Kwanini tunasubiri matokeo ndio tuongelee mfumo wetu wa elimu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini tunasubiri matokeo ndio tuongelee mfumo wetu wa elimu?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mbunifu, Feb 7, 2011.

 1. m

  mbunifu New Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nashangazwa na hii hali. Kwanini tusubiri matukio ndio yatuibulie mijadala juu ya mambo muhimu kama kiwango cha elimu. Je, kama matokeo ya mwaka huu yangekuwa wanafunzi wamepasi kwa asilimia 80 tungesema kuwa madarasa yasiyo na madawati, shule zisizo na maabara, walimu wanaokaririsha majibu na wanafunzi wasio na maadili ndio vinaleta ushindi? Kwanini, mitihani ndio kipimo chetu cha elimu?
   
 2. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wametuambia kuwa elimu is free, tunakimbizana na malengo ya MDG, lakini tunailipia kwa kuwa na vijana wengi wasio'achieve basic education. Kutoijadili ni dili kwa wenye mashule ya private, kwani inakuwa kila mzazi ajitegemee, kujaribu kumpa mwanae this gift.
  Msolo, see you again next year for more comments, in the meantime, mashule (English Medium) zyatakuwa mengi na yakutosha, wenye nazo wataipata elimu, wengine wasubiri...
   
 3. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwa sababu matokeo ndiyo kiashiria cha kushuka kwa elimu, full stop!
   
 4. m

  mbunifu New Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dume, hebu rudia tena. Inawezekana, kuna kipimo bora zaidi cha elimu zaidi ya mtihani. Kumbuka, unakaa darasani kwa mamia ya masaa kwa miaka minne, ama saba, kwa mwanafunzi wa shule ya msingi, kisha unafanya mtihani kwa masaa machache tu.

  Pia, tazama muda unaokuwa shule, si wote unakua darasani, kuna vitu unajifunza nje ya darasa. Nafikiri elimu ni kujifunza, hii ni tofauti na kujiandaa kwa ajili ya mtihani wa kuvuka darasa.

  Hebu, chuja tena, tafuta mtihani uliofaulu hadi kufika hatua ya madarasa uliyonayo, kisha tazama yale uliyojifunza darasani, ulinganishe na yale unayotumia unapohitaji kufanya jambo ambalo waona ni muhimu kwa mafanikio yako--kama kufanya kwa umahiri kila kipengele cha kazi uliyoajiriwa, kuongeza kipato kwa kufungua project, mahusiano na watu, networking, afya ya familia yako, pengine hata starehe. Unafikiri bila huo kupasi huo mtihani, ungekuwaje? Ungeshindwa vile unavifanya sasa hivi?

  Au, je kwa kupasi mtihani umevifanya kwa umahiri zaidi? Ukimaliza kufikiri hilo, hebu ona wale uliowaacha nyuma kimadarasa, je wameshindwa kupata mafanikio? Je, kila mahali ulipoenda ili kutafuta fursa za maendeleo mtihani uliofaulu ulikusaidiaje? Ama ni jumla ya mafunzo yako, tangu nyumbani, mazingira ya shule, na wepesi wa kutia katika maisha kile ulichojifunza ndio uliokutoa kwenye hatua moja hadi nyingine ya mafanikio yako.
   
 5. m

  mbunifu New Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Elimu, haitaweza kuwa bure, amini usiamini. Kweli shule inaweza ikubali kukuandikisha bila ada. Lakini elimu ya bure? Inawezekana kweli hiyo? Naona kama tayari ulikuwa unajijibu mwenyewe kwa kusema english medium zipo. Lakini English medium is not everything about education, it could turn out to be the miseducation of a generation.
   
Loading...