Kwanini unashindwa kujiamini?

Kwanini unashindwa kujiamini?

Joined
May 20, 2019
Posts
6
Reaction score
5
je unajiamini?
kwanini ninasfhindwa kufanya vizuri?
habari zenu ndugu zangu
nataka kuweka wazi kitu hiki ili kiweze kuwa na manufaa kwangu,kwako na wengine.

je unajiamini?
jiulize mwenyewe unajiamini kama unaweza kufaulu
au unajiamini kama unaweza kufanikiwa katika maisha
unajiamini kama biashara unayo ifanya itakutoa kimaisha
unajiamini kama wewe unanguvu za kumpinga adui yako?
hili ni jambo muhimu sana kuamini kama wewe ndio kiongozi wa maisha yako na hakuna mwingine wakuja kukufanya wewe uwe bora kama wewe hujiamini kama unaweza.
wengi tumeshikwa na uoga wa kutojiamini.kwa sababu majirani,rafiki,wazazi,na watu wakaribu wanatufanya tushindwe kujiamini. ni kutokana na maneno yao kama vile.
wewe huwezi kufanya hili.
kule kuzoea kusikia kama mimi siwezi kufanya kitu chochote
kuna haribu ule mfumo wako wa nguvu na kukufanya ujione ni dhaifu.
pindi unapo amini kuwa unaweza unafufua nguvu ndani ya mwili wako na kuufanya mwili uwe na nguvu ya kutosha ya wewe kuweza kufanya vizuri katika kila jambo ufanyalo.
jenga picha ndani ya akili ya kuwa wewe ni mshindi mara zote.
jisemeshe mwenyewe kimoyo moyo
"mimi naweza kufanya biashara"
"mimi si shindwi "
yaseme maneno hayo ya kujiona wewe unaweza mara kwa mara huku ukimuomba mwenyezi mungu akuwezeshe utafanikiwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.
imeletwa kwenu na MWL.Jafary Mahugi
 
Back
Top Bottom