewa fika kuwa hawana uwezo au wana mgongano wa kimaslahi au kwa kufanya hivyo watadhoofisha taaluma zao.

Hii ni tofauti kabisa na nchi za Ulaya ambapo ni jambo la kawaida kabisa kuona mtu akiwajibika hatakama hakuna ushaidi wa moja kwa moja kama amehusika kwenye jambo fulani. Aidha ni jambo la kawaida mtu kukataaa uteuzi. Hivi karibuni tumesikia viongozi walioteuliwa na Rais wa Marekani wa kikataa nyadhfa kubwa kabisa ambazo zingewaletea heshma pamoja na maslahi makubwa.

Wanataaluma wa kweli ifike sehemu wakatae baadhi ya teuzi ili umahiri walio nao usije ukapotea kwenye nafasi za kisiasa, ambapo anguko la kisiasa linapotokea mtu hupoteza vyote, kwani ukisha kubali kuingia kwenye teuzi za kisiasa na kwa bahati mbaya ukawajibishwa ni ngumu sana kurudi kufanya mambo ya kitaaluma kwa kujiamini kwani anguko linalotokana na siasa lina athari kubwa sana kiasi cha kupoteza kuaminiwa utakapo jaribu kurudi kwenye mambo ya kitaluma.

njaa, ukatae teuzi au ukatae ulaji tena? ujiuzulu ule wapi tena?
 
Back
Top Bottom