Kwanini UKAWA itashindwa vibaya?

Kwanini UKAWA itashindwa vibaya?

Hebu acha kuongea propaganda za mwenyekiti wenu Mbowe. Hujui kuwa Mbowe na cohorts wake ndiyo wako bize kuchafua yeyote aliyepingana naye! Mtu asipokubaliana nae basi ni msaliti!

Kwanza nilitaka kujua wewe chama gani hilo nimepata jibu hivyo haina haja kubishana na watu waliofail in more than 50 years.
 
Kwanza nilitaka kujua wewe chama gani hilo nimepata jibu hivyo haina haja kubishana na watu waliofail in more than 50 years.

Hivi kwa akili yako kila mtu ana chama? Wengine ni wana mabadiliko na tulisapoti sana harakati za Chadema asilia ila si hawa Ukawa uchwara!
Lakini hujajibu point niliyokwambia. Mbowe ni mharibifu na mbinafsi na amekiuza chama! Dawa yake iko jikoni!
 
Yaani hapo ulichosema ni kwamba wapinzani wasiaminiwe kwa vile wanatumiwa na CCM. Kauli za namna hii ndio huwa zinawafanya wananchi wasichague vyama vya upinzani. Unadhani unaichafua ACT kumbe unachafua upinzani wote.

Mkuu kuna vijana wadogo wamekuwa mashabiki mandazi wa political personalities and know nothing about principles!
 
Mkuu kuna vijana wadogo wamekuwa mashabiki mandazi wa political personalities and know nothing about principles!

Anguko la Ukawa la mwaka huu litakuwa somo la utangulizi kwa siasa za vyama vingi barani Afrika.
 
Hivi kwa akili yako kila mtu ana chama? Wengine ni wana mabadiliko na tulisapoti sana harakati za Chadema asilia ila si hawa Ukawa uchwara!
Lakini hujajibu point niliyokwambia. Mbowe ni mharibifu na mbinafsi na amekiuza chama! Dawa yake iko jikoni!

Wewe unachama tena kijani,ungekua mwanamabadiliko husingekua na idea nyembamba kiasi hicho,put astray weakness za mbowe all we need ni kufumua mfumo wa chama dola na ndio lengo la mpinzani wa kweli then baada ya hapo ndo watu watajua njia bora ya kutawala,ukikuta mtu anatetea kijani na kudai ni mpinzani huo unafiki
 
We mpare, ulisapoti slaa and you never went outside the box
 
ACT wanaonekana kuwa wasikivu zaidi. Wakiendelea hivihivi watakuwa chama kikuu cha upinzani. Chadema wataponzwa na siasa za matukio...

Litakuwa jambo zuri pia. Kwa watu ambao hatuna maslahi binafsi na chama chochote tunatamani uwepo wa upinzani wenye nguvu na uwezo wa ushindani, bila kujali unatolewa na chama kipi. Cha muhimu wawe wanafanya juhudi za kweli kujenga demokrasia na kukibana sawa sawa chama tawala.
 
Hivi kwa akili yako kila mtu ana chama? Wengine ni wana mabadiliko na tulisapoti sana harakati za Chadema asilia ila si hawa Ukawa uchwara!
Lakini hujajibu point niliyokwambia. Mbowe ni mharibifu na mbinafsi na amekiuza chama! Dawa yake iko jikoni!

Kale malimao tu, mabadiliko ni lazima mwaka huu
 
Wewe unachama tena kijani,ungekua mwanamabadiliko husingekua na idea nyembamba kiasi hicho,put astray weakness za mbowe all we need ni kufumua mfumo wa chama dola na ndio lengo la mpinzani wa kweli then baada ya hapo ndo watu watajua njia bora ya kutawala,ukikuta mtu anatetea kijani na kudai ni mpinzani huo unafiki
hivi kwa akili zako fupi unadhani ccm itatolewa kirahisi hivyo? Thubutu, mpaka aje Yesu mara ya pili labda
 
Litakuwa jambo zuri pia. Kwa watu ambao hatuna maslahi binafsi na chama chochote tunatamani uwepo wa upinzani wenye nguvu na uwezo wa ushindani, bila kujali unatolewa na chama kipi. Cha muhimu wawe wanafanya juhudi za kweli kujenga demokrasia na kukibana sawa sawa chama tawala.

I totally agree.
Wasichokijua wana Chadema/Ukawa na CCM ni kuwa, katika kundi hili tuko wengi tu ambao tungependa kuona siasa za principles na mikakati inayopimika badala ya ushabiki kama ilivyo sasa.
 
