Kwanini ukimwangalia usoni aliyelala huamka?

Kwanini ukimwangalia usoni aliyelala huamka?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,888
Reaction score
831,220
Ni sayansi gani hii? Ni uchawi!? Ni mazingaombwe ama ni jambo la kufikirika tu lisilo na ukweli wowote?

Niliahidi kuleta mada hii, baada ya Dr. Shika kuchagiza kwenye simulizi yake ya kutoroka watesi wake kwamba hakumwangalia yule mtesi mlinzi aliyebaki naye machoni la sivyo jamaa angeamka!

Tujadili kipengele kwa kipengele.

A. Kwenye mada zilizopita za jicho la tatu, majinamizi na jicho la rohoni tuliona jinsi jicho la tatu lilivyo na nguvu pale macho yaonekanayo yakiwa yamefumba, yamelala.. Kumbuka jicho la tatu liko kwenye paji la uso.. Tunapozungumzia mawasiliano ya kiroho kiunganishi ni jicho hilo la tatu kwamba kuna muunganiko usioonekana kati ya jicho la tatu na jicho la tatu lingine...
Kama nilivyosema kwenye mada ya majinamizi na ndoto mbaya hatushauriwi kulala chali kwakuwa juu yetu zinapita roho nyingi na za kila aina, ambazo connection yake ni jicho hilo la tatu

B. Wachawi na wanga hutumia sana jicho la tatu kufanya mawasiliano ya kiroho na ndio maana wanapotaka kuingia ndani ya nyumba kwanza kuingia kinyume nyume kwa rivasi na wakiwa uchi... Hapa ni kuepusha uwezekano wowote wa wewe kuna na direct connection ya jicho la tatu na yeye... Akishafanikiwa kuingia ndani akakukuta umelala chali hapo hataweza kuwanga tena bali yataanza mapambano mengine ya kutaka akugeuze au kukupindua ili afanye yake... Lakini kwakuwa tayari ile connection ishakuwa established basi subconscious mind inakuwa alert na ndio mwanzo wa kukabana..
Jiulize kwanini wanaoingiliwa na popobawa hawana kipingamizi chochote, hujikuta tayari washachafuliwa..

C. Muingiliano mwingine wa jicho la tatu ni ndege kunguru mwewe, huyu ni ndege mwerevu na mwepesi sana huwezi kumpiga akiwa mbali, hivyo wajuzi huenda kinyume nyume mpaka kumkaribia kabisa ndio hugeuka na kumpelekea moto... Ukiweza kurudi rivasi kwa kunyooka, unaweza kumkaribia kunguru mpaka umbali wa mita tano.. Unaweza kufanya majaribio

D. Mwili wetu huu una mashine tatu moja ni conscious mind na nyingine ni subconscious mind na ya tatu ni unconscious mind
-conscious mind- ni hii hali tuliyo nayo ya kuweza kufanya kila kitu kwa utashi na bila utashi, kuandika kuongea kuvaa nguo nk nk, ni katika hali hii subconscious mind (jicho la tatu) nayo hufanya kazi.. Hii hufanya kazi ya ulinzi kuzunguka mwili wote na ndio maana huwa tunahisi kuna mtu anatunyemelea, kuna mtu yuko nyuma yetu ama kuna hatari inatukaribia.. Lakini vilevile hufanya kazi ya machale... Jicho la tatu huona zaidi ya kuona (seeing beyond) huwa tunapewa tahadhari na nafsi zetu, huwa tunasita kufanya jambo . hii ni kazi ya subconscious mind... Halafu kuna hali ile ya kuzirai ama kupoteza fahamu... Hii ndio unconscious mind... Macho yote mawili yamezima, jicho la tatu nalo linakuwa kwenye dormance state.. Lipo lakini utendaji hupungua uwezo mpaka kufikia chini ya asilimia 50 ili kulinda uhai kidogo uliobakia. Ni sawa na kukipunguzia mizigo chombo baharini kinachokaribia kuzama ili kisizame

Sasa tuhitimishe kwa suala la Dr Shika, aliachwa na mlinzi lakini akalala kutokana na uchovu pombe na madawa.. Lakini kwakuwa tayari ana ufahamu (inbuilt intuition) wa kumlinda Dr, hivyo hata alale vipi lile jukumu kiroho hubaki kwenye subconscious mind/jicho la tatu na ikitokea ukamwangalia usoni una establishe connection kati yako na yeye na kumfanya ashtuke na kuamka
 
mara nyingi hujikuta nikipambana sana nyakati ziwe mchana au usiku hii ina maanisha nini kwangu?
 
ninatokewa sana na hali ya mapambano na nafsi yangu hunipelekea kuwa napaa kama ndege apaavyo hii ina maanisha nini kwangu?
 
Kwanini kukiwa na hali tofauti ya giza ikininyemelea na kunipelekea kuingia kwenye mapambano kila niki kemea kwa jina la Yesu,mapambano hayo hutoweka.
 
Mara nyingi upo uhusiano mkubwa katiya fikra za mtu na matokeo ya jambo fulani.

Wakati mwingine watu huviita MALENGO,JUHUDI NA MAFANIKIO


Hongera sana Mshana kwa mada za kufikirisha,kufurahisha na kuelimisha,hakika wewe ni great thinker
 
mara nyingi hujikuta nikipambana sana nyakati ziwe mchana au usiku hii ina maanisha nini kwangu?
Hupambani wewe ni roho kupitia jicho la tatu huona visivyoonekana kwa macho ya nyama
 
Mara nyingi upo uhusiano mkubwa katiya fikra za mtu na matokeo ya jambo fulani.

Wakati mwingine watu huviita MALENGO,JUHUDI NA MAFANIKIO


Hongera sana Mshana kwa mada za kufikirisha,kufurahisha na kuelimisha,hakika wewe ni great thinker
 
Kumbe ndo maana huwa nikilala Chali, napata tabu sana, mara nkabwe koo, nipige kelele af sauti haitoki, unakuwa unatamani kuamka af huwezi,kumbe jicho la tatu bwana, Ahsante sana mshana kwa kunifungua macho.
 
Kumbe ndo maana huwa nikilala Chali, napata tabu sana, mara nkabwe koo, nipige kelele af sauti haitoki, unakuwa unatamani kuamka af huwezi,kumbe jicho la tatu bwana, Ahsante sana mshana kwa kunifungua macho.
 
Kuna uhusiano gani? Jicho kucheza na kupata habari nzuri au mbaya.
 
lkn pia Mimi nikimkazia mtu kumtazama kichogoni lazima mtu huyo ageuke hii hali husababishwa na nini? Yani huwa sipatagi tabu kuinua sauti yangu kumuita mtu, kama mtu nashida nae huwa nalenga macho yangu ktk ncha ya kichogo chake kwa umakini bila kukopea lazima mtu huyo ageuke kunitazama.
 
Ni sayansi kwamba binadamu ana zaidi ya milango mitano ya fahamu. Milango mingine ndiyo hiyo inawezesha kuhisi unatazamwa hata kama haumuangalii mtu au umelala.
 
Yaani mimi hata kama si kuamka lazima nitahisi tu kuna mtu alinisimamimia mbele yangu.
 
Nimekuelewa sana bro kuhusu hilo jicho la tatu
Mkono wangu wa kushoto ukiwasha nitapoteza pesa au kitatokea kitu kunifanya nitoe pesa ambayo itaniuma katika nafsi yangu

Na mkono wangu wa kulia ukiwasha napata pesa

Nahisi hapo ndio jicho la tatu linatangulia kuona
 
Back
Top Bottom