Kwanini unga wa ngano haupikiwi ugali?

Ukiuchanganya na dona unapata ugali flani mtamuuu.
Jamani hivi mnavyosema ni kweli au mnatuuzia chai?


Nakumbuka nikiwa nyumbani niliwahi kupiga uji wa unga wa ngano, nilikuwa naelekea kusonga ugali, nikaambiwa niumwage.
 
Habari!

Naomba kujua kwa nini unga wa ngano hua haupikwi ugali kama unga mwingine wa muhogo, mahindi nk.
Jibu ni rahisi mkuu nunua kilo moja ya unga wa ngano chukua sufuria lenye maji bandika jikoni anza kupika ugali kwa kutumia huo unga wa ngano utapata jibu sahihi
 
Jamani hivi mnavyosema ni kweli au mnatuuzia chai?


Nakumbuka nikiwa nyumbani niliwahi kupiga uji wa unga wa ngano, nilikuwa naelekea kusonga ugali, nikaambiwa niumwage.
Ninachokwambia ni kweli kabisa, usiukoroge uji tho!
Uji koroga wa dona kama kawaida ila wakati wa kusonga ugali, changanya ngano(isokobolewa) na dona, inakuwa kama umeweka unga wa muhogo.

Ni mtamuuuuu.
 
Unapika Mimi nimewahi kula nilipokuwa sumbawanga ila inakuwa ni ile ngano isiyokoborewa
 
Mahindi na ngano ukisaga pamoja.ni bonge LA unga.alaf ugali wake mtamu balaaaa.alafu unaongeza nguvu za kiume.
 
Mimi na changanya ngano, mtama mweupe,mahindi ya njano na unga wa muhogo kisha nasaga,da fully Lishe hautaji mboga,ukikoroga uji wake hauna haja ya sukari na mwili unakuwa na fully nguvu.
 
Mmenikumbusha pindi nasoma nilienda kupima unga
Bahati mbaya yule mwana mama akanipimia ngano
Wakati huo niliacha maji yanachemka
Nilipofika tu nikachota nikaweka mmh yani nilistuka kuona rangi
Nikahisi huenda huu unga wa mahindi kuna udaga ulikuwemo
Nilisonga lakini naona haueleweki ikabidi nimuite rafiki yangu
Kuja akaanza kushika unga akasema aise hii ni ngano
Ilibidi tuumwage ila ulikuwa ugali tu nilihofia kula huenda ukafunga haja
uliposema udaga ...umenikumbusha mbali kinyama..n....
 
Back
Top Bottom