Acheni habari za vijiweni Maticha, Hizo habari za Rita ni huko kwenye kuomba mikopo ya Elimu ya juu au Kati.
Huku utaratibu umeainishwa kwenye tangazo la kazi husika, toa kopi nyaraka zako zote za kitaaluma, na vyeti vingine, peleka kwa hakimu athibitishe kwa kukugongea muhuri, hii ilikuwa kipindi cha kufanya maombi ya kazi na kama ulifanya kinyume chake interview utaisikilizia kwenye vyombo vya habari.
Endapo umeitwa interview wewe beba nyaraka original, nenda nazo kwa ajili ya uhakiki, pale hawahitaji muhuri wa mahakama, labda kama una kiapo au deedpoll.