Kwanini tunaipenda North Korea?

buzitata

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2017
Posts
2,370
Reaction score
7,900
habarini wana jamvi

leo nimeona niwaletee japo kwa kiduchu sababu ambazo wengi zmetufanya tuipende north korea na sio us

first of all watu wengi wamechoshwa na ukoloni mambo leo.. kwa wale waliosoma history vizuri wamenielwa

ni dhahiri kwamba serekari ya Pyongyang ni miongoni mwa serekali ambazo zinajitahidi vikali kuupinga ukoloni mambo leo ambao serikali ya marekani umekua ukiuendesha kwa miongo mingi tangu vita kuu za dunia kumalizika

nchi nyingi za kiafrika zinatamani kuwa kama north korea yani kujitegemea zenyewe pasipo kupangiwa viongozi na mfumo wa maisha wasioutaka lakini mwisho wa siku zinaambulia patupu kwasababu ya njaa wanaamua kukubali kuendelea kutawaliwa

amini usiamini kwa ulimwengu huu tulionao ni nchi chache sana ambazo hazitawaliwi (hazipo chini ya ukoloni wa nchi nyingine)

afrika kulikua na nchi kama libya, nchi ambayo ilijitoa kimasomaso kuukataa ukoloni mambo leo na tukaona namna ambavyo walibya walivokua wanakula bata yani ilikua mtu ukitaka kuoa serikali inachukua jukumu la kukutafutia makazi pia kulikua na marupuupu ambayo raia walikua wanapewa yani ilikuwa ni full raha lakini maskini ya mungu hayo yote yaliyeyuka baada ya kuukubali ukoloni mambo leo uwatawale

nchi zote unazoziona duniani zina mafanikio ujue hazitawaliwi

tunarudi kwa north korea

watu wanasema sijui eti watu wa huko (NK) wanapata shida mara sijui hawautaki utawala wao hayo yote ni uongo mtupu watu wanafurahia maisha yao.. watu wenye fikra pana wanasema ni bora kula mihogo kuliko kula ugali wa msaada tena wenye masharti

NK ni inchi iliyowekewa vikwazo vingi vya kiuchumi lakini bado mpaka leo hii wanaendelea kupasua anga tu hawalali njaa na bado nuclear wanairutubisha kama kawaida

haihitaji akili nyingi kuukataa ukoloni mambo leo ni just viongozi kuamua tu kutumia rasilimali zao ila unakuta nchi nying za afrika kila wakijaribu kufukuta unakuta wanaangukia pua ..why??????

all in all marekani ameshashindwa kumtungua bwana mdogo mapanki saiv anahangaika tu kujisafisha kwamba NK hapaingiliki


KARIBUNI.....
 
Saaaafi.haya ndio mawazo ya mtu alie hai.anatembea huku akili yake ikiwa hai.kuna wengine akili ni mfu kbs kw taalifa yako mm naichukia malekani kw sbbu ya yale inayiyafanya.jikumbushe kdgo.patrice lumumba aliuwawa na malekani.eduardo mondlaine wamalekani.thomas sankala.malekani.augustino neto wa angola wamalekani pia mtizame ghadaff.mtizame saadam hussein hizi zoote ni damu za viongozi waliouwa na malekani kw sbbu tu walikataa mambo ya wamalekani.kw hiyo yeyote mpenda haki lazima aichukie malekani.
 
Korea ambalo limeamua kuishi maisha yenye Uhuru wa kweli na liko radhi kukabiliana na vikwazo vyote kwa gharama ya Uhuru wao! Mataifa mengine yaliyo huru kabisa ni urusi, Cuba na Zimbabwe!
China taratibu ameanza kuhisi kutawaliwa na marekani kwa ajili ya hofu yake ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na marekani!
 
pamoja
pamoja sana
 
Kila napoyatazama mashimo ya buhemba ambayo hao mabepari walichimba dhahabu na kuacha NAUMIA, kila napoiangalia Nyamongo na jinsi inavyonyonywa na ACACIA GOLD MINE LTD pia NAUMIA, bila kusahau Geita wanavyonyonywa na BARRICK yaani NACHUKIA ZAIDI, Bado Tz haiko huru, bado sana Africa kuwa huru kwasababu vijana wengi wamefunzwa na hao Mabepari kuwa WASTAARABU wakati mali zetu zinazidi kuibiwa. 2nd AGE OF AFRICAN DARKNESS.
 
Pia ukuenda tanga Handeni kwa msisi na kule Ifakara mngeta utajua kwa nini Korea ni marafiki wa Tanzania

Mkuu hivi bado wapo Mgeta Ifakara au walituachia mashamba na vitendea kazi, jamaa hawa ni mfano wa kuigwa kimsimamo - stance zao katika masuala ya Geopolitics wanawakirisha/wasemea raia wote wa Dunia ya tatu - members wanao wasema vibaya Wakorea kasikazini na Kiongozi wao hawajui kinacho endelea Duniani - wanarudia rudia propaganda za MSM bila ya kutafakari media hizo zina serve interest ya Mataifa gani!!

