Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Ninyi endeleeni tu kutokwenda kanisani kwa amani, hakuna anayewahukumu, japokuwa naamini hapa yenyewe nafsi zenu zinawasuta ndiyo maana mnajifanya kutafuta justification tu ya matendo yenu hamna lolote..!
Ajabu na wewe huwenda hujaenda
 
Ulitaka uhubiriwe nini mtoa mada? Hayo unayotaka kuhubiriwa una uhakika utayafuata? Ukiambiwa mpende jirani yako kama nafsi yako utafanya hivyo? Ukiambiwa uache wivu, masengenyo, uzinzi n.k utaacha?
@Khantwe hili si ndio lengo kuu la kuanzisha kanisa...linapaswa lipewe msisitizo zaidi kuliko mengine. Mambo muhimu hayazungumzwi ila ya sadaka yanazungumzwa tena kwa ukali.
 
Dahhhh.....
Ila kwetu michango imezidi mnoooo.....
1. Zaka
2.Sadaka
3. Mavuno
4. Utoto mtakatifu
5. Ujenzi wa nyumba ya Paroko
6. Ukarabati wa kanisa
7. Mfuko wa parokia
8. Wageni wa kanisa
9. Viti vya jumuiya
Kanisa linajengwa na wewe, mimi na yule........

Usichoke kutolea...
 
Huyajui ndio maana unalialia hapa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],,, "Zaka na sadaka ni mali ya bwana"....au ule unaosema "Leteni zaka kamili ghalani ili kiwepo chakula cha kutosha nyumbani kwa Bwana"....hii mistari imetumika mara nyingi mpaka siwezi kuisahau ile ule wa "Mpende jirani yako.... " ndio umenikumbusha leo.
 
Msipolijenga kanisa nani atalijenga ? Michango yote hiyo ni kwa ajili ya kuendesha shughuli za kanisa
Kwani zamani waliwezaje kuyamudu yote hayo kwa Zaka na Sadaka pekee..??
 
 
Kipindi fulani niliacha karibia mwaka mzima bila kwenda kanisani kisa nilisalitiwa na watu wenye nafasi nzuri kanisani tena niliowaamini ila baadae nkaelewa natakiwa kwenda kanisani kumuambudu Mungu wangu wala sio viongozi wa kanisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…