Kwanini UKAWA itashindwa vibaya?

Kwanini UKAWA itashindwa vibaya?

nashangaa tu:
katika andiko lililokosa maana, umeweza kuliona goli la mkono?
Ni kweli huelewi kushindwa vibaya au hutaki kuamini.
kwa chadema iliyopata chini ya 30% ktk chaguzi zote zilizotangulia, ikipata 40% hapo haijashindwa vibaya, lkn ikipata 10% itakuwa imeshindwa vibaya.
Msomaji mzuri naye anatakiwa kumsoma muandishi kila eneo na sio kuchagua paragraphs zinazomvutia tu!

Ni kweli. Kuna watu wanadhani hali halisi inaweza kubadilishwa kwa maneno ya kujifariji. Baada ya uchaguzi kuna watu watajifanya wachambuzi, lakini uchambuzi wa baada ya tukio ni usanii. Uchambuzi mzuri unatoa picha ya jambo litakalotokea
 
Eti ndio wanasema kampeni zimeandaliwa Vizuri yaani wanamuandalia hadi masufuria ya kupika Ugali.

blogger-image--124668832.jpg
 
Kuna tafiti zinafanyika ofisini na kuna tafiti zinafanyika mitaani...

attachment.php


Watu waliojingia maofisini vs wanatembea mitaani...kazi kwenu!
 
Fikara nzuri sana. Kuongezea kwenye uliyoandika; pia tusidharau mambo mawili ambayo hayaongelewi sana:
  1. Udhalilishwaji wa Dr. Slaa, Prof. Lipumba n.k.: Wapo wengi ambao wamekatishwa tamaa na hili tendo. Kwa hiyo baadhi ya wafuasi wao sio ajabu hawatampigia kura LOWASSA na sio ajabu wakaamua hata kumpigia kura Magufuli.
  2. Wapo wana UKAWA wengi ambao hawamtaki LOWASSA: Sababu yao ni moja tu, UFISADI wake ambao wameupiga vita kwa miaka mingi. Hawa sauti zao zimenyamazishwa na wale wenye midomo mikubwa, lakini nina uhakika wapo wengi. Kwa hawa, sio ajabu wanashiriki hata kwenye mikusanyiko ya UKAWA lakini wakiulizwa na TWAWEZA, wanamchagua mtu tofauti na Lowassa.

Kweli mkuu, mie nilikuwa CDM na kadi yangu ni 0393395 lakini kuja kwa Lowassa kumenifanya kuondoka na nasubiri niwape kichapo cha mbwa ..mwaka huu ni bora CCM itawale milele kuliko marehemu kuingia Ikulu natuko wengiiii sanaaaaa
 
Mtaji wa siasa ni watu, mtaji huu huwa unakuwa mkubwa sana ikiwa watu hao watakuwa katika mazingira ya kufanya maamuzi kishabiki. Mara nyingi ushabiki huwa na matokeo mabaya kwenye siasa, tofauti na kwenye mipira au muziki kwani katika siasa baada ya mechi ndipo malipo ya ushabiki yanahitajika sana. Ni kupitia ushabiki ndipo umuhimu wa kampeni na kusikiliza sera unakuwa haupo kwasababu wanaotakiwa wasikilize sera, tayari washakuwa washabiki. Sera hazina maana tena.

Kwa bahati mbaya, mwaka huu uchaguzi umetawaliwa na ushabiki, kuzidi au sawa na ule wa 2005. Wanasiasa wa Tanzania wamejua kuwa Watanzania tunapenda kufanya mambo kwa kishabiki.

Kamwe tusiingie kwenye mtego wa ushabiki linapokuja suala la uchaguzi. Ushabiki tuuache majukwaa ya mpira na muziki. Hapa tuchague mtu aje atufanyie kazi tunayotaka ifanywe kwa takribani miongo kadhaa.

Inawezekana, epuka ushabiki.

Hii ni kweli. UKAWA walipaswa kujua kuwa wana kazi kubwa zaidi ya kuhakikisha ujumbe wao unawafikia watu na wanaukubali. Katika uchaguzi huu wameshindwa kufanya hivyo kwa kuruhusu unnecessary distractions kama kupokea watu controversial toka CCM. Matokeo yake mada zinazopewa kipaumbele sio zile ambazo zingeongeza watakaoipigia kura UKAWA.

Anguko la UKAWA mwaka huu ni fundisho kwa chaguzi zijazo...
 
mbatia jana kasema ONLINE wanaongoza sasa sijui inakuwa huko online maana mtu mmoja anaweza piga kura zaidi ya mara 30 . huo ndio MBATIA anaoukubali
 
mbatia jana kasema ONLINE wanaongoza sasa sijui inakuwa huko online maana mtu mmoja anaweza piga kura zaidi ya mara 30 . huo ndio MBATIA anaoukubali

Online mtu mmoja ana id tano...Mbatia ndio wakuhurumiwa kabisa kapoteza muelekeo kabisa
 
Kuna tafiti zinafanyika ofisini na kuna tafiti zinafanyika mitaani...

attachment.php


Watu waliojingia maofisini vs wanatembea mitaani...kazi kwenu!

