Over expectations ndio sumu ya Gn'z

Over expectations ndio sumu ya Gn'z

Joined
Jul 28, 2026
Posts
51
Reaction score
108
Over expectations ndio sumu ya kisasa. Unajitarajia maisha yawe hivi, mtu akupende hivi, pesa ije hivi - ikitokea tofauti, mwili wako ndio unateseka. Stress, usingizi kupotea, presha.

Mimi huwa naona hivi:

Expectations zikizidi, furaha inapungua.

Ukitaka 100 na ukapata 70, utalia. Lakini kama hukutarajia chochote na ukapata 70, utashangilia sana.

Sio kwamba usiwe na ndoto. Ndoto ni sawa. Lakini usifunge furaha yako kwenye matokeo ya kesho. Furaha iwekwe kwenye leo.

live the moment. Chai ya leo inyonye vizuri, usifikirie chai ya kesho haipo. Mazungumzo na mtu wa leo yafurahie, usijali kama kesho hatakuwepo.

Watu wengi hawaumizwi na maisha yenyewe, wanaumizwa na picha ya maisha waliyoitengeneza kichwani.
 
Back
Top Bottom