Dar ni sehemu yenye raha nyingi kama kulivyo na karaha nyingi pia. Japo kwangu nikipima naona karaha ndio zimezidi.
Ni kawaida sana kukuta misururu ya foleni ya watu wakigombea usafiri tena unakuta ni mida mibovu kabisa. watu wanalundikwa kwenye daladala na mwendokasi utadhani ni bidhaa. hata km una usafiri binafsi foleni ni kila kona.
Ukitaka kuwahi sehemu ili uwahi asbh kwa mfano hospitali bac hakikisha unaamka mapema sana tena ikiwezekana saa nane uko au tisa usiku.
Hali ya usafi mitaani mitaa michafu, vyoo vya paspoti na kuwekwa mapipa chini, , mapusha na wateja wao wa madawa ya kulevya, wadangaji, chemba zilizowazi zinazochangia hewa chafu ni changamoto na kero zingine lundo. Licha ya haya yote kuna mtu humtoi nje Dar!
Sasa ndugu yangu wew nini hasa kinachokufanya ung'ang'anie kuishi mahali yenye karaha hivyo.
Mnaongangania kuishi huko niwajulishe tu nje ya Dar kuna maisha pia. Tena maisha ya

stress kabisa na kila kitu kinaenda sawa.