Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,725
- 830,783
- Thread starter
- #21
Reasoning kama hizi ndio zinawafungua watu, kwa upande wangu mambo ya rangi sijui namba ya bahati au matukio kuhusisha na rangi hua haipo kabisa.
Kwenye kila kitu kuna dunia 3
1.dunia ya uhalisia- sayansi na technolojia
2.dunia ya kufikirika -mambo ya rangi nyota uchawi ushirikina ulozi nk
3.dunia tusiyoitambua-vitu vinatokea bila uwezo wetu akili zetu wala maarifa yetu.Dunia ya Mungu
Sasa kwa asilimia kubwa wengi huchanganywa na kushindwa kujua kuwa aishi au kufuata dunia gani kwakuwa zote zipo kwa wakati mmoja na Zikiwa na mahusiano nawe kwa njia moja au nyingine
Mkanganyiko unakuja zaidi zinapochanganyika na mila desturi na tamaduni za sehemu mbalimbali ..usipokuwa makini na kujua unataka kujikita kwenye nini kujua kipi na kufuata nini..shida huanzia hapo
Kwa mfano kwenye hizi mada unaona kabisa baadhi ya replies mtu anajibu kutokana na muktadha huo hapo juu dunia ya 1-3 au tamaduni mila na desturi za mahali fulani