Kwanini unaniacha wakati nakuhitaji?

Nina imani kuwa huyo mwanamke ana akili timamu na wazo la kuondoka kwako ni lake yeye mwenyewe. Ninahisi atakuwa kapata mtu wa kumchezea akili na hisia zake huko aendako....jamaa akimchoka na kumsaliti baada ya kumla atarudi kwako huku akilia. Njaa mbaya wewe usisiskie...mara nyingi wanawake wenyewe ndiyo huharibu ndoa zao kwa ajili ya tamaa ya shilling 1000 tu ya mshikaki na muhogo wa kuchoma.
 
Brother c kwamba una mapenzi na wanao tu hapana unampenda mkeo sana, ila mapenzi uliyonayo hayo yatakuua. Ningekuwa mimi hata matumizi ya watoto nisingetoa bila yeye kuniomba, ningemlia kimya nikafunga Vioo kabisa, na anayemuharibu ni Shost yake mama yake.

Hukupeleka mahari kwa mama yake bali ulipeleka kwa baba. Mimi hata kwa mama mkwe nisingekanyaga. Since ushamwambia baba usithubutu kupiga simu au sms hizo zinakuchora. Siku ya kikao chenu usikubali kifanyikie kwa mama kifanyikie kwa baba basi. Ukimkazia huyu atakuheshimu ila usipomkazia utakuwa shamba boy kwako
 

Asante nitaufanyia kazi ushauri wako asante
 
Huyo mwache aende mbona atarudi mwenyewe tu
 
Baba na mama yake wameshatengana, wewe ni nani hata usitengwe!
 
Halafu acha lugha ya ubinafsi kwa watoto, kila kitu watoto wangu watoto wangu... ni watoto 'wenu' sio watoto wako.
 

Unamshauri ujinga, huwezi kuishi kwa kujilamba kwa mama mkwe namna hiyo... hiyo si sawa.
 
Unamshauri ujinga, huwezi kuishi kwa kujilamba kwa mama mkwe namna hiyo... hiyo si sawa.

Mkuu kwenye ushauri tofauti tofauti ndipo mtu unachagua ushauri unaokidhi hitaji lako.

Kumbuka hapa tunatoa ushauri bila kuwa na taarifa za pande zote, hivyo tutakuwa tunajitahidi kutafuta suluhu.

Halafu nikupe ushauri, jifunze jinsi ya ku-address kitu kilicho tofauti na mawazo yako kiustaarabu, haikupunguzii kitu.
 
Kama ni mtu wa Dodoma aisee achana naye narudia tena achana naye utaumiza kichwa mwili muda utapoteza Ila hatarudi nikuashauri Tu fanya kama unapotezea wanao wataletwa Ila mwanamke hutampata na hakupendi jua hilo Tu hakupendi utapambana utashindwa ni ayo Tu pole sana
 
Hivi wanaume wengine mko Sawa kweli, vipi mama yake akifariki mtu kama hajui umuhimu wa ndoa haezi kubadilika na ushauri Tu ukiona mwanamke kalelewa Sana na mama yake muogope kama ukoma amuweke mama karibu kwani kamuowa yeye apo hapendwi aangakie ustaarabu mwingine maisha mengine tunajipa stress Tu alafu tumamsingizia Muumba wakati akili tumepewa za kuchanganua
 
Huyu mwanamke ana gubu, hana subira, hana hekima wala hana busara..... Nakushangaa unavyolialia kuhusu mtu wa namna hii
 
Asipozingatia haya mtoa mada atakuwa zumbukuku ulimwengu upo huku
 
Pole Sana, kwa kipindi hiki, usimfuatilie, huenda ikawa bado ana hasira na wewe au pengine kuna mtu anampotosha, jipe hata miezi 3, kuhusu watoto, usiwe na shaka, watakula na watavaa vizuri tu, naamini kabla ya mkeo kufanya hayo maamuzi, alikwishajipanga na huenda kuna mfadhili, MUNGU akutie nguvu kwakuwa ni mambo yanayoumiza Sana.
 
Tuliza akili, jifanye umepotezea, kimya hata mwaka mzima - atajileta na kuomba msamaha. Najua utaumia hasa watoto wako ila jipe moyo.
 
Daah niseme wewe umeolewa kimwili na kiakili yaani kama ni zobe au zombi una viwango. Hongera sana kwa mahaba niue
 
Kuna maswali mawili ya msingi inabidi ujiulize na ujijibu kwa uwazi

Je umemkosea sana au kawaida? Kama umemkosea sana basi shuka mbembeleze hata kwa kutumia mtu anayemuheshimu

ILA nasema tena ILA kama ameondoka kwa sababu ya kawaida na kibr ndani yake ni bora aondoke moja kwa moja kuliko wewe kujishusha maana kwa kujishusha kwako uta prove udhaifu ambao ndo itakuwa mwanzo wa kupoteza heshima yako kama mwanaume...

Mwanaume msimamo. Na msimamo ni kitu kidogo ukikiangalia but trust me ni muhimu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…