Kwanini unaogopa kifo?

Kwanini unaogopa kifo?

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
53,092
Reaction score
53,568
Tupeane sababu hasa zinazokufanya uogope kifo [endapo unaogopa]. Na kama huogopi, unaweza kutoa sababu pia.

Binafsi siogopi kabisa kifo sababu kubwa ni kwamba, ni lazima nitakufa tu. Hakuna haja ya kuogopa. Nina ndugu, jamaa na marafiki wengi nimewazika. Naumia siku ya kwanza ila ndani ya muda nasahau. Kwahiyo, nimeshaona kifo ni kitu cha kawaida sana.

Iwe leo au kesho au hata mwakani ila najua ipo siku itatokea. Ila swali linakuja, je ni kifo cha aina gani? Je, wewe unaogopa kifo? Kama ndio, kwanini? Kama sio, kwanini?
 
naogopa kufa nikifikiria unachimbiwa chini na mchanga juu hmmm...inatisha. halafu pia naogopa kama nitakuja kufa halafu niache watu ambao wananitegemea uwepo wangu...nahisi kama watapata shida...kila siku naomba Mungu kama nitakufa basi nisiache mtu ambaye ananitegemea niache watu ambao wako tayari kujiangalia wenyewe hata kama nikiwa siko
 
Umejiandaa na hiyo hali? Ya kuacha wategemezi wajetegemee wenyewe?
 
Umejiandaa na hiyo hali? Ya kuacha wategemezi wajetegemee wenyewe?
nadhani hiyo hali ikifika kila mtu anakuwa yuko tayari kwa kujiandaa nayo tatizo muda na mazingira...binafsi sina mtu ananitegemea kwa sasa lakini katika akili yangu hiko kitu kipo...
 
Natamani tungekuwa tuna kufa mara mbil.
Ukifa mara ya kwanza inakuwa kama onyo,ukishindwa kujirekebisha na kufa mara ya pili ndio iwe nitolee mazima.
 
Natamani tungekuwa tuna kufa mara mbil.
Ukifa mara ya kwanza inakuwa kama onyo,ukishindwa kujirekebisha na kufa mara ya pili ndio iwe nitolee mazima.
Au kuwe na levels mbalimbali.
Ukifa dunia hii, unazaliwa dunia nyingine kama hii katika hali hii.
Hii process inaendelea milele.
 
Natamani tungekuwa tuna kufa mara mbil.
Ukifa mara ya kwanza inakuwa kama onyo,ukishindwa kujirekebisha na kufa mara ya pili ndio iwe nitolee mazima.
Kwa hiyo kama ukijirekebisha maisha yaendelee milele baada ya kurudi mara ya pili???
 
me sikiogopi kifo ila nakichukia coz naona kinanikatisha maisha so sitajua nini kinaendelea duniani hasa kuhusu sayansi,binadamu tumefikia wapi n.k
 
Siogopi kufa ila naogopa kutangulia!

Kama kufa tutakufa ni suala la mda tu!
 
Kifo mi nakiogopa kusema ukweli,kwasababu napenda kula starehe za dunia mwanzo mwisho mpaka pale nitakapo zeeka sana,ila mambo ya kufa bado kijana sitaki hata kusikia.
 
Back
Top Bottom