Kwanini unaniacha wakati nakuhitaji?

Kwanini unaniacha wakati nakuhitaji?

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
614
Reaction score
322
Habari Waungwana

Najuwa wapo watakaonibeza na kunidharau ila haya yalionikuta usiombe yakufike yasikie tuu kwa mwenzako maana mzigo wa mwenzako ni polo la usufi.

Naamini hakuna mahusiano ambayo hayana Changamoto ila mengine Kiboko siku ya 30/12/2020 nimeachwa na mke wangu bila ya sababu ya msingi na kuondoka na watoto wangu 2 ambao mmoja yuko na miaka 5 na mwengine ni miaka 2. Kwa hakika ni kuwa hakuna kosa la msingi tulipishana na lugha tuuu akanuna kwa siku 3 nikimpigia simu asubuhi hapokei na mimi nilikua safarini basi na mimi kama hakupokea simu humtumia sms na kumpigia tena siku itayofuata asubuhi.

Baada ya siku tatu nilisikia kutoka kwa ndugu wa familia kuwa mke wako anakunja vyombo nikajibu sawa ila baada ya muda alinitumia sms kuwa siku inayofuata atondoka na mimi sikujibu, akanipigia simu akaniuliza hivi "kesho mimi naondoka mchana unataka nikuachie kitu gani chako nisikichukue" na mimi nikamjibu " niachie wanangu tuuu " akasema kuwa hatowaacha siku iliyofuata nilifunga safari kurudi nyumbani saa 10 za jioni nilimkuta ameshavaa yeye na watoto kwa ajili ya safari nikamuita ndani na kumuliza kwa nini unaondoka akajibu kuwa nimemtolea jeuri nikamuambia basi yaishe akagoma na akaondoka na wanangu. Ndani amekunja nguo zake zote na za wanawe, chumbani kaacha vyombo tuuu kasema atakuja kufuata siku nyengine.

Naomba ushauri wenu kwa hakika bado namuhitaji hasa siwezi kuwa mbali na wanangu, wengine wanasema nimpotezee tuuu na watoto wakikua watanitafuta ila moyo wangu haukubali, nimesema nimpelekee chakula maana kwao sio safi sana wengine wanasema nisimpelekee ili ajifunze maisha kwa hakika niko njiia panda usiku umekua mkubwa nipeni mawazo.

Natanguliza shukrani
 
Kwa ulivyoandika hapo ni kwamba anakwenda kwao, ayway uzuri kwao unapaju fany kuwashirikisha watu wakubwa wenye kuheshimika kisha uitishe kikao msuluhishe.

Baba ma mama yake wameshatengana yeye kaenda kwa mama, nimeshamueleza baba yake ila naona kanambia atashughulikia ila kimya na mama niko na mashaka kuwa yuko shauri moja na mwanawe unajua wasichana kwa mama zao.
 
Pambana Mkuu usikubali kupoteza ndoa yako na watoto kirahisi rahisi hivyo. Kutofautina lugha kwa mume na mke si kitu cha ajabu lakini haiwi chanzo cha kufunga virago ili kuivunja ndoa hasa ukitilia maana ni bado unampenda mkeo na kutaka kuendelea na ndoa yenu. Huyo anatingisha kibiriti ili kuona kina unazidi upi. Tuhabarishe kinachoendelea
 
Baba ma mama yake wameshatengana yeye kaenda kwa mama nimeshamueleza baba yake ila naona kanambia atashuhulikia ila kimya na mama niko na mashaka kua yuko shauri moja na mwanawe unajua wasichana kwa mama zai

Huu ndiyo msingi mkuu wa tatizo.
 
