Kwanini UK inataka kujitoa EU? Madhara yake ni nini hasa?

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,303
23,055
Nimekuwa nafuatilia mtanange wa UK kutaka kujitoa katika umoja wa ulaya kwa kuitisha kura ya maoni nchini mwao, Brexit.

Ingawa mpaka sasa sijajua sababu kubwa ya maana ambayo inaifanya UK kujiondoa kwao ukiachilia mbali suala la kupokea wahamiaji.

Kwa wenye uelewa wa suala hili tunaomba anisaidiee kujibu maswali haya.

1. Sababu za uk kujiondoa EU

2. Athari ambazo UK inazipata ikiwa katika umoja huo

3. Athari za UK itazipata ikijiondoa katika umoja huo

4. Ushawishi wa UK nje ya umoja huo

5. Uhusiano Wa a kibiashara wa UK ndani ya EU na nje ya EU
 
Kuendelea kuwepo kwenye umoja huo, kutashusha thamani ya pesa yake kwakuwa euro ndio inatumika zaidi kama common currency. Ikumbukwe kuwa, pound ya uingereza ndio pesa yenye nguvu kuliko pesa za nchi wanachama wengine
 
Kwan wakijitoa EU hawatoweza tumia euro?
 
Sababu zipo nyingi na watu wa hali ya kawaida wanaona wanaathirika moja kwa moja. .....kuna suala la mchango wa ulinzi :UK wao wanatumia visa yao hivyo wanawajibika kulinda mipaka yao lakini pia wanawajibika kuchangia gharama za ulinzi wa jumuiya ya ulaya ambayo inatumia visa moja. ......mbili. ..sheria za Uero kwa sasa ndio kama zinaongoza UK, mtu akishindwa mahakamani hapa basi anauwezo wa kukata rufaa Brussels na akishinda kule basi mambo yanabadilika. ....wahamiaji wengi wamepata 'stay' kwa style hiyo. ...pia suala la wahamiaji kutoka ulaya mashariki (hawa ni zile nchi maskini) kufurika Uingereza na ku abuse system yao (walikuja waka claim benefits bila kufanya kazi then kuchukua pesa ya benefits na kwenda kujenga kwao).....hizi ni baadhi tu ya kwanini wanataka kijitoa. ..lkn faida za kuwepo kwenye muungano pia zipo nyingi. ....mojawapo ni uuzwaji wa bidhaa zao kwenye nchi za muungano, ulinzi kama nchi mwanachama akivamiwa. ..juzi kati russia alikuwa anarusha ndege zake na kuingia mpk kwenye anga la muingereza hivyo ingetokea la kutokea ilikuwa ni Uero wote wanawajibika kumsaidia muingereza
 
Kero kubwa ni kwamba mnamo mwaka 1992 jamaa walikubalina mambo kadhaa kwenye ‘Maastricht Treaty’ kuwa kutakuwa na sera ya pamoja kwenye mambo ya usalama wa ndani na kimataifa, sera moja ya mambo ya nje ya bara kimataifa, sheria zinazolingana katika nyanja karibu zote za mambo ya ndani na European citizenship isiyo na mipaka.

Kuhakikisha kila mtu ana comply na 'Maastricht Treaty' European Commission wakaja na 'Article 267 Treaty on the Functioning of the European Union’ (TFEU) which was established in 2009. Hii article imetengenezwa Brussels na influence za wachache ambapo nchi nyingi awana sauti za juu including UK na moja ya jambo kuu ni kwamba wameipa mamlaka ya juu ya kisheria Court of Justice of the European Union’ (CJEU).

Kwakuwa kuna EU regulations ambazo nchi zote lazima zisifuate kama zilivyo kisheria na secondary legislations ambazo nchi inaweza implement itakavyo, under article 267 TFEU kukiwa na kesi yenye mzozo wa interpretation swala inabidi lirudi CJEU sio tena kwenye mahakama za juu za rufaa kwenye kila nchi (these means all the nation precedence do not matter any more).

Hilo swala ni kinyume na 'legal positivism' za nchi nyingi ambazo bunge na judicial system inaweza jiamulia; kwa sasa 60% ya sheria zote zinatoka Brussels na waingereza cant do nothing but to comply as part of supranationalism wanayotaka kutengeneza na hizi sheria zinagusa kila sehemu ya jamii kuanzia biashara mpaka government services sectors; hapo sasa ndio mzozo ulipo wengine wamechoka na wengine wanasema hakuna tatizo (however even the in campaign admit there is the need to renegotiate some terms).
 
