Kwanini umauti unaleta heshima kuliko uhai?

wolverineGG

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2025
Posts
1,970
Reaction score
3,682
Salaam.
Nimejiuliza hili swali kwa muda mrefu na hua nakosa majibu. Huu ukiritimba tumeukuta na hatujawahi jiuliza kwanini tunauendeleza mpaka leo.

unaweza ukakuta jitu lilikua la hovyo sana mtaani, lakini baada ya kufa tu watu wanamheshimu saana. Na wanasoma historia ya marehem as if hajawahi kufanya baya lolote.

Kwamba inamaanisha kifo ni ukombozi au ni namna gani.. maana jamii zetu za kiAfrika zimepashikilia hapa mpaka sio poa. Watu inafaka mahali wanaheshimu kabuli la mama kuliko baba alie hai.
 
Jamii zetu zimekaa kinafki sana ,ila pamoja na hilo sio jambo la busara kuanika madhaifu ya marehemu kwenye kadamnasi ili hali kila mtu anayake ya sirini ya hovyo tu.
Kuna watu wanataka marehemu aorodheshewe tabia zake na zitajwe kwa sauti hadharani k.m wizi,uzinzi,ugonjwa halisi uliomtwaa,gubu,ugomvi,ulafi,uvivu,msengenyaji,mfitini,mnunaji maarufu, ushoga,usenge-baridi,uvuta bangi,ulevi,mdoweaji,shankupe,ushangingi,utapeli n.k.
 
Ibada ya mazishi ni heshima kwa sababu ni sherehe ya mwisho (hitimisho) la mtu hapa duniani ! Ndio maana kila mtu anaheshimu na kuhuzunika kwa pamoja ,, ukiwa msibani unapata utulivu wa kipekee na reflection ya maisha halisi ya hapa duniani !

Wacha ;
Majivuno
Kiburi
Ukatili
Mauwaji
Uzulumati
Usaliti
Dhambi n.k

Maisha ni mafupi sana, enjoy your moment ungali na nguvu, siku uking'ata shuka watu wako pamoja na machawa waliokuwa wanakusifia wataogopa hata kuisogelea maiti yako,,, Pesa na mali ulizoacha hutozikwa nazo, waliobaki watatumbua wawezavyo !

Mzee mmoja aliniusia, sio maneno yangu !
 
Haka ni kaunafiki fulani hivi
Salaam.
Nimejiuliza hili swali kwa muda mrefu na hua nakosa majibu. Huu ukiritimba tumeukuta na hatujawahi jiuliza kwanini tunauendeleza mpaka leo.

unaweza ukakuta jitu lilikua la hovyo sana mtaani, lakini baada ya kufa tu watu wanamheshimu saana. Na wanasoma historia ya marehem as if hajawahi kufanya baya lolote.

Kwamba inamaanisha kifo ni ukombozi au ni namna gani.. maana jamii zetu za kiAfrika zimepashikilia hapa mpaka sio poa. Watu inafaka mahali wanaheshimu kabuli la mama kuliko baba alie hai.
 
Jamii zetu zimekaa kinafki sana ,ila pamoja na hilo sio jambo la busara kuanika madhaifu ya marehemu kwenye kadamnasi ili hali kila mtu anayake ya sirini ya hovyo tu.
hilo ndo swali langu. kwanini akiwa hai mnamuita malaya, mwizi n.k. lakini akifa mnaacha? hiyo busara ni yanini sasa? mnachagua mzoga kuupa thamani kuliko mtu hai. mnanipa ukakasi sana
 
Salaam.
Nimejiuliza hili swali kwa muda mrefu na hua nakosa majibu. Huu ukiritimba tumeukuta na hatujawahi jiuliza kwanini tunauendeleza mpaka leo.

unaweza ukakuta jitu lilikua la hovyo sana mtaani, lakini baada ya kufa tu watu wanamheshimu saana. Na wanasoma historia ya marehem as if hajawahi kufanya baya lolote.

Kwamba inamaanisha kifo ni ukombozi au ni namna gani.. maana jamii zetu za kiAfrika zimepashikilia hapa mpaka sio poa. Watu inafaka mahali wanaheshimu kabuli la mama kuliko baba alie hai.
Hata linapokuja suala la michango, Maiti hupata hela nyingi kuliko mgonjwa.
 
hilo ndo swali langu. kwanini akiwa hai mnamuita malaya, mwizi n.k. lakini akifa mnaacha? hiyo busara ni yanini sasa? mnachagua mzoga kuupa thamani kuliko mtu hai. mnanipa ukakasi sana
Marehemu alisimangwa alipokuwa mzima.Kuanza kumsema wakati hasikii wala hawezi kujirudi na kufanya masahihisho ni kupotezea muda wazikaji.Watu wanakuwa moto wanataka kuwahi "kunawa mikono" msiba ulipo.
 
hayo mazuri ndo anayasikia? tena mnatunga mengine ambayo hayapo, hamuoni bado mnappteza muda wa "kunaw mikono" msiba ulipo?
 
Kijijini kwetu huwa tunamremba marehemu ili mke au mume,watoto na jamaa wengine wasihuzunike.Mkiwaudhi wafiwa mtakuwa hamnawi mikono yenu.Mtaagana makaburini.
 
Sifa za mtu zutajwe kama zilivyo na unafiki uachwe mara Moja.
Mtu akiwa fasadi hata akifa kwenye msiba wake basi aendelee kuitwa fisadi.

Naomba tusimame katika ukweli bila kupindusha mambo bila kujalisha tuko sehemu gani.
 
Back
Top Bottom