Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,010
Nilikuwa na mjadala na rafiki yangu mmoja siku chache zilizopita kuhusiana na tabia ambayo miaka hiyo ya 47 tulikuwa hatuchukulii kwa namna yoyote mbaya na ambayo bado inaendelea kwa namna moja au nyingine. Kulikuwa na tabia kwamba ukiwa na GF wakati ule wa shule basi alikuwa anakutegemea kwa matumizi madogomadogo.
Hivyo, akija kwako alikuwa anatarajia kuwa ataondoka na "chochote" na kwa kweli "mkikutana" bila "kupeana" chochote ilikuwa ni kama jambo lisilo la kawaida. Hii tabia iliendelea lakini ilikuwa ni tofauti kwa wale ambao walikuwa kama kwenye boarding schools ambapo hela zilikuwa zinakuja kwa mgao toka kwa familia kama mgao wa Tanesco. Huko boarding school mtu na gf wake walikuwa wanategemeana mmoja akipata chochote basi mwingine naye alikuwa ananeemeka.
Lakini katika mazingira ambayo wote mlikuwa bado mnaishi kwa wazazi au mahali ambapo kijana alikuwa au ana kazi bora kidogo bado kuna matarajio kuwa fedha inatolewa. Hapa tukumbuke sizungumzii watu wazima au watu wenye ajira zao ambao wanakubali kuchunwa au watu ambao kutokana na mapenzi kati yao wanasaidiana hapa na pale kwa kadiri ya uwezo wao. Ninazungumzia mapenzi yale ya gf na bf wakati wa shule hasa wakati wa Msingi au hata Sekondari.
Hoja ambayo ilisababisha kuwa na mjadala mkali kati yangu na rafiki yangu huyo ni kuwa mmoja wetu alikuwa na maoni kuwa tulikuwa tunawaprostitutisha magf wetu kwani tulikuwa tunawapa fedha baada ya kitendo na wao walikuwa wanategemea kupata fedha baada ya kitendo. Tena wakati mwingine hata bila ya kitendo kuna watu walitarajiwa kutoa kitu kidogo kwa binti ambaye bado anaishi na wazazi wake.
Cha kushangaza tukakumbushana kisa ambacho binti alitegemewa na wazazi wake kujitegemea kimapato - kutoka kwa bf wake kiasi kwamba walianza kumnyima fedha za matumizi ya hapa na pale huku wakimsukumiza "kwani huyo bf wako hana hela?" walimuambia.
Nikakumbuka kisa cha yule binti ambaye hakutaka kwenda kumuomba bf wake hela kwa sababu walikorofishana na wazazi wake walimkasirikia kwa sababu kina alikuwa anasaidia hadi pale nyumbani na wakamlazimisha binti kwenda kuomba msamaha ilimradi kijana asikate msaada.
Ukikumbuka mazingira kama haya unachukuliaje tabia hiyo kuwa ni sehemu ya utamaduni wa mapenzi au ni kitu ambacho kinahitaji kuwekwa kwenye maudhui yake - yaani siyo jambo baya kwa kipimo chochote.