Mtaji wa siasa ni watu, mtaji huu huwa unakuwa mkubwa sana ikiwa watu hao watakuwa katika mazingira ya kufanya maamuzi kishabiki. Mara nyingi ushabiki huwa na matokeo mabaya kwenye siasa, tofauti na kwenye mipira au muziki kwani katika siasa baada ya mechi ndipo malipo ya ushabiki yanahitajika sana. Ni kupitia ushabiki ndipo umuhimu wa kampeni na kusikiliza sera unakuwa haupo kwasababu wanaotakiwa wasikilize sera, tayari washakuwa washabiki. Sera hazina maana tena.

Kwa bahati mbaya, mwaka huu uchaguzi umetawaliwa na ushabiki, kuzidi au sawa na ule wa 2005. Wanasiasa wa Tanzania wamejua kuwa Watanzania tunapenda kufanya mambo kwa kishabiki.

Kamwe tusiingie kwenye mtego wa ushabiki linapokuja suala la uchaguzi. Ushabiki tuuache majukwaa ya mpira na muziki. Hapa tuchague mtu aje atufanyie kazi tunayotaka ifanywe kwa takribani miongo kadhaa.

Inawezekana, epuka ushabiki.
 
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015 ushirikiano wa vyama wa UKAWA utashindwa vibaya. Hali hii ni bayana kwa wale wote wanaofuatilia hali ya kisiasa tangu CCM ilipomchagua mgombea wake mpaka hivi sasa.

Sababu kubwa itakayowafanya UKAWA washindwe vibaya ni kubalika kwa mgombe wa CCM Dk. John Pombe Magufuli na mikakati madhubuti ya CCM kuusaka ushindi. Hata hivyo kuna sababu nyingine mbili za ndani ya UKAWA wenyewe zitakazochangia kuwaangusa:

1.kushindwa kutoa ujumbe unaoeleweka
2. kushindwa kuratibu shughuli za kampeni na mahusiano ndani ya UKAWA.

Katika kufutilia Kwangu mijadala mbalimbali nimeona kuwa wanoitetea UKAWA hawana ujumbe zaidi ya kusema lengo lao ni kuitoa CCM. Kauli hii ni sawa na kusema lengo lao ni kupata madaraka tu. Kuingia madarakani bila kuwa na mkakati ni ujumbe unaoweza kukubaliwa na wafuasi kindakindaki ambao wala huna haja ya kuwaomba kura. Unapoenda kumuomba kura mtu asiye mfuasi wako ni lazima uwe na ujumbe zaidi ya kutaka madaraka. Hili litaiangusha sana UKAWA kwenye uchaguzi huu.

Kwenye kushindwa kuratibu shughuli za uchaguzi na mahusiano ndani ya UKAWA imedhihirika kuwa kila kukicha kunaibuka mgogoro mpya. Watu walioajiriwa na kampeni hawapati malipo, mgawanyo wa majimbo na kata hauheshimiwi na hakuna mkakati mmoja wa kutafuta ushindi.

Katika uratibu, kuna kosa kubwa sana la kiufundi ambalo UKAWA wanalifanya. Kuna majimbo mengi ambayo wagombea wa UKAWA zaidi ya mmoja wamerudisha fomu. Katika majimbo hayo yapo ambayo wagombea wengine wameamua kutokufanya kampeni na kumuachia mwenzao, lakini yapo pia ambayo wagombea zaidi ya mmoja wanafanya kampeni. Kutokanana sheria y uchaguzi, wagombea wote waliorudisha fomu majina yao yatakuwepo kwenye karatasi za kura. Hii itasababisha kura nyingi za wagombea wa UKAWA kuharibika na kugawanyika. Uchaguzi wa mwaka huu unaweza kuwa na kura nyingi zilizoharibika kuliko chaguzi zote katika historia ya nchi yetu.

Tafiti mbaimbali zinaonyesha watu wengi (zaidi ya asilima 40) wanategemea kuona UKAWA kwenye karatasi ya kura. Hata hivyo tafiti hizo hazielezei watu hao baada ya kutoona UKAWA, wale ambao lengo lao lilikuwa kuchagua UKAWA watafanyaje. Kwa kiasi kikubwa watu wa namna hii wataharibu kura kwa kuchagua mtu zaidi ya mmoja na wengine kuchagua wa chama chao hata kama siye aliyeachiwa nafasi ya UKAWA.