Uingereza kwa sasa ni 'waarabu' wa Ulaya so wamejaa malalamishi na kuhisi kuonewa onewa tu.
Ndiyo maana wanataka kujitoa, katika shirikisho wao wanataka utambulisho kama nchi ubaki yaani kama zanzubar. Full ubinafsi, wanadai utamaduni na pride yao hawataki vimezwe na umoja huo. Wamekua waaarabu pyua kabisa.
 
Kero kubwa ni kwamba mnamo mwaka 1992 jamaa walikubalina mambo kadhaa kwenye ‘Maastricht Treaty’ kuwa kutakuwa na sera ya pamoja kwenye mambo ya usalama wa ndani na kimataifa, sera moja ya mambo ya nje ya bara kimataifa, sheria zinazolingana katika nyanja karibu zote za mambo ya ndani na European citizenship isiyo na mipaka.

Kuhakikisha kila mtu ana comply na 'Maastricht Treaty' European Commission wakaja na 'Article 267 Treaty on the Functioning of the European Union’ (TFEU) which was established in 2009. Hii article imetengenezwa Brussels na influence za wachache ambapo nchi nyingi awana sauti za juu including UK na moja ya jambo kuu ni kwamba wameipa mamlaka ya juu ya kisheria Court of Justice of the European Union’ (CJEU).

Kwakuwa kuna EU regulations ambazo nchi zote lazima zisifuate kama zilivyo kisheria na secondary legislations ambazo nchi inaweza implement itakavyo, under article 267 TFEU kukiwa na kesi yenye mzozo wa interpretation swala inabidi lirudi CJEU sio tena kwenye mahakama za juu za rufaa kwenye kila nchi (these means all the nation precedence do not matter any more).

Hilo swala ni kinyume na 'legal positivism' za nchi nyingi ambazo bunge na judicial system inaweza jiamulia; kwa sasa 60% ya sheria zote zinatoka Brussels na waingereza cant do nothing but to comply as part of supranationalism wanayotaka kutengeneza na hizi sheria zinagusa kila sehemu ya jamii kuanzia biashara mpaka government services sectors; hapo sasa ndio mzozo ulipo wengine wamechoka na wengine wanasema hakuna tatizo (however even the in campaign admit there is the need to renegotiate some terms).
Sikujua kabisa kwamba Tanzania kuna watu wenye weledi mkubwa namna hii wa kutathmini masuala ya miungano given the tendency tuliyokuwa nayo inapokuja kwenye suala letu, huwa tunaongelea faida za kuoleana na kuzaliana! Hayo ndio exactly masuala ambayo wenzetu wanayachambua. Such an amazing grasp of the issues.

Sababu zipo nyingi na watu wa hali ya kawaida wanaona wanaathirika moja kwa moja. .....kuna suala la mchango wa ulinzi :UK wao wanatumia visa yao hivyo wanawajibika kulinda mipaka yao lakini pia wanawajibika kuchangia gharama za ulinzi wa jumuiya ya ulaya ambayo inatumia visa moja. ......mbili. ..sheria za Uero kwa sasa ndio kama zinaongoza UK, mtu akishindwa mahakamani hapa basi anauwezo wa kukata rufaa Brussels na akishinda kule basi mambo yanabadilika. ....wahamiaji wengi wamepata 'stay' kwa style hiyo. ...pia suala la wahamiaji kutoka ulaya mashariki (hawa ni zile nchi maskini) kufurika Uingereza na ku abuse system yao (walikuja waka claim benefits bila kufanya kazi then kuchukua pesa ya benefits na kwenda kujenga kwao).....hizi ni baadhi tu ya kwanini wanataka kijitoa. ..lkn faida za kuwepo kwenye muungano pia zipo nyingi. ....mojawapo ni uuzwaji wa bidhaa zao kwenye nchi za muungano, ulinzi kama nchi mwanachama akivamiwa. ..juzi kati russia alikuwa anarusha ndege zake na kuingia mpk kwenye anga la muingereza hivyo ingetokea la kutokea ilikuwa ni Uero wote wanawajibika kumsaidia muingereza
Very illuminating take. Kwenye suala la ulinzi nadhani NATO inawatosha Waingereza kwa sababu NATO inajumuisha bigger and better defenses kutoka nchi nje ya EU.

Full ubinafsi, wanadai utamaduni na pride yao hawataki vimezwe na umoja huo. Wamekua waaarabu pyua kabisa.
Quite far from that. Utamaduni has never been an issue within the brexit camp. Utamaduni wa Mwingereza na Mjerumani, kwa mfano, unatofautiana nini cha mno cha kusema unajitenga kuukwepa? Watu wa dunia ya kwanza hawachambui mambo kama sisi tunavyotathmini masuala ya Muungano wetu kwa kuangalia "tamaduni zetu na babu zetu wamoja..." hell no. Wanaangalia mambo substantive kama yalivyoongelewa na wadau wengine hapo juu.
 
Back
Top Bottom