ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,681
- Thread starter
- #21
Yes kuna haja ya kutoa elimu ya namna ya kuvijua vyama vya Ukawa.
Ni kweli, lakini je muda wa kufanya hivyo kikamilifu upo?
Yes kuna haja ya kutoa elimu ya namna ya kuvijua vyama vya Ukawa.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015 ushirikiano wa vyama wa UKAWA utashindwa vibaya. Hali hii ni bayana kwa wale wote wanaofuatilia hali ya kisiasa tangu CCM ilipomchagua mgombea wake mpaka hivi sasa.
Sababu kubwa itakayowafanya UKAWA washindwe vibaya ni kubalika kwa mgombe wa CCM Dk. John Pombe Magufuli na mikakati madhubuti ya CCM kuusaka ushindi. Hata hivyo kuna sababu nyingine mbili za ndani ya UKAWA wenyewe zitakazochangia kuwaangusa:
1.kushindwa kutoa ujumbe unaoeleweka
2. kushindwa kuratibu shughuli za kampeni na mahusiano ndani ya UKAWA.
Katika kufutilia Kwangu mijadala mbalimbali nimeona kuwa wanoitetea UKAWA hawana ujumbe zaidi ya kusema lengo lao ni kuitoa CCM. Kauli hii ni sawa na kusema lengo lao ni kupata madaraka tu. Kuingia madarakani bila kuwa na mkakati ni ujumbe unaoweza kukubaliwa na wafuasi kindakindaki ambao wala huna haja ya kuwaomba kura. Unapoenda kumuomba kura mtu asiye mfuasi wako ni lazima uwe na ujumbe zaidi ya kutaka madaraka. Hili litaiangusha sana UKAWA kwenye uchaguzi huu.
Kwenye kushindwa kuratibu shughuli za uchaguzi na mahusiano ndani ya UKAWA imedhihirika kuwa kila kukicha kunaibuka mgogoro mpya. Watu walioajiriwa na kampeni hawapati malipo, mgawanyo wa majimbo na kata hauheshimiwi na hakuna mkakati mmoja wa kutafuta ushindi.
Katika uratibu, kuna kosa kubwa sana la kiufundi ambalo UKAWA wanalifanya. Kuna majimbo mengi ambayo wagombea wa UKAWA zaidi ya mmoja wamerudisha fomu. Katika majimbo hayo yapo ambayo wagombea wengine wameamua kutokufanya kampeni na kumuachia mwenzao, lakini yapo pia ambayo wagombea zaidi ya mmoja wanafanya kampeni. Kutokanana sheria y uchaguzi, wagombea wote waliorudisha fomu majina yao yatakuwepo kwenye karatasi za kura. Hii itasababisha kura nyingi za wagombea wa UKAWA kuharibika na kugawanyika. Uchaguzi wa mwaka huu unaweza kuwa na kura nyingi zilizoharibika kuliko chaguzi zote katika historia ya nchi yetu.
Tafiti mbaimbali zinaonyesha watu wengi (zaidi ya asilima 40) wanategemea kuona UKAWA kwenye karatasi ya kura. Hata hivyo tafiti hizo hazielezei watu hao baada ya kutoona UKAWA, wale ambao lengo lao lilikuwa kuchagua UKAWA watafanyaje. Kwa kiasi kikubwa watu wa namna hii wataharibu kura kwa kuchagua mtu zaidi ya mmoja na wengine kuchagua wa chama chao hata kama siye aliyeachiwa nafasi ya UKAWA.
Kushindwa kwa UKAWA kwenye uchaguzi wa mwaka huu kunatokana na maandalizi hafifu na kuendeshwa na matukio. Hili ni fundisho kwa chaguzi zijazo...
Kwa mwenendo wa hali ya kisiasa ulivyo, CCM imeshashinda, ila asilimia ya ushindi ndiyo haina uhakika...
Neno au Jina Dubwana Sio lBinafsi na hili sijaficha lawama nyingi zitaenda kwa CHADEMA. Sijui ni genius gani huko aliyeamua kuingia kwenye hili dubwasha la UKAWA limevuruga sana siasa za upinzani. Kushindwa kwao watalaumu wengine wote isipokuwa wao wenyewe. Na kitu ambacho hatutakikubali ni watu hawa hawa ambao wamechukua hatua zitakazosababisha upinzani ushindwe waje tena na kusema waongoze tena harakati za mabadiliko 2020. Hili tumeshalikataa mapema.
Binafsi na hili sijaficha lawama nyingi zitaenda kwa CHADEMA. Sijui ni genius gani huko aliyeamua kuingia kwenye hili dubwasha la UKAWA limevuruga sana siasa za upinzani. Kushindwa kwao watalaumu wengine wote isipokuwa wao wenyewe. Na kitu ambacho hatutakikubali ni watu hawa hawa ambao wamechukua hatua zitakazosababisha upinzani ushindwe waje tena na kusema waongoze tena harakati za mabadiliko 2020. Hili tumeshalikataa mapema.
Mwandishi makini huhakikisha anaepuka kutumia vivumishi vyenye utata kwenye maandiko yake. Kama kuna kushindwa "vibaya" ina maana kuna "kushindwa" na kushindwa "vizuri". Usipotolea maelezo maana ya kushindwa vibaya, andiko lako linakosa maana kwa msomaji. Na ukitaka kusema kushindwa vibaya kuna maana gani, lazima ueleze imekubaliwa na nani kwamba kiwango fulani ni "vibaya" na kipi ni "vizuri"...
Kuhusu hilo la kura kuharibika, nimeshanusa mchezo wa bao la mkono kwa style ya kuharibu kura za wapinzani. Hilo itabidi lipigiwe kelele na kufanyiwa kazi...
Kupo kushindwa kubaya na kushindwa kuzuri. Kushindwa vibaya ni pale unapokuwa na nyenzo ya kushindia ukaziacha na kuzidharau ukachukua nyenzo nyingine kwa mbwembwe nyingi halafu nyenzo hizo zikakuletea matatizo badala ya mafanikio. Ukawa ilikuwa inaanza kuunda structure fulani ya utawala ndani yake. Structure ile imebomoka yote baada ya wao kukubali kuendeshwa na matukio. Huko ni kushindwa vibaya...
Sawa... next time watakuconsult...
ACT wanaonekana kuwa wasikivu zaidi. Wakiendelea hivihivi watakuwa chama kikuu cha upinzani. Chadema wataponzwa na siasa za matukio...
Amka wewe,ACT ipo funded na ccm sio wapinzani,amekuja kugawa kura za wapinzani,mbona mmelala mpaka akili zenu?
Amka wewe,ACT ipo funded na ccm sio wapinzani,amekuja kugawa kura za wapinzani,mbona mmelala mpaka akili zenu?