Kwanini unaniacha wakati nakuhitaji?

Kwanini unaniacha wakati nakuhitaji?

All the best. Mlipoambiwa kuishi na sisi kwa akili Ni kwa sababu Muumba wetu anatujua

Kweli dada yangu nashkuru kwa kujua wakati ninaoupitia, kwa sasa mtoto wangu yuko nasar anaingia nasari 2 mwaka huuu kaenda nae kwao inabidi amtafutie shule
 
Kweli dada angu nashkuru kwa kujua wakati ninaoupitia kwa sasa mtoto wangu yuko nasar anaingia nasari 2 mwaka huuu kaenda nae kwao inabidi amtafutie shule
Wewe jifanye hayo yote huyajui. Anajua kabisa unajali na utamfata na ndio maana kakulia timing anajua shule zinafunguliwa. Wewe kausha. Tena ikiwezekana hata simu usipokee tuma mahitaji tu. Akikupigia Ma Mkwe pokea ongea nae fresh akikuuliza mwambie huwezi mfata sababu hujamfukuza na hata hivyo umeona amuache apumzike kwao.
 
Habari Waungwana
Najuwa apo watakaonibeza na kunidharau ila haya yalionikuta usiombe yakufike yasikie tuu kwa mwenzako maana mzigo wa mmwenzako ni polo la usufi.

Naamini hakuna mahusiano ambayo hayana Changamoto ila mengine Kiboko siku ya 30/12/2020 nimeachwa na mke wangu bila ya sababu ya msingi na kuondoka na watotot wangu 2 ambao mmoja yuko na miaka 5 na mwengine ni miaka 2 kwa hakika ni kua hakuna kosa la msingi tulipishana nalugha tuuu akanuna kwa siku 3 nikimpigia simu asubuhi hapokei na mimi nilikua safarini basi na mimi kama hakupokea simu humtumia sms na kumpigia tena siku itayoffuta asubuhi baada ya siku tatu nilisikia kutoka kwa ndugu wa familia kua mke wako anakunja vyombo nikajibu sawa ila baada ya muda alinitumia sms kua siku inayofuata atondoka na mimi sikujibu akanipigia simu akaniuliza hivi "kesho mimi naondoka mchana unataka nikuachie kitu gani chako nisikichukuwe" na mimi nikamjibu " niachie wanangu tuuu " akasea kua hatowaacha siku iliofuata nilifunga safari kurudi nyumbani saa 10 za jioni nilimkuta ameshavaa yeye na watoto kwa ajili ya safari nikamuita ndani na kumuliza kwa nini unaondoka akajibu kua nimemtolea jeuri nikamuambia basi yaishe akagoma na akaondoka na wanangu.
ndani amekunja nguo zake zote na za wanawe chumbani kawacha vvyombo tuuu kasema atakuja kufuata siku nyengine.

naomba ushauri wenu kwa hakika bado namuhitaji hasa siwezi kua mbali na wanangu wengine wanasema nimpotezee tuuu na watoto wakikua watanitafuta ila moyo wangu haukubali nimesema nimpelekee chakula maana kwao sio safi sana wengine wanasema nisimpelekee ili ajifunze maisha kwa hakika niko njiia panda usiku umekua mkubwa nipeni mawazo

natanguliza shukrani
Pole sana ndugu haya mambo yapo hata Mimi yalinikuta, nilikua na mke wangu na mtoto mmoja nilimpenda sana mke wangu ila ndio akaondoka.. Nachoshukuru mtoto hakuondoka nae ndio imebaki faraja yangu.
 
Ni mke wangu wa ndoa tena halali kabisa
Sawa. Cha kwanza. Shirikisha familiyako ili papatikane kikao cha pamoja kisha yatajulikana mbichi na mbivu. Kama kikao hakijafua dafu. Basi Unitafute pm ntamrudisha kwa uwezo wa mwenyezimgu. ila kunifwata pm ni lazma umefanya jitahidi zote kimeshidikana. Ndo ntakupitisha ktk njia mbadala.
Kunya maji ya sukari na uchibe vizuri. Pengine ni chamrachamra za mwaka mpya
 
Pole sana ndugu yangu najua maumivu na ghalika la moyo, unapitia kipindi kigumu sana mimi yaliwahi kunikuta, niliwashirikisha ndugu zake lakini walikuwa pamoja nae hasa kaka wa mke wangu. Ushauri wangu kwako kama familia ulikooa wana hofu ya Mungu, swala lenu ni dogo sana...ila kama hawana dini (hofu ya mungu umekwisha)sasa fanya hivi mbembeleze mkeo na msihi naimani atajirudi mtakuwa wote.
 
