Kwanini UDASA isiwe Chama cha Wafanyakazi?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
University of Dar es Salaam Academic Staff Association almaarufu kama UDASA si chama cha wafanyakazi. Ni mkusanyiko tu wanazuoni wahadhiri ambao 'hutetea' maslahi hasa ya wahadhiri UDSM. Zipo enzi za UDASA za kupigiwa mfano.Ni zile za Hayati Prof. Chachage Seth Chachage kama mwenyekiti. Hata wakati wa Dr.Nyaoro na Dr.Mkumbo Kiltila UDASA ilisikika.

UDASA hushirikishwa kwenye vikao vya maamuzi vyote vya chuoni UDSM. Hushindana kiuwakilishi na THTU na RAAWU ambavyo ni vyama vya wafanyakazi chuoni hapo. Lakini UDASA bado inabakia kuwa si chama cha wafanyakazi. Kudhihirisha hili,UDASA,mwaka 2010 iliandaa mgomo wa wahadhiri.Mgomo haukufanikiwa.Sababu ni moja: si chama cha wafanyakazi kama kilivyo cha akina-Gratian Mkoba na vingineyo.

Sasa,UDASA inashirikishwa vikaoni kama nani? Kwanini UDASA isisajiliwe kama chama cha Wafanyakazi? Najua Dr.Kitila umo humu javini. Tusaidie juu ya hili. Na wengine karibuni pia
 
Ungeweka na malengo yote ya UDASA pengine ungekuwa na hoja. Mwingine anaweza kukuuliza kwa nini UDASA iwe chama cha wafanyakazi? Kwani lengo la vyama vya wafanyakazi ni kuandaa migomo?
 
Ungeweka na malengo yote ya UDASA pengine ungekuwa na hoja. Mwingine anaweza kukuuliza kwa nini UDASA iwe chama cha wafanyakazi? Kwani lengo la vyama vya wafanyakazi ni kuandaa migomo?

Kiufupi,UDASA yafanya kazi zote za Chama cha wafanyakazi LAKINI YENYEWE SIO
 
Back
Top Bottom