Uchaguzi 2020 Kwanini Tundu Lissu anatumia muda mwingi kutafsiri Katiba na Sheria badala ya kutangaza sera?

Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu huleta Amani na Furaha

Kwa sababu katiba ndiyo msingi wa kila kitu, mtawala akikuta katiba inamuongoza katika haki basi watu watakuwa na furaha na hata wakilia watakuwa wanalia kwa machozi ya furaha.

Kama hujaelewa hilo la Uhuru na Haki basi jiongoze kwa kumsikiliza Bishop Mpemba

Source : Bishop Augustine Mpemba
 
Mwandishi wa makala sijui nijiweke kundi gani,mbona wengine Kila Mara wanasema wamejenga hiki na kike wakati ni kazi yao na kitu Cha kawaida kwa kuwa wananchi wanalipa Kodi,walitaka ajenge Nani wakati wao wanakusanya Kodi,Sasa hizo nazo ni sera?
Bora yeye anaetafsiri katiba anatufundisha na sisi wengine tusiojua
 
Haki za watu zimeelezwa katika sheria, mtu akijua haki zake basi hata kumwonea inakuwa ni ngumu. Kutokana na namna watu walivyobambikiwa kesi, basi faraja kubwa ya wananchi ni kutaka kujua wapambane vipi zamu yao yao ikifika ya kubambikiwa kesi, hata mipango ya uchumi ina base zake katika sheria.
 
Anagombea kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania
 
Sielewi anatuchukuliake watanzania... hata kama ndo kutafuta kuungwa mkono na nchi zilizotutawala lakini sio kiivyo hii ni aibu watanzania hatupo hivi
 
Majukwaani wanadai maendeleo hayana vyama. Ila wenye kuleta hayo maendeleo kwa fedha ya walipa kodi uangalia kwanza ni wapi chama chao kinaongoza na huko kunakoongozwa na vyama vingine tofauti na wao ni kwa watoto wa kambo ambao hawalipi kodi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…