Kwanini tunaipenda North Korea?

Thread hii wale wanaowakumbatia imperialists huwezi kuwaona
hahah...unanikumbusha kauli za Iddi Amin Dada akiwapiga mkwala utawala wa South Africa chini ya uongozi wa makaburu.... Hata hivyo elewa kwamba humu Duniani kila binadamu ana malengo yake based on need and choices. kuna makundi makuu 3 ya mifumo ya kiuchumi, nayo ni ubepari, uchumi mchanganyiko na ujamaa. kila nchi huamua inataka kufuata mfumo upi na kwa malengo gani...hata hivyo ujamaa haujawahi kufaulu kokote duniani( prove me wrong..) soma kitabu cha Robin Blackburn on The Failure of Communism and the Future of Socialism or kasome kitabu cha Antony Polonsky on Poles, Jews, Socialists: The Failure of an Ideal , Volume 9...
 
mkuu kama umenielewa vizuri hakuna sehemu ambayo nimeelezea mrengo wa nchi hapo mimi nimegusia ukoloni mambo leo (neo colonialism )

kama ulikua hujui huko marekani saiv kuna vuguvugu la kubadili mrengo wao wa capitalism wengi wa wanaharakati wanauona ni mfumo uliopitwa na wakati

hakuna sehemu yoyote duniani ambayo mfumo wa ujamaa umefeli achana na UTOPIAN SOCIALISM kinachotokea ni nchi za kibepari zinaingilia kwa makusudi nchi za kijamaa ili kuziharibu

usishangae siku unaamka unakuta us imebadili mfumo na kuingia kwenye ujamaa ila wakiwa wameuboresha
 

Utabiri wako ni SPOTON kabisa, hilo litakuja kuikumba USA hata wanao jifanya ni marafiki watamgehuka wakiona anakaribia kushindwa na madui wake, Mataifa kama Japan(bado wana makovu ya mabom ya nuclear ingawa hawasemi wazi wazi lakini deep down wanataka kulipiza kisasi at opportune time) Taifa lingine ni Ujerumani(kutokana na Miji ya Taifa lao kupigwa mabom na ndege za Marekani na kuua raia wengi mwisho mwishoni mwa WW2 hapakuwepo na ulazima wa kudondosha mabom hayo wakati walishajua Hitler amekwisha shindwa vita) Taifa lingine ni Italy - mambo yakiwaendea vibaya USA mataifa yote tajwa hapo juu yatajiunga na maadui wa USA kwa lengo la kuikomesha.
 
umehitimu kidato cha nne???

Mkuu huna haja ya kujibizana na binadamu wa design hii, sina hakika kama anaelewa kinacho zungumzwa hapa!! Kwenye society watu wa namna hiyo hawakosekani - hana la maana la kuchangia kazi kuzodoa watu tu na kutoa lugha zisizo na staha.
 
Sawa ila mi team UsA ikiwa kiushabiki,kivyovyote mi team UsA
 

Mkuu unategemea vitabu vilivyo andikwa na watu wenye damu/asili ya Anglo-Saxon wataandika nini? - Nimeona mwandishi mwingine ana jina la ki-Pole, hizo ni zuga tu za kuendeleza propaganda zao.

Mbona hawazungumzii kipindi cha miaka ya 1950/60 wakati uchumi wa USSR ulipokuwa imepiku wa USA - wanaweza kutueleza USSR ilifanikiwa vipi wakati itikadi zao zilikuwa ni za U-Communism, je, China imefika fikaje kuwa Taifa la pili Duniani lenye Uchumi mkubwa nyuma ya Amerika and come 2020 itakuwa imezidi Uchumi wa USA - mark you, China ni Taifa la kikomunisti don't U 4get that!!!

Hizi propaganda za mataifa ya Ulaya na Marekani kuandika vitabu na ngojera za kutaka kuhadaa Dunia kwa madai yao yenye lengo la kuonyesha "Blessings za U-Capitalism na evil of Communism" adithi hizi mpaka lini, wanataka tuabudu U-Capitalism ili waendeleze unyonyaji wao kwenye nchi masikini, watuibie maliasili zetu na kutuachia mashimo - nani ambaye ajui ukweli huo? Wakumbuke hivi sasa Dunia imekwisha elevuka.
 
Sure bro....
 
Mimi mwenyewe Niko mbaali sana na hawa mabepar,kwa sababu wamesababisha asillimia kubwa ya sisi waafrica kuwa omba omba vilevile wamesababisha dharau/ubinafsi among wasionacho na wenyenazo Niko tayale kuungana na NK kwaajili ya kupoteza hawa pepo..
 
Mi
umehitimu kidato cha nne???
Siku izi ni darasa la elimu msingi yan la kumi seko bado
 
Hata mimi naichukia sana Marekani. Naichukia kutokana na upuuzi,uonezi na uchokozi wao.
Natamani siku moja Mapanki awatandike Wamarekani kwa kipigo ambacho kitakuwa ni cha aina yake na cha kihistoria.
 
"Tuipende" umeandika kama mko wengi kumbe uko mmoja. ungeandika "kwanini naipenda north korea" , si wote wanaipenda so ingekuwa ni vizur kujielezea mwenyewe na si kujumuisha watu wengine maana misimamo yao huifahamu.
 
Mkuu hapo umenena kweli. Mi kiongoz ninaemkubal Africa peke yake ni RobertMgabe, na Maguful kidogo. Wengne n Puppets tu
 
"Tuipende" umeandika kama mko wengi kumbe uko mmoja. ungeandika "kwanini naipenda north korea" , si wote wanaipenda so ingekuwa ni vizur kujielezea mwenyewe na si kujumuisha watu wengine maana misimamo yao huifahamu.
mkuu chambua maudhui na sio kuchambua sentensi kama ina kiima ama kiarifu

nimeweka uwingi kwasababu siko peke yangu ni watu wengi wanamawazo kama yangu na ndio maana nimetumia wingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…