Mtoa mada, unapoandika bandiko lako humu jukwaani, kwanza jitathmini ndio uandike ndugu yangu, unapozungumzia suala la uwanja wa ndege ujue unazungumzia moja ya vitu vikubwa sana ambavyo vina gharimu ma bilion ya pesa, sasa ujue kuna vitu viwili inatakiwa uvifahamu.
1: Kuwekeza pesa
2: Kuzika pesa
Sasa unapozungumzia suala la uwanja wa ndege wa chato , kimsingi ni lazima tukubali kwamba ule sio uwekezaji bali ni uzikaji wa pesa , tafsir halis ya kuwekeza ni kwamba unawekeza sehemu ambapo kuna shughuli fln za kiuchuni zinafanyika, sasa kama utatumia mabilion ya pesa kwenda kuweka kitu ambacho ni kwa manufaa yako ww binafs maana yake huo sio uwekezaji bali ni uharibifu wa pesa za uma.
Binafs sina chama na wala sijishughulishagi na mambo ya siasa ila pale penye ukweli sina budu kufanya ivyo kama mtanzania mwenye mapenzi na nchi yangu, pesa kama ile angeamua kuipeleka kwenye miradi ya maendeleo ingemjengea sifa kubwa sana sababu ni miongon mwa vitu ambavyo angeweza kuviongea kwenye ilan ya chama chake, lakin kwa kile alichokifanya hawezi akasimama mbele ya watu akaongea kwamba moja ya maendeleo aliyoyafanya ni pamoja na kujenga kiwanja uko kwao.
Kwaiyo kujenga viwanja 11 ni jambo jema sana na la kimaendeleo lakin je! viwanja ivyo umevijenga wapi? sehemu ulipojenga kuna shughuli za kiuchumi zinaendelea uko? kwaiyo ndugu yangu tusiongee kishabiki bali tuongee kwa mapenzi ya tanzania na inapendeza ukiwa mkwel zaid ili hata kama mh atakuwa anasoma makala zetu atayafanyia kazi aya tunayoyazungumza hapa, msipende kusifia kitu ambacho kina muharibia mtu uwajibikaji , inatakiwa tuwe wawazi ili ajue na apate kuyafanyia kazi aya tunayoyazungumza. Mungu ibariki Africa , Mungu ibariki Tanzania & Mungu mbariki rais wetu mpendwa Dr John