Kwanini umueleze shoga mambo yako ya ndani?

NIMPENDENANI

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
6,114
5,388
Habari za leo waungwana,

Kuna vitu nashindwa kuelewa naomba muongozo hasa kutoka kwa wanawake wenzangu,naomba nitoe sababu yakutaka muongozo, kuna mdada hapa kazini ana report kwangu ni mdada wa mjini kiasi hua anapenda sana kueleza mambo yake ya nyumbani ,kila anachofanya akija lazima awambie wenzie,akigombana na mumewe,akifanya mapenzi,akipewa kitu yani hana kifua chaku nyamaza.

Weekend walienda na shoga zake Bagamoyo wakachukua na waume zao wakawa huko kuanzia Friday mpaka Sunday wakarejea, sasa leo amekuja kazini nasikia wanatukanana matusi ya nguoni na shoga yake mwanamke utakua usojua kumridhisha mumeo mie kwanza nilijua utani nikampigia simu mmoja wapo nikamwambia pole pole kelele zinafika mpaka huku,sijakaa hata dakika 10 nasikia watu wanakimbia jikoni kuna nini wanapigana mtu na shogake.

Kisa anamuelezea matatizo yake kumbe yeye ndio sababau ya matatizo,amekuta sms,na hata walipokua huko Bagamoyo yule mdada alochukua mume wawatu alisahau make up kit kwenye gari ya jamaa,yani nimarefu kaongea mpaka BP imepanda.

Niwasihi wanawake wenzangu na nafsi yangu kama una neno lako mweleze mama yako au ndugu yako,huu ushoga wa makopa wakukutania pakachani hapana.
 
Ni kwel wamekosea kuyaleta nje. Kwa bahat mbaya sana na ww umeyaleta huku nje. Tena kama yalivo
 
Ni kwel wamekosea kuyaleta nje. Kwa bahat mbaya sana na ww umeyaleta huku nje. Tena kama yalivo
kuyaleta nikuwapa wanawake wenzangu elimu kua sio vizuri kuleta mambo yenu ya ndani kumuelezea mtu sikuleta kwa ubaya..nna imani wapo watakao soma nakupata japo 1 kwenye hili..naomba uelewe...
 
Kwa maana ingine wameibiana mabwana siyo?
huyu mdada anaeongea amechukuliwa mumewe na kosa ni lake la kusema sijui ananifanya hivi,mara leo kataka
asubuhi subuhi mara jana speed ilipungua,mara anauliza nani unamjua anadawa ya kuongeza maubile,mara hodari wa kuzama chumvini yani promo kibao,sasa amelipa thamani kubwa...mpaka namuonea huruma..
 
I see...Vry bad na iwe funzo hata kwa wanaume wale wanaopenda kusifisifia mautundu ya wanawake zao kwa mabest zao...Huwa kuna watu hawaridhiki hadi nayeye ahakikishe mwenyewe sasa hapo ndo balaa huanzia..
 
Back
Top Bottom