Kushindwa kwa UKAWA kwenye uchaguzi wa mwaka huu kunatokana na maandalizi hafifu na kuendeshwa na matukio. Hili ni fundisho kwa chaguzi zijazo...

Fikara nzuri sana. Kuongezea kwenye uliyoandika; pia tusidharau mambo mawili ambayo hayaongelewi sana:
  1. Udhalilishwaji wa Dr. Slaa, Prof. Lipumba n.k.: Wapo wengi ambao wamekatishwa tamaa na hili tendo. Kwa hiyo baadhi ya wafuasi wao sio ajabu hawatampigia kura LOWASSA na sio ajabu wakaamua hata kumpigia kura Magufuli.
  2. Wapo wana UKAWA wengi ambao hawamtaki LOWASSA: Sababu yao ni moja tu, UFISADI wake ambao wameupiga vita kwa miaka mingi. Hawa sauti zao zimenyamazishwa na wale wenye midomo mikubwa, lakini nina uhakika wapo wengi. Kwa hawa, sio ajabu wanashiriki hata kwenye mikusanyiko ya UKAWA lakini wakiulizwa na TWAWEZA, wanamchagua mtu tofauti na Lowassa.
 
Tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa kitaasisi wa chama cha mapinduzi, ulioruhusu kustawi kwa siasa za kimtandao ambazo ni matokeo ya kuwa na jamii dhaifu ya kitanzania na waliotufikisha hapa ndio sasa tunawataka.
Chalenge kwa magufuli ni namna atakavyowadhibiti wanamtandao waliobaki ndani ya chama cha mapinduzi kama atashinda ingawa sioni akifanikiwa.
Lakini chalenge kwa chadema ni namna watakavyowadhibiti friends ambao kimsingi ni very powerful
kama atashinda. Sioni namna watavyoweza
nani atashinda? Mnajua ninyi ambao bado mna matumaini na wanasiasa wa kitanzaniaas to me i dont trust them all and am not a voter.

Wengi tumekatishwa tamaa na wanasiasa wetu, ila hatuna namna na hatuna mtu wa kumzilia nchi yetu.

Ila hatutaacha kupiga kelele, japo sauti zetu zinazimwa kwa nguvu na wenye midomo mikubwa.

Naamini muda sio mrefu wataishiwa sauti, hapo ndipo tutakaposikika japo tutakuwa tumechelewa na kurudi hatua kadhaa nyuma.!
 
Mwandishi makini huhakikisha anaepuka kutumia vivumishi vyenye utata kwenye maandiko yake. Kama kuna kushindwa "vibaya" ina maana kuna "kushindwa" na kushindwa "vizuri". Usipotolea maelezo maana ya kushindwa vibaya, andiko lako linakosa maana kwa msomaji. Na ukitaka kusema kushindwa vibaya kuna maana gani, lazima ueleze imekubaliwa na nani kwamba kiwango fulani ni "vibaya" na kipi ni "vizuri"...

Kuhusu hilo la kura kuharibika, nimeshanusa mchezo wa bao la mkono kwa style ya kuharibu kura za wapinzani. Hilo itabidi lipigiwe kelele na kufanyiwa kazi...

nashangaa tu:
katika andiko lililokosa maana, umeweza kuliona goli la mkono?
Ni kweli huelewi kushindwa vibaya au hutaki kuamini.
kwa chadema iliyopata chini ya 30% ktk chaguzi zote zilizotangulia, ikipata 40% hapo haijashindwa vibaya, lkn ikipata 10% itakuwa imeshindwa vibaya.
Msomaji mzuri naye anatakiwa kumsoma muandishi kila eneo na sio kuchagua paragraphs zinazomvutia tu!
 
Umejuaje ndicho alichomaanisha? Usishangae CDM wakipata 48 lakini wasishinde akasema ndio kushindwa vibaya hivyo...
 
Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Karangalala tayari kuhutubia wakazi wa Geita mjini.​

Umati ukiwa umefurika kumsikiliza mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Karangalala,Geita mjini.
Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Geita mjini kwenye uwanja wa Karangalala ambapo aliwaeleza wakazi wa mji huo kuwa atahakikisha viwanda vinajengwa , wacimbaji wadogo wadogo wanapata maeneo ya kuchimba, ataboresha maslahi ya wafanyakazi , kuhakikisha madawa na huduma za afya zinakuwa bora zaidi na elimu bure kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha nne​
 
Back
Top Bottom