Kwanini unaniacha wakati nakuhitaji?

Kwanini unaniacha wakati nakuhitaji?

mahirtwahir huachi unyonge kakangu!
Miaka nenda rudi.
Pole maskin!
Ila huyu mke kuna namna unamuacha akuendeshe mno, haya sio mapenzi aiseeh.
Mana umemkosea nn hapo, unless hujasema vyote.
Ila hapana,
Hebu Kaza kidogo, ila ndo huwezagi maskini!
Mi hata sijui nikusaidieje.
 
Kwa haya machache niliyosoma kama ni kweli ulichoandika, unatakiwa uwe Mwanaume ili huyo mwanamke ajue kaolewa na Mwanaume na sio kuwa baba wa hao watoto. Una Akili ndogo mno!
 
Pole, ilishawahi kunitokea, mke kaondoka na mtoto kurudi kwao, niliongea na mama yake akajifanya kama haelewi kinachoendelea ...niliwalamba block wote nikabadilisha na vitasa vya mlango na nyumbani kwetu nikawaambia wasiniite kwenye kikao chochote, hata ada ya mtoto sikutuma miezi mitatu alihangaika kuja kuniomba msamaha, hawa viumbe uiwaendekeza utapigwa drama ujute kuzaliwa
 
Unajua mara nyingine sisi wanaume huwa hatuongei ukweli,cha muhimu mpiganie mke wako umludishe, hakuna thamani kubwa kama mke aliyekuzalia watoto, mengine yanasameheka tu
 
Kapata mwanaume mwingine huyo mm Ilishanitokea na kwa kua mchezo mzima Nilishapewa kutoka kwa rafik yake sikuumiza kichwa kabisa .
 
Mimi siku zote humsamehe ila yeye hufutuka, kuna siku alilalamika hana nguo nikamuambia nitakununulia mwisho wa mwezi kwani hali ya maisha sio sawa akalalamika nikamuambia mbona mambo yalipokuwa safi ulikua husemi nakununulia basi alisema nimemsumbulia na akavhukuq nguo zote nilizomnunuliq na kuzipeleka kwa mama angu kwangu lilikuq tusi kubwa ila nilimsamehe
Huyo sio mke, ongea na moyo wako kwamba ulikosea, nenda kwao kiume mwambie umekubali matokeo ila utakuwa unahudumia wanao na utakuwa responsible muda wote, then mtakie kila la heri then chapa lapa, kaa mwezi mmoja ukiona hajakutafuta tena tafuta mwanamke mwingine, safari hii utumie kichwa cha juu umpate mke mwenye akili. Kheri ya mwaka mpya!!!!
 
Hata mm sipati la kukushauri maana inaonekana ni mpole haswa au umekaliwa
watoto wawili bado anakusumbua
cha kufanya
  • Kanunue madira mawili ya kina mama kubwa hasa
  • nunua nguao za ndani kufuki km 3 oversize
  • sidiria hivyo hivyo
iaelekea umepanga nyumba yenye wapangaji wengi haya km kuna mmoja mwanamke, sasa fanya hivi asubuhi zifue na uanike kwenye kamba ya jumla, halafu urudi usiku sana uzianue siku ya pili hivyo hivyo anika aina nyingine na kufuli zake usiku uanua na km hawazioni kabanie dira mojja kwenye mlango nusu nje nusu ndani chumbani
Wambeya watampa taarifa km hakuja mbio siku hiyohiyo
NAKUPA SIKU 3 tangu apate ujumbe huo
URUDISHE JIBU HAPA JAMVINI mm naweka wekundu
 
Habari Waungwana
Najuwa wapo watakaonibeza na kunidharau ila haya yalionikuta usiombe yakufike yasikie tuu kwa mwenzako maana mzigo wa mwenzako ni polo la usufi.

Naamini hakuna mahusiano ambayo hayana Changamoto ila mengine Kiboko siku ya 30/12/2020 nimeachwa na mke wangu bila ya sababu ya msingi na kuondoka na watoto wangu 2 ambao mmoja yuko na miaka 5 na mwengine ni miaka 2. Kwa hakika ni kuwa hakuna kosa la msingi tulipishana na lugha tuuu akanuna kwa siku 3 nikimpigia simu asubuhi hapokei na mimi nilikua safarini basi na mimi kama hakupokea simu humtumia sms na kumpigia tena siku itayofuata asubuhi.

