Kwanini tunaibeba DP World kiasi hiki?

Nani kakudanganya africa ina shida ya hela wewe. Africa wanashida na ufisadi na poor management. Hela inayoibwa ni mara kumi ya hela inayoingia serIkalini. So hata wakiwa wanatupa trillion mia kwa mwaka bado ni yale yale. Hiv husomagi repori ya CAG wewe? Africa haijawah kupata uhuru mkuu. Bado mindset zetu zinaacti kizungu katika kujisimamia. Hapa kwetu jambo la kwanza kabisa ni elimu. Wekeza sana kwenye elimu then the rest inakuwa historia. Binadamu mpe elimu tu inamtosha sana. Coz watu walioelimika wanaish kwa facts sio blah blah na wanafanya kila kitu wakibez na research na wanajali muda. Sasa hapa kwetu wameharibu mfumo wote wa elimu tuna wasomi wa hovyo waoga wa maisha wanaotegemea hisan ya siasa kuish.
 
Aione Faiza Foxy kwenye jalada!
 
Na hio tofauti unajiaminisha ni elimu kubwa sana timu ile ya wanasheria yaani hawajui kitu kabisa sisi huku mtaani ndio tunajua hilo.
 
Kafara ya mchakamchaka wa Moto, MOU Kati ya wakuu wa Kaya na Lucifar ili Lucifar atulindie amani ya Kaya yetu, imewaacha watz wengi mazuzu, na huu ndio mtaji wa wakuu wa Kaya, wataturudisha kwenye ukoloni huku tunaishia kukalamika kwenye keyboