Nadhani mkuu hujaelewa mantiki nzima ya huu uzi.....hata hao matajiri uliowatolea mfano....wote wanatimiza mahitaji yao ya leo na baadae kupanga mahitaji ya kesho........wanaifikiria kesho baada ya kukamilisha na kuyatimiza ya leo.......Mawazo ya kiafrica haya, ila sishangai ndio tumeumbwa hivyo, nenda hata marekani mamilionea wanaoongoza kwa kufilisika ni wenye asili ya africa, makampuni ya kizungu, kiyahudi, hata kihindi yana survive miaka 200 lakini kampuni za kiafrika zikidumu sana ni kizazi kimoja halafu zinakufa.
races zote zimetuacha nyuma kwa miaka 100 na zaidi badala ya kufikiria ku save kwa ajili ya kujiendeleza sisi na vizazi vijavyo tunajifikiria namna ya kutumia fedha tuizozipata ili tusije kufa kabla ya kuzifaidi!!!
na watu wanapata kazi wanalipwa fedha nyingi wanajiachiaaa sana, miaka inapita anastaafu hana kitu zaidi ya mafao yake, watoto unakuta amewasomesha shule za ghali ila hawana ajira wala discipline ni uzururaji na kuvuta bangi,
au ana biashara nzuri badala ya ku save hata awekeze zaidi ili atoe ajira zaidi kwa wengine yeye ni ku spend tu kwa kuwa ana uwezo wa ku spend, eti kesho au miaka 10 ijayo naweza kuwa nimekufa, sasa hata ukifa huna ndugu au watoto ambao watasaidiwa na hizo savings au uwekezaji wako?
ubinafsi uliojaa na kujifikiria mwenyewe basi, mtu hawezi kupanda hata mti ambao utaleta tija kwake au kwa watoto wake miaka 20 ijayo kwa kuwa hana uhakika kuwa atakuwepo ukamfaidisha yeye
waafrica tutazidi kukaribisha wawekezaji wa kichina na kihindi kuja kuwekeza hata kwenye vitu vidogo kama supermakets, visima vya maji, kilimo cha mboga kwa sababu ya attitude kama hii, vision fupi sana, dah hii inasikitisha.
Mkuu nadhani hujaelewa maana ya huu uzi....mimi nilipoanza kazi nilikuwa nalipwa 400,000, kodi ya pango nilikuwa nalipa 50,000, halafu matumizi mengine niikuwa natumia 100,000 hivyo 250,000 nikawa na save, nilipofikisha savings ya 2,000,000 nikawekeza kwenye mradi uliokuwa unanipa 100,000 kwa mwezi,
nikaendelea kuwekeza hadi sasa bado nimeajiriwa lakini zaidi ya nusu ya kipato changu kinatoka kwenye kwenye miradi yangu na nimeajiri ndugu zangu wawili, ikitokea nimeshindwana na waajiri wangu au kampuni ime fail kutokana na utumbuaji majipu na uchumi haueleweki unaelekea wapi mimi bado nipo secured
sasa ningefuata hii kanuni ya kujiachia maisha matamu ya mtoa mada ningekuwa naishi kwa wasiwasi sana
Hivyo alivyochambua huyo jamaa hapo juu ndiyo mantiki nzima ya mada yangu......kuna mtu ambaye hali ana utapia mlo au anatembelea matambara na ana kipato kikubwa? huyo atakuwa chizi, ila wapo wenye kipato kikubwa ambao huvaa modest na kula kawaida ambayo hayo sio maisha matamu anayomaanisha mtoa mada
mkuu kipato always huwa hakitoshi,huo mfano wangu hapo juu "nilifanya hiyo amount initoshe" maana ningeweza pewa hata milioni 5 na isinitoshe kwa matumizi yangu ya mwezi,Mkuu nadhani hujaelewa maana ya huu uzi....
Kwa mfano wewe umesema kwenye mshahara wako ulikuwa unalipia pango kwa shilingi 50,000/= na mahitaji mengine ya msingi 100,000 maana yake ni kwamba hiyo hela hapo juu ilikuwa inakutosha kwa mahitaji yako ya mwezi mzima....na ndio maana ikabaki nyingine ambayo umeifanyia mambo ya maana......
Mzizi wa mada hii sio watu kuishi maisha ya kujiachia au kuishi maisha ya anasa.....la hasha bali ni kuhakikisha kwanza pato lako linakidhi mahitaji yako alafu ile inayobaki ndio unaitunza na kuifanyia mipango ya baadae.......
Kwenye dini ya kikristo kwa mfano, watu wanahimizwa na Biblia kujiwekea akiba Mbinguni kwa ajili ya wakati ujao...!!! "Lakini jiwekeeni hazina mbinguni, mahali ambapo nondo na kutu haviharibu, wala wevi hawavunji na kuiba." (Matthew 6:20)Maada nzuri sana na yenye kuleta changamoto, ila kwa uelewa wangu, imekaa KIDINI sana, kuna maneno mengi sana Dini zetu zinatuaminisha kutoisumbukia kesho.
Ila kwa watu wa Uchumi, waliobobea huko, ukiwaeleza hayo juu hapo, mtakesha kubishana kama siyo kueleweshana.
Na ndiyo maana unasikia Serikali ama Taasisi fulani ama Mtu binafsi, wanatenga bajeti ya miaka mitano ama 30 baadaye huko kimaendeleo, na hiyo kinadharia ni KESHO.
'Rejea Bajeti inayochambuliwa Dodoma huko.'
Ahsante!