Kwanini unaishi Dar es salaam?

Kwanini unaishi Dar es salaam?

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
5,165
Reaction score
8,959
Dar ni sehemu yenye raha nyingi kama kulivyo na karaha nyingi pia. Japo kwangu nikipima naona karaha ndio zimezidi.

Ni kawaida sana kukuta misururu ya foleni ya watu wakigombea usafiri tena unakuta ni mida mibovu kabisa. watu wanalundikwa kwenye daladala na mwendokasi utadhani ni bidhaa. hata km una usafiri binafsi foleni ni kila kona.

Ukitaka kuwahi sehemu ili uwahi asbh kwa mfano hospitali bac hakikisha unaamka mapema sana tena ikiwezekana saa nane uko au tisa usiku.

Hali ya usafi mitaani mitaa michafu, vyoo vya paspoti na kuwekwa mapipa chini, , mapusha na wateja wao wa madawa ya kulevya, wadangaji, chemba zilizowazi zinazochangia hewa chafu ni changamoto na kero zingine lundo. Licha ya haya yote kuna mtu humtoi nje Dar!

Sasa ndugu yangu wew nini hasa kinachokufanya ung'ang'anie kuishi mahali yenye karaha hivyo.

Mnaongangania kuishi huko niwajulishe tu nje ya Dar kuna maisha pia. Tena maisha ya stress kabisa na kila kitu kinaenda sawa.
 
Mnaitamani sana Dar eeeh.
Nyuzi kibao msimu huu ni Dar Dar Dar

Mbona haiko hivyo mnavyoisema vibaya, foleni sio kila sehemu, uswazi pia sio kila sehemu.
Labda mwenyeji wako ndo anaishi uswazi mno ndio maana ukaondoka na picha mbaya kuhusu Dar.
 
Dar es salaam ni kama mikoa mingine tu, uzuri wa daslam hata ukiuza karanga zinatoka, sasa hapo Dodoma unamuuzia nani karanga? mbeya utaitegemea biashara ya karanga? si utakuwa mgonjwa, lakini daslam hizo karanga zimeongezewa thamani zinauzika na ni biashara kubwa tu.

Daslam Kuna magodown mengi kiasi kwamba kama una nguvu zako za kubeba mizigo hela hukosi na watu wameboresha maisha kwa njia hiyo, ukizungumzia changamoto kila sehemu kuna changamoto, huko mikoani ni kweli hakuna foleni lakini barabara ni mbovu kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine, ni safari ya siku nzima, mfano tu kutoka Morogoro mjini kwenda wilaya ya Ulanga/Mahenge ni shughuli pevu, wakat hapa kutoka Ilala kwenda kinondoni unatembea kwa mguu

Mzunguko wa hela daslam ni mkubwa mno, yaani mtu kukupa msimbazi sio issue kubwa, mkoani mtu atakupa msimbazi kizembe bila kumtaarifu siku tatu kabla?
 
Dar es salaam ni kama mikoa mingine tu, uzuri wa daslam hata ukiuza karanga zinatoka, sasa hapo Dodoma unamuuzia nani karanga? mbeya utaitegemea biashara ya karanga? si utakuwa mgonjwa, lakini daslam hizo karanga zimeongezewa thamani zinauzika na ni biashara kubwa tu.

Daslam Kuna magodown mengi kiasi kwamba kama una nguvu zako za kubeba mizigo hela hukosi na watu wameboresha maisha kwa njia hiyo, ukizungumzia changamoto kila sehemu kuna changamoto, huko mikoani ni kweli hakuna foleni lakini barabara ni mbovu kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine, ni safari ya siku nzima, mfano tu kutoka Morogoro mjini kwenda wilaya ya Ulanga/Mahenge ni shughuli pevu, wakat hapa kutoka Ilala kwenda kibindoni unatembea kwa mguu

Mzunguko wa hela daslam ni mkubwa mno, yaani mtu kukupa msimbazi sio issue kubwa, mkoani mtu atakupa msimbazi kizembe bila kumtaarifu siku tatu kabla?
Au ukauze maji kilimanjaro, utajuta.
 
Dar ni sehemu yenye raha nyingi kama kulivyo na karaha nyingi pia. Japo kwangu nikipima naona karaha ndio zimezidi.

Ni kawaida sana kukuta misururu ya foleni ya watu wakigombea usafiri tena unakuta ni mida mibovu kabisa. watu wanalundikwa kwenye daladala na mwendokasi utadhani ni bidhaa. hata km una usafiri binafsi foleni ni kila kona.

Ukitaka kuwahi sehemu ili uwahi asbh kwa mfano hospitali bac hakikisha unaamka mapema sana tena ikiwezekana saa nane uko au tisa usiku.

Hali ya usafi mitaani mitaa michafu, vyoo vya paspoti na kuwekwa mapipa chini, , mapusha na wateja wao wa madawa ya kulevya, wadangaji, chemba zilizowazi zinazochangia hewa chafu ni changamoto na kero zingine lundo. Licha ya haya yote kuna mtu humtoi nje Dar!

Sasa ndugu yangu wew nini hasa kinachokufanya ung'ang'anie kuishi mahali yenye karaha hivyo.

Mnaongangania kuishi huko niwajulishe tu nje ya Dar kuna maisha pia. Tena maisha ya stress kabisa na kila kitu kinaenda sawa.
Nita print hii niisambaze maana kuna watu kama wamefungwa kamba huko Dar, maisha magumu na hawatoki!
 
Mi mwenzenu nikisafiri toka Dar kwenda mkoa mwingine mwili unaniwasha kama nimemwagiwa upupu.. Nikianza safari ile kufika hapo Kibaha tu muwasho unaanza .. Mwaka jana nilikuwa Kanda ya ziwa kwa miezi miwili nimerudi Dar Nina ukurutu mwili mzima.. Bora nijikalie Dar tu kuepuka mateso..
 
Back
Top Bottom