Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,480
- 5,506
Leo nataka nigusie eneo tata na ambalo ni moja kati ya kitu kinatamkwa sana na vijana na watu wengine wanapotaka kufanya Biashara nalo ni ukosefu wa MTAJI.
Mtaji ni nini? Ni uwekezaji wa mmiliki katika biashara yake,yaani ni kile ambacho wewe mmiliki wa biashara unaingiza katika biashara yako,inaweza kuwa ni gari yako binafsi,nyumba yako, muda wako, akili yako, nguvu zako au vyote kwa pamoja. Katika zama hizi za utandawazi hata elimu na maarifa yako ni uwekezaji tosha katika biashara yako.Ili nieleweke vizuri ngoja nitoe mfano rahisi wa hili andiko langu.
Kuandaa hili andiko kumenihtaji mimi kufikiria kwa kina,kisha nikachukua muda kuandika na kisha nikapost hapa kwenye platform ya JF.Mimi sina PHD katika hili ninaloandika ila nina ufahamu wa kutosha wa kuweza kukuongoza wewe na kukushauri kidogo kuhusu uelekeo wa biashara. Iwapo utasoma andiko hili na kufikiri kwamba mimi naweza kufanya kazi na wewe basi utakuwa umekuwa mteja wangu katika biashara yangu.Ila uwekezaji wangu niliotumia ni muda na bundle,na akili kidgo ili kukuletea taarifa hii fupi tuijadili.
Mtaji sio mkopo, Mkopo katika biashara ni ni Liability yaani ni deni ambalo biashara inapaswa kulipa. Mtaji unatakiwa utoke kwa mmiliki, sisemi kwamba huwezi kukopa kuanzisha biashara hapana ila nasema kwamba unapokopa kuanzisha biashara yule mkopeshaji ndo mmiliki mpaka umalize kulipa deni, wewe utakuwa unamsaidia kusimamia tu.
Kwa kawaida hakuna biashata ambayo inaanzishwa bila mtaji,yaani lazima kuwe na input ili uweze kuwa na outpu. Sasa wengi huwa tunafikiri input lazima iwe ni pesa kumbe wakati mwingine kinachohitajika ni muda na akili basi. Chukulia mfano wa madalali wa nyumba na viwanja, wengi wao mtaji ni muda wao na mguu wao maisha yanaenda.
Leo nataka tujadili kwa uhalisia Je nini kifanyike ili kushughulika na hili tatizo la watu ama kukosa mitaji au kufikiri kwamba hawana mitaji?
Karibu tujadili