Kiongozi, Uchaguzi huu mpaka hapa ulipofikia numbers are not on Chadema's side.
Kampeni inayo nafasi ya kugeuza numbers, lakini tatizo ni kwamba Chadema/Ukawa hawaonekani kujifunza kutokana na makosa na ushauri wanaopata. Ndio maana kila siku wanaporomoka. Ile imani kuwa mgombea wao ataivunja CCM imeshagundulika kuwa haikuwa na ukweli, sasa walitakiwa kutafuta njia nyingine ya kuwaaminisha watu kuwa wanatosha kukabidhiwa nchi na kuleta mabadiliko yenye manufaa kwa nchi sio kwa kikundi kidogo cha wanasiasa.
 
Nianze kwa kusema ,duniani hakuna aliyemkamilifu tumejaa udhaifu mwingi ndiyo maana nadhani ndiyo sababu Mungu aliweka amri 10 na sheria zingine ndogondogo kulingana na wkt na uhitaji hii ni kuwabana watenda kaz katika nyumba yake kwa kila jambo muhimu wafanyalo ktk ktk utumishi wao na jamii yao kwa ujumla.

Hii imekuwa kiu ya watanzania kila uchaguzi na nchi nyingi za kiafrika kila uchaguz tukimsaka perfect man(mtu mkamilifu) ambaye kihalisi hayupo, sisemi tuweke yeyote bali tunapaswa kwanza tuamini kuwa hakuna aliyekamilika bali tuamini tunaweza kuwa na mfumo bora wenye kuwabana watu japo kutumika ktk masirahi mapana ya uma.

Ukitaka kujua uhalisi wa hoja hii fuatilia kila mgombea wako utagundua kuwa hakuna asiye na doa either kimaamuzi /kiutendaji ktk wizara/idara aliyowahi kuaminiwa.

Huwezi walaumu ni mfumo wetu uliosababisha haya kutuaminisha kuwa kuna mtu mkamilifu hivyo kumkabidhi mamlaka makubwa kimaamuzi kwa niaba ya taifa kitu ambacho wote tunakubali kuwa umefeli.Hii ni kutokana na ushahidi ulio wazi kuwa watu wamefanya maamuzi ya taifa kwa masrahi yao.

Ndiyo maana tunasema hatuhitaji mtu bali tunahitaji mfumo ongozi na siyo mtu mkamilifu ambaye hayupo.Mfumo huu msingi wake ni katba yenye masrahi mapana ya umma, ilakayotupa new structure(Muundo mpya) wa serikali yenye kuweka nguvu kubwa ya kimaamuzi kwa watu na sio mtu.

Leo utakuta tunawalaumu mawaziri/viongozi kuwa waliamua vibaya sio kosa lao they are actually expressing that they are human being thus, they are not perfect.

Maamuzi ya masuala ya umma yaamliwe /yachakatwe na wengi(wabunge wetu, wataalam wetu) ambapo maamuzi yote yatazingatia mazingira yote kiuchumi, kisiasa,kisheria nk.

Ukimuona Obama anatangaza kitu sio yeye bali wachumi na wataalam wote wameshachaka kuona masrahi mapana ndani ya uamuzi huo...

Binafsi naunga mkono jitihada zote zinazodai mabadiliko ndani ya nchi hii tukianza na katiba.

Watanzania hatuhitaji mtu tunahitaji mabadiliko ya mfumo mzima hasa katika maamuzi ya umma.
 
Kazi nyingine mlionao chadema, ni kumsafisha kwanza mgombea, alafu ndo muanze kunadi sera…sasa kwenye majukwaa ni kazi ngumu sana, kuna kitu kimoja Mbowe utajuta sana, kumpa lowasa agombee urais!! Wewe umeonaa sawa, lakini itakucost sanaa!!!
 
Kweli mkuu, mie nilikuwa CDM na kadi yangu ni 0393395 lakini kuja kwa Lowassa kumenifanya kuondoka na nasubiri niwape kichapo cha mbwa ..mwaka huu ni bora CCM itawale milele kuliko marehemu kuingia Ikulu natuko wengiiii sanaaaaa

Ondoka faster gamba na mnafiki mkubwa wewe. Unajidai CHADEMA kumbe ni gamba mkubwa. Hatuhitaji kura yako
 
ukawa watashindwa maana wameisha shindwa kusimamia vinywa vyao kuwa lowasa fisadi serikali ya ccm iache kumlinda lowasa eti tunaushahidi tosha dhidi ya lowasa leo lowasa msafi hahaha wananchi wengi hawaelewi na wanawashangaa sana pia ndani ya ukawa wenyewe hususani chadema wengi hawatampigia lowasa kura maana hawajiridhika na ujio wake ndani ya chadema na ukawa
 
Hakuna alokatishwa na tamaa na lolote linalohusiana na slaa na lipumba
 
hawa ccm wanajidanganya kwenye magroup yao... waje waanzishe thread huko halafu waishabikie kwa maneno ya uongo mmefeli
 
CCM magufuli hauziki hata kwa mafungu eleweni tu na ndio maana hata ilani ya uchaguzi ya CCM kaiweka pembeni then anabaki kushangaa
 
ukawa watashindwa maana wameisha shindwa kusimamia vinywa vyao kuwa lowasa fisadi serikali ya ccm iache kumlinda lowasa eti tunaushahidi tosha dhidi ya lowasa leo lowasa msafi hahaha wananchi wengi hawaelewi na wanawashangaa sana pia ndani ya ukawa wenyewe hususani chadema wengi hawatampigia lowasa kura maana hawajiridhika na ujio wake ndani ya chadema na ukawa

Na ndio tatizo la kuendeshwa na matukio. Wanajikuta hawana kauli thabiti, kauli zinabadilikabadilika kutokana na matukio...
 
Back
Top Bottom