Nimekuelewa hapa nilikuwa najazia tu maana kaniki kwa Dodoma ni kama Suti kwa MwanasheriaNimechukulia dhana nzima kwa mtazamo wa jamii na mifano niliyotoa na uhalisia wake kama nilivyojaribu kuainisha hapo kwenye post
kwa sababu kule kijijini kwetu ni vazi la kawaida sana,sasa unapohisi limetengenezwa ama linavaliwa kwa lengo maalum ndo nataka kufahamu hapo
Inaelekea kijijini kwenu ndio kwenyewe kwa mambo hayo. Shughuli zote za uganga na uchawi lazima kaniki iwepo. Sehemu utakapoona matumizi ya kaniki ni makubwa tambua kuwa uchawi na uganga vipo kwa kiwango hicho hicho. Swali la kujiuliza ni kwa nini kaniki iwe ndiyo vazi kuu?
Naomba kujua mshana jr, kama mtu kavaa kaniki ambayo inasadikiwa kuwa ina mambo ya giza, yaani mfano mdada wa kazi kaletwa kwenye mji ambao wanafanya mambo ya giza, ya kichawi kwa maana hiyo, na huyo binti akawa akienda labda kufua, anapewa hiyo kaniki na kuivaa kila mara, na bila ya kujua undani wake. Nauliza anaweza pata madhara yoyote?! Nijuze Plz!
Ahsante!
Hawa ni Rabbi wa Kiyahudi, dini isiyowataka lakini nyie hamuishi kuishobokea kila uchao, nao vepeh? Acha kupotosha mkuu....
Uchangie kwa kuuliza kama hivi..kumbuka kuna post mwendelezo zaidi ya kukufikirisha kama hivi
Tuongezee tu kidogo, hata kwenye misiba rangi nyeusi inatawala kwa kawaida na kwa kua ndio rangi ya kaniki, wajuvi watatusaidia hapo.
Cha ajabu ile sanda hua inakua nyeupe...kitu kinachozidi kuuchuja huu mtanange kuzidi kujikita kwenye rangi nyeusi na nyeupe ​kwenye mambo ya imani.
Yeah ni sahihi lakini Ukiangalia hapo si imani zote zinatumia sanda na pia kwa mfano wachina rangi ya msiba kwao ni nyeupe na si nyeusi