Colonial hangover bado inatawala sana akili za baadhi ya Wafrica, as far as they're concern Dunia ni Ulaya na Marekani basi, uwambii kitu!! Wanaendelea ku-support blindly mabeberu wanasahau kabisa kusoma historia ya udhalimu, mauaji na ukatiri wa Mataifa haya ya magharibi - nani ambaye hajui Mayhem waliyo sababisha Africa, middle East, far East na East Europe na bado wanaendeleza siasa zao za ku-stir turmoil kila kona ya Dunia, Mataifa ambayo miaka ya karibuni yamekuwa na uwezo mkubwa kijeshi wanapaswa kushirikiana na kumwambia Uncle SAM na mapuppet wao kwamba enough is enough - they have a choice namely:Number one, wajifunze kuheshima Mataifa yote Duniani, Number two, wakiendeleza ubabe wao basi nchi hizo zitaungana kijeshi na kumkomesha, wasipo kuwa na ujasiri wa kumu-confront headon na ultimatum mkononi basi USA itaendelea kuchezea Dunia.
 
Thread hii wale wanaowakumbatia imperialists huwezi kuwaona

3% ya madini wao 97% nyie na bado kodi wanakwepa huku wakiacha mashimo lukuki

Halafu unamkuta mtu anatoka povu kuwashabikia na kuwaponda Pyongyang
 
Naunga mkonyo hoja, mi nauzika sana na tabia ya Marekani kujivika uMungumtu wa dunia. Wanataka kujifanya wao ndio remote ya nchi zote, kwahiyo wakijitokeza watu wanaopingana nao kama hawa wakorea kaskazini nakuwa upande wao
 

Well said mkuu, ila kidogo umeisahau IRAN nayo ina msimamo thabiti tangu miaka ya sabini - ila utawala na msimamo wa Ti Xing Ping hauleweki eleweki!!! Juzi hapa nilimshangaa Ti Xing Ping alipo mjia juu Kim na kumuwekea vikwazo vya kutonunua mkaa wa mawe kutoka KK!! Sasa sijui kama hayo yalikuwa ni maaigizo ya kutaka kumchota akili Trump au la.

Tukumbuke vile vile kwamba Ti Xing Ping aliwahi kuishi Amerika wakati wa masomo yake ya fani ya Kilimo katika Chuo Kikuu nimekisahau jina, alikuwa anaishi na familia ya wenyeji wake hakupanga chumba au kuishi kwenye Hostel, sasa sijui kama na hii inachangia China kuonekana hiko a bit reserved linapo kuja suala ya kukabiliana na matendo ya USA Govt.
 
Kwenye kampeni za Trump alisema ataishusha dhamani ya hela ya china makusudi kisa china ilikuwa inafanya biashara Marekani biashara haramu na udanganyifu wa hela.....

China sasa hivi anaangalia ni wapi kuna maslai makubwa kwake kati ya USA na N.Korea
 
Toa hizo L weka R
Marekani
Sankara
Sababu
kidogo

uandishi/ uandishi /uandishi
 
WE UNA KICHAA WEWE SEMA KWA NINI UNAIPENDA NORTH KOREA WEWE BINAFSI! NANI KAKUAMBIA WOTE HUKU TUNAIPENDA! YAANI MJITU UNAAMKA TU UNAANZISHA UZI HATA HUJUI UNAONGEA NINI
 
muhhidinramadhan Ni kitu ambacho hakiwezekani kwa nchi za kiafrika...... Viogozi wa Africa ni watu wenye tamaa ya hela halafu siyo wazalendo.... Niwalafi ni wabinafsi na hapo ndiyo mzungu anatumia huo mwanya kufanya yake.... Waafrica wanapigana wenyewe kwa wenyewe angalia Somalia, Sudani, Congo, Nigeria ni lini watakumbuka kuimarisha uchumi wa nchi yao

Gadaffi alikuwa na mpango wa kuanzisha bank ya Africa yaani tusiwe tunakopa tena kwa wazungu..... Wazungu walivyo shtuka angalia walicho mfanya....
 
Nilipokuwa primary palikuwa na mwenzetu mbabe yaan anaweza tia makonzi class lote na hakuna wa kubisha Sasa kuna jamaa alikuwa kafungwa bandage anakidonda kama kawaida yule Tyson wetu akampiga teke kwenye kidonda hadi bandeji kudondoka jamaa alilia kama mtoto akivuja damu Tyson akawa anamcheka Sasa mwenye kidonda aliponyamaza alisimama alimpiga bonge la kichwa Tyson chali! Huwezi amini mbabe wetu siku ile aking'oka meno 3 na tulipoona mbabe kazidiwa watu walishangilia na tangu siku hiyo akawa mdebwedo na hakuota meno hadi leo! Kisa hiki nakifananisha na US kwamba wanaomchekea ni vile hawana namna lakini mioyo yao inatamani siku US atolewe mapengo tena na asiyetegemewa na ndo hii dunia itapowa na si mda mrefu US asipokuwa na adabu atapapaswa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…