Kwanini Viongozi wa ACT Wazalendo wamedanganya umma kuhusu Jengo lao Jipya?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,693
218,212
Nimetafakari sana kuhusu Jambo hili na hasa Wadanganyaji wenyewe kuwa viongozi wa juu wa Chama, akiwemo Zuberi Zitto, sijaelewa hasa LENGO LAO LA KUDANGANYA JAMBO LINALOFAHAMIKA.

Ni kweli kabisa kwamba wamezindua Jengo la ofisi yao kuu ya Tanganyika, Jengo hilo linaitwa "MAALIM SEIF" , lakini Jengo hilo hawakujenga kama wanavyojinadi mbele za umma bali wamepaka rangi na kuchomea na kupiga Puti mageti yaliyokuwa yamechakaa ama kushika kutu, Hili Jengo lilikuwa la Maalim Seif na lilitumika na Cuf ya Upande wake, wakati ule CCM iliyoongozwa na Magufuli ilipoamua kumlipa fadhila Haruna Lipumba.

Kulikuwa na Ugumu gani kwa viongozi hawa wa ACT kusema tu kwamba nyumba hii ni ya Mwanachama wetu ila tumeipaka rangi na kuweka sofa mpya ? Uongo wao huu umelenga nini? Sisi wengine tumefanya siasa na Maalim Seif tena katika jengo hilohilo, tunafahamu tunayoyaandika.

Bali ifahamike kwamba 2015, wakati wa ule uchaguzi mkuu ambao Maalim Seif alidhulumiwa Ushindi wake wa kishindo kule Zanzibar na CCM, Tiss , Polisi na mshirika wao Salim Jecha, Wabunge wote wa Upinzani waliondoka bungeni Kupinga Dr. Shein aliyeangukia pua kuingia bungeni kwenye uzinduzi wa Bunge, aliyeitwa Mpinzani aliyebaki kwenye uzinduzi wa bunge lile lililokuwa na Mjumbe haramu Dr. Shein alikuwa Zitto Kabwe (Tafakari)

Watu wa Pwani wana msemo mmoja kwamba, Nanukuu "KAMA KIBABA HAKIKUJAA NDOO HAIWEZI KUJAA" mwisho wa kunukuu.
 
Bado tunarudi kulekule shit hole country.

Unajinasibu vipi mbele ya umma jengo la mtu binafsi kuwa limejengwa na chama
Unaweza kutoa ushahidi kuwa jengo la mtu na sio chama wamejenga? Au kusema ni jengo la mtu ni mbinu yenu Chadema kupunguza maumivu ya kutokuwana Ofisi huku mkijinadi eti mkiingia madarakani mtawaletea maendeleo wananchi?
 
Back
Top Bottom