Pambana Mkuu usikubali kupoteza ndoa yako na watoto kirahisi rahisi hivyo. Kutofautina lugha kwa mume na mke si kitu cha ajabu lakini haiwi chanzo cha kufunga virago ili kuivunja ndoa hasa ukitilia maana ni bado unampenda mkeo na kutaka kuendelea na ndoa yenu. Huyo anatingisha kibiriti ili kuona kina unazidi upi. Tuhabarishe kinachoendelea

Mimi siku zote humsamehe ila yeye hufutuka, kuna siku alilalamika hana nguo nikamuambia nitakununulia mwisho wa mwezi kwani hali ya maisha sio sawa akalalamika nikamuambia mbona mambo yalipokuwa safi ulikua husemi nakununulia basi alisema nimemsumbulia na akavhukuq nguo zote nilizomnunuliq na kuzipeleka kwa mama angu kwangu lilikuq tusi kubwa ila nilimsamehe
 
Nakubali ndio nikawa sina pa kushika wala pakishtaki wazeee hawaelewani ma nahofu tukitengana dhambi kama hii atakujaipata mwanangu si wazee wasema mtoto hufuata kichogo cha mlezi wake

Naogopa kuandika ninachowaza, ila jaribu kuchunguza ukaribu wake na mama yake. Au anashauriwa nini na mama.

Kiafya siyo mzuri kwa ndoa yenu.
 
Mimi siku zote humsamehe ila yeye hufutuka kuna siku alilalamika hana nguo nikamuambia nitakununulia mwisho wa mwezi kwani hali ya maisha sio sawa akalalamika nikamuambia mbona mambo yalipokua safi ulikua husemi nakununulia basi alisema nimemsumbulia na akavhukuq nguo zote nilizomnunuliq na kuzipeleka kwa mama angu kwangu lilikuq tusi kubwa ila nilimsamehe
Kwa hiki ulichoandika hii inamaanisha kuna mengi hujayaandika pia mkeo siyo rational.

Anajua unampenda.

Anajua utaenda kumsaka.

Anajua saa hii utakua unalia.

Ungekua kaka yangu ningekuambia kuwa mwanaume achana naye ila wewe sikujui so nakushauri sikiliza moyo wako endelea kumlilia hivyo hivyo.
 
Naogopa kuandika ninachowaza, ila jaribu kuchunguza ukaribu wake na mama yake. Au anashauriwa nini na mama.

Kiafya siyo mzuri kwa ndoa yenu.

Ukweli awali mama alikua hataki nimuowe ilifikia kumsusa ila baada ya kumuowa mke wangu alikua na bifu na mama yake ila mimi nikaona isiweshida nikafanya jitihada za kumuambia yule ni mama ake asimdharau nikamuelekeza basi wakawa si mama na mwaa ni kama marafiki maaana walikua karibu sana basi kumbe mama akiambiwa dogo la kwangu anamubia si nilikukataza na wife anaweka moyoni
 
Mwanamke mwenye mtoto anaondoka anaenda wapi, Huko anatest maji tu, mkuu jaribu kuangalia kama umepunguza upendo kwa wife wako au kuna namna unamsumbua jirekebishe alafu MPE muda tu huko alipo watamchoka , mwache kidogo ajifunze dunia ilivyo kuna mambo huwa wanaona in rahisi rahisi sababu kuna mwanaume wa kushugulikia wewe tulia tu atarudisha majeshi huyo
 
Kwa hiki ulichoandika hii inamaanisha kuna mengi hujayaandika pia mkeo siyo rational.

Anajua unampenda.

Anajua utaenda kumsaka.

Anajua saa hii utakua unalia.

Ungekua kaka yangu ningekuambia kua mwanaume achana naye ila wewe sikujui so nakushauri sikiliza moyo wako endelea kumlilia hivyo hivyo.

Ni kweli nampenda sana ila watoto nawapenda zaidi iua mbali na wtoto ndio shida nimezoya nikiingia hapa baba baba leo nyumba iko kimya kama kaburi hebu vaaa kiatu changu useme kama ni wewe ungefanyaje
 
Mwanamke mwenye mtoto anaondoja anaenda wapi Hugo anatest maji tu, mkuu jaribu kuangalia kama umepunguza upendo kwa wife wako au kuna namna unamsumbua jilekebishe alafu MPE muda tu huko alipo watamchoka , mwache kidogo ajifunze dunia ilivyo kuna mambo huwa wanaona in rahisi rahisi sababu kuna mwanaume wakushugulikia we we tulia tu atarudisha majeshi huyo

Asante mkuuu nitajitahidi kusema na moyo wangu ila mioyo ikisahauliana ni vigumu kurudisha penzi la kweli
 
Back
Top Bottom