Kwanini vijana wa siku hizi wanasema mapenzi yalikuwa zamani ?

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
4,640
4,426
Kwanini vijana wengi wa siku hizi wanasema kuwa,mapenzi yalikuwa zamani ila kwa sasa ni wizi na udanganifu mwingi?

Ni kweli mapenzi yalikuwa zamani,zile zama zetu sisi ila kwa vijana wa sasa poleni sana.mapenzi hakuna tena zaidi ya wizi na udanganyifu mtupu.

Zamani unamtongoza msichana leo,anaomba miezi 6 ya kukufikiria.ikiisha anaomba umuongezee miezi mingine 6 ya kukuchunguza,yaani ndani ya muda wa mwaka mzima bado unakuwa na shauku naye.
Na ndani ya huo mwaka wote wa kukufikiria na kukuchunguza,hujapata hata nafasi ya kumshika hata mkono.
Akikukubalia sasa mnapanga siku ya kukutana kwa ajili ya maongezi,siku hiyo unavaa vizuri sana ili upendeze,na pia siku hiyo unakuwa na uhakika kuwa utamshika hata mkono,hivyo unasafiri umbali wa kilometa 10 au 15 kwa miguu ili kwenda kumshika mkono mpenzi wako.
Unaishi mwaka mwingine ukiwa katika mahusiano na mpenzi wako,na hujawahi kuona hata goti tu.mkija kuwa pamoja hamuwezi kuchokana maana kila siku ataonekana mpya kwako,hasa pale unapokumbuka ni jinsi gani ulivyomsumbukia.

Ila leo hii sasamsichana kabla hujamtongoza ulishaona kila sehemu ya mwili wake,na ukimtongoza hana kukuchunguza wala kukufikiria,ndani ya dakika 5 mambo yameisha.
Mnaingia kwenye mahusiano msichana anakuwa hana kitu special cha kujivunia kwa mvulana wake.maana vyote mvulana aliviona kabla ya kumtongoza.
Ndio maana mahusiano ya siku hizi yakidumu sana ni wiki moja tu,yaani yanazidiwa hata na kifurushi cha mwezi.Lakini hayo yote yanaletwa na waschana wao wenyewe,wewe unapopost picha za nusu uchi au uchi kabisa sio ujanja huo.bali ni kutia tamaa vijana,na kawaida ya tamaa huisha haraka.hebu angalieni utamu wa Big G na muda wa kuisha utamu ule.

Hakuna mwanaume mjinga ambaye anaweza kuoa msichana aliyekuwa anapost picha za hovyo mitandaoni,halafu anatag wanaume ili waone alivyoumbwa kwa ndani eti kesho anataka aheshimike.
tapatalk_1504328020027.jpeg
-%20BYiNqzQg7f0%20Image%20by%20gift_of_africa.jpg
 
Back
Top Bottom