Baada ya siku tatu nilisikia kutoka kwa ndugu wa familia kuwa mke wako anakunja vyombo nikajibu sawa ila baada ya muda alinitumia sms kuwa siku inayofuata atondoka na mimi sikujibu, akanipigia simu akaniuliza hivi "kesho mimi naondoka mchana unataka nikuachie kitu gani chako nisikichukue" na mimi nikamjibu " niachie wanangu tuuu " akasema kuwa hatowaacha siku iliyofuata nilifunga safari kurudi nyumbani saa 10 za jioni nilimkuta ameshavaa yeye na watoto kwa ajili ya safari nikamuita ndani na kumuliza kwa nini unaondoka akajibu kuwa nimemtolea jeuri nikamuambia basi yaishe akagoma na akaondoka na wanangu. Ndani amekunja nguo zake zote na za wanawe, chumbani kaacha vyombo tuuu kasema atakuja kufuata siku nyengine.

Naomba ushauri wenu kwa hakika bado namuhitaji hasa siwezi kuwa mbali na wanangu, wengine wanasema nimpotezee tuuu na watoto wakikua watanitafuta ila moyo wangu haukubali, nimesema nimpelekee chakula maana kwao sio safi sana wengine wanasema nisimpelekee ili ajifunze maisha kwa hakika niko njiia panda usiku umekua mkubwa nipeni mawazo.

Natanguliza shukrani
We lete dem nyumban kwako majiran wakiona wata mwambia mkeo na lazima mkeo atakuja

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Mpaka mke kuondoka, kuna issue kubwa sana umeifanya..ni vile tu umeandika hapa story ya upande mmoja.
 
Pole sana,
Nimepata shauku kubwa sana ya kukushauri kwa hichi unacho kipitia kwa sasa,
Iko hivi:
Calm your mind(tuliza akili yako kwanza) usifanye maamuzi yeyote kwa sasa mpka utakapopata angalau utulivu wa kiakili, itakusaidia kufanya chaguzi bora,
Kama ka-amua kuondoka mwache aende, cha kuzingatia mwambie asinyime mawasiliano yako na watoto,
Huyo ni wako chance ya kuolewa na mtu mwingine ni ndogo sana, chance ya kurudi baada ya hasira zake kuisha ni kubwa sana,
Funga kinywa chako uepuke maongezi yatakayo chochea ugomvi kama una wish arudi kwake,
Usi-ache kuwahudumia wote watatu.
 
Mwanamke mwenye mtoto anaondoka anaenda wapi, Huko anatest maji tu, mkuu jaribu kuangalia kama umepunguza upendo kwa wife wako au kuna namna unamsumbua jirekebishe alafu MPE muda tu huko alipo watamchoka , mwache kidogo ajifunze dunia ilivyo kuna mambo huwa wanaona in rahisi rahisi sababu kuna mwanaume wa kushugulikia wewe tulia tu atarudisha majeshi huyo

Huu ndio ushauri unao faa kufanyiwa kazi kwa hatua za Awali.!
Katika yote Pole sana kwako mtoa maada .! Changamoto tumeumbiwa wanadamu pambana
 
Basi Acha nikupe Hali halisi.

It seems sasa hivi hapo home maisha yameyumba kidogo... Ambayo ni kawaida na hasa kwa mwaka huu.

Sasa inabidi ujikaze kiume hata kama unampenda for the sake of the kids. Ukimuendekeza kuwa anaondoka Kila mara watakaoteseka Ni wanao sababu itawakosti Hadi shule.

So nakushauri ujikaze. Kata mawasiliano na yeye. Usimpigie, usimtext, mkaushie. Hela ya matumizi mtumie then kausha. Uchune kabisa. Akikupigia pokea lakini make it short na kuhusu watoto tu. Then kata na akipiga usipokee tena.

Kwao usiende eti kumfata arudi. Acha akae akili atarudi mwenyewe. Bahati nzuri watoto bado wadogo.

Mwanamke ganii unataka kumnyanyansa mumeo kisa ameyumba kimaisha. Uchukue nguo alizokununulia kweli umpelekee Mamake mzazi? With no shame at all? Sio sahihi.

Man Up ndugu! For the sake of your kids. Weka mapenzi pembeni.
Umenena mkuu, mimi wangu nae alifanya hivyo hivyo yapata miaka nane imepita.
Nilichomsihi ni kuniruhusu aniachie watoto 2 ambao tulikuwa nao. Namshukuru Mungu nimewalea toka wakiwa wadogo, na sasa wamekua.
Nasikia alipata jamaa mwingine na amepata mtoto pia.
Sasa naona kila wakati huwa ananipigia simu na kuandika msg lakini mimi kwangu sihitaji tena ukaribu nae kwani tayari ni mke wa mwingine na nisije kuwa chanzo cha mgogoro katika mahusiano yao.
 
Back
Top Bottom