Basi Acha nikupe Hali halisi.

It seems sasa hivi hapo home maisha yameyumba kidogo... Ambayo ni kawaida na hasa kwa mwaka huu.

Sasa inabidi ujikaze kiume hata Kama unampenda for the sake of the kids. Ukimuendekeza kuwa anaondoka Kila Mara watakaoteseka Ni wanao sababu itawakosti Hadi shule.

So nakushauri ujikaze. Kata mawasiliano na yeye. Usimpigie, usimtext, mkaushie. Hela ya matumizi mtumie then kausha. Uchune kabisa. Akikupigia pokea lakini make it short na kuhusu watoto tu. Then kata na akipiga usipokee tena.

Kwao usiende eti kumfata arudi. Acha akae akili atarudi mwenyewe. Bahati nzuri watoto bado wadogo.

Mwanamke ganii unataka kumnyayansa mumeo kisa ameyumba kimaisha. Uchukue nguo alizokununulia kweli umpelekee Mamake mzazi? With no shame at all? Sio sahihi.

Man Up ndugu! For the sake of your kids. Weka mapenzi pembeni.
Hapa ndio umeshamaliza kila kitu, lazima achukue ushauri huu full stop!!
 
Kaka nimekuelew vizuri sana nitajaribu kiongozi
Usiiambie nafsi eti utajaribu, please fanya, hii si kwa wanao tu bali pia hata kwako itakufanya u relax lasivyo ukiendelea kuweka mapenzi mbele utakufa bro, kama siyo basi ugonjwa wa DYSANIA utakunyemelea kisha ushindwe kufanya mambo ya KIUCHUMI, be strong enough !!
 
Wewe jifanye hayo yote huyajui. Anajua kabisa unajali na utamfata na ndo maana kakulia timing anajua shule zinafunguliwa. Wewe kausha. Tena ikiwezekana hata simu usipokee tuma mahitaji tu. Akikupigia Ma Mkwe pokea ongea nae fresh akikuuliza mwambie huwezi mfata sababu hujamfukuza na hata hivyo umeona amuache apumzike kwao.
Point
 
Mama Mariam aliwahi kumletea upuuzi wa namna hii mumewe, kwakuwa baba Mariam alimpenda sana mkewe akawa anambembeleza weeeee anatulia kidogo analipuka tena

Kila akileta ujinga wake ilikuwa lazima aombe nauli ya kweda kwao. Basi siku tukamkalisha baba Mariam tukampa somo, jirani yetu huyu mwanamke atakusumbua sana kwakuwa anajua unampenda sana hivyo kwa vyovyote vile ni lazima utampigia magoti

Cha kufanya siku moja akikuzingua jiondoe ufahamu, akikuomba nauli mpe aende na akishaondoka kata mawasiliano naye kabisa badala yake tuma hela ya matumizi kwa mama mkwe kwaajili ya watoto na umsisitize mkweo kwamba mke wangu asirudi huku kwangu hadi nitakapomfuata mimi mwenyewe.

Aiseee baba Mariam alipozinguliwa kaombwa nauli katoa mke akaondoka na watoto wawili. Mama Mariam alikaa kwao miezi nane hadi aliomba msamaha. Tukamshauri baba Mariam amwache amalize mwaka kabisa ndio aende kuwafuata.

Siku ya kwenda alipiga simu kwa mama mkwe kwamba nipo njiani nakuja kuifuata familia yangu. Anakwambia alipofika pale woooooote kimyaaa hakuna aliyediriki kuuliza swali. Akamwambia mke wake kama yupo tayari kurejea nyumbani au bado anataka aendelee kubaki na wazazi wake, mama Mariam alijibu twende nyumbani mume wangu. Asubuhi na mapema wakawahi bus wakarejea nyumbani. Baada ya kufika nyumbani mama Mariam alimuomba radhi mumewe kwa tabia aliyokuwa nayo ya kumsumbua mara kwa mara na aliahidi kuiacha na kukua (kuacha utoto).

Baada ya hapo hakuwahi kusumbua tena na heshima ikaongezeka baina yao
 
Wewe ni muislam ?If Yes mwambie unaoa wife no 2.Uone atasemaje.
Kama wewe ni mkristo basi piga kimya kimya. Mtumie pesa za matumizi tu,ukipiga simu ni kusalimia wanao tu.Atarudi mwenyewe.
Wewe jifanye hayo yote huyajui. Anajua kabisa unajali na utamfata na ndo maana kakulia timing anajua shule zinafunguliwa. Wewe kausha. Tena ikiwezekana hata simu usipokee tuma mahitaji tu. Akikupigia Ma Mkwe pokea ongea nae fresh akikuuliza mwambie huwezi mfata sababu hujamfukuza na hata hivyo umeona amuache apumzike kwao.
Safi sana naona hata ninyi hamjakubaliana na alichofanya mwenzenu.
 
Pambana Mkuu usikubali kupoteza ndoa yako na watoto kirahisi rahisi hivyo. Kutofautina lugha kwa mume na mke si kitu cha ajabu lakini haiwi chanzo cha kufunga virago ili kuivunja ndoa hasa ukitilia maana ni bado unampenda mkeo na kutaka kuendelea na ndoa yenu. Huyo anatingisha kibiriti ili kuona kina unazidi upi. Tuhabarishe kinachoendelea
Sema mkuu mwanamke wa hivi ni pasua kichwa.
Ukishamfuata kwao na kubembeleza akarudi, ataitumia hiyo kama silaha. Kitu kidogo tu atakua anatishia kuondoka. Jamaa atachoka at some point.
 
Basi Acha nikupe Hali halisi.

It seems sasa hivi hapo home maisha yameyumba kidogo... Ambayo ni kawaida na hasa kwa mwaka huu.

Sasa inabidi ujikaze kiume hata Kama unampenda for the sake of the kids. Ukimuendekeza kuwa anaondoka Kila Mara watakaoteseka Ni wanao sababu itawakosti Hadi shule.

So nakushauri ujikaze. Kata mawasiliano na yeye. Usimpigie, usimtext, mkaushie. Hela ya matumizi mtumie then kausha. Uchune kabisa. Akikupigia pokea lakini make it short na kuhusu watoto tu. Then kata na akipiga usipokee tena.

Kwao usiende eti kumfata arudi. Acha akae akili atarudi mwenyewe. Bahati nzuri watoto bado wadogo.

Mwanamke ganii unataka kumnyayansa mumeo kisa ameyumba kimaisha. Uchukue nguo alizokununulia kweli umpelekee Mamake mzazi? With no shame at all? Sio sahihi.

Man Up ndugu! For the sake of your kids. Weka mapenzi pembeni.
ukifata maelezo haya... hamalizi siku 30 anarudi mwenyewe kwa magoti
 
Jaribu kukausha mkuu jikaze kiume ndani ya mwezi mmoja atarudi mwenyewe na siku nyingine usiombe msamaha kwa kila kosa.
 
Pambana Mkuu usikubali kupoteza ndoa yako na watoto kirahisi rahisi hivyo. Kutofautina lugha kwa mume na mke si kitu cha ajabu lakini haiwi chanzo cha kufunga virago ili kuivunja ndoa hasa ukitilia maana ni bado unampenda mkeo na kutaka kuendelea na ndoa yenu. Huyo anatingisha kibiriti ili kuona kina unazidi upi. Tuhabarishe kinachoendelea
Kweli kabisa, kama hakuna usaliti wa kutisha ni muhimu apiganie ndoa yake...

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ni kweli nampenda nampenda sana ila watoto nawapenda zaidi iua mbali na wtoto ndio shida nimezoya nikiingia hapa baba baba leo nyumba iko kimya kama kaburi hebu vaaa kiatu changu useme kama ni ww ungefanyaje
Anajua madhaifu yako.....
Swali ushawahi kumchapa hata kofi? Sidhani
Wanawake hawapendi kind men.... pale ulipo ingia ndani ukamkuta anakunja nguo ungemchapa kofi kwanza hahaaaaa
 
Back
Top Bottom