KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 18,896
- 36,213
Habari za wakati huu wapendwa....bila ya shaka sote tuwazima wa afya....na wale wapendwa wetu ambao afya zao zina mushkeli tuzidi kuwaombea kwa muumba na wao awajaalie afya njema ili waufurahie ulimwengu na kuutukuza ufalme wake.....
Kila mmoja wetu yupo kwenye mahangaiko na pirika pirika....ni mahangaiko ambayo ni muhimu kwa maisha yetu sote ya sasa na ya baadae.....
Kila siku asubuhi jua likichomoza kila anaelekea anapo pajua yeye mwenyewe kwa ajili ya kujitafutiw mkate wake wa kila siku....
Ni jambo zuri na la kheri kwa kuwa iliandikwa kuwa watu watakula kwa jasho na ndio maana watu hawatulii katika pirika pirika kila kukicha kwa ajili kutoa jasho ili wapate kula au ridhki.....
Lakini kikubwa kinachowafanya wanadamu wa nyakati wanaishi kwa wasi wasi na hofu nyingi ni kuhusu mustakabali wa KESHO....
Si kuwa kesho atakaporudi kwa muumba wake bali ni kesho katika siku zake usoni....
Wapo watu leo wamegawa kipato chao na kujinyima kwa ajili ya kujiwekea akiba ya KESHO.....
Wapo watu wanalazimika kuvaa mavazi yaliyochakaa kwa ajili ya kuokoa fedha kwa ajili ya matumizi ya KESHO.....
Wapo watu wanalazimika kula robo ya mchele ili kilo itakayobakia imfae kesho....
Lakini cha ajabu sasa hiyo kesho haina mwisho maana kila kesho inazaliwa kesho mpya...kwa hiyo ni muendelezo wa KESHO KESHO KESHO KESHO......
Si jambo baya kujiwekea akiba...lakini ni jambo baya uwekaji huo wa akiba ukaathiri matumizi yako na mahitaji yako ya leo....jitosheleze leo...jishibishe leo....kata kiu leo....kwani siku yako ni kila iitwayo leo na sio kesho...kwani hiyo hata huyo aliyeandika kalenda hakuwahi kuiona KESHO.......
Muendelezo wa mapambano ya kuipigania kesho kunamfanya mwanadamu asiyafurahie maisha mpaka anaaga dunia........anaihangaikia kesho ambayo hajawahi hata kuiona na hana hata asilimia moa ya uhakika wa kuiona kesho......
Kesho inakuwa kesho kweli mpaka itakapo timia kesho kwani wote tunafika kesho kwa neema tu na wala sio kwa ujanja ujanja wetu.....
Maisha yako ni leo.....uhai wako unao leo....ishi leo.....furahia leo.....tabasamu leo....
Kama umetamani suruali nzuri na leo hela unayo nunua....kwani unaweza ukaiona kesho na ukatamani kuvaa hiyo suruali na huku ukiwa na hela lakini bahati mbaya kesho imekufika ukiwa hauna tena miguu...
Kama umeipenda saa nzuri na hela unayo...nunua tu ndugu yangu...maana unaweza ukafka kesho ukatamani kuvaa saa lakini ukawa hauna mikono.....
Kwa kifupi hakuna mwenye kuifahamu kesho zaidi ya muumba pekee......
Wapo watu waliopambania kesho kwa kuhifadhi kila walichoona kitawafaa kesho lakini kwa kudra za muumba kesho hiyo imewakuta wakiwa hoi vitandani wakiwa wagonjwa.....na hata hawakitamani hicho walicho kihifadhi kwa ajili ya kesho.......
Ndugu umetamani jambo fulani inaweza kuwa chakula kizuri mahali pazuri....au nguo nzuri au jambo lolote lile litakalo kufanya uyafurahie maisha na uwezo wa kufanya hivyo unao leo basi wewe lifanye tu kwani huwezi jua kuwa kesho yako itakuwaje......
Wapo watu walionunua mapea ya viatu mengi kwa ajili ya kuwafaa kesho lakini kesho ikawakuta hawana miguu....
NB; Sipingani na suala mtu kujiwekea akiba lakini kwanza kidhi mahitaji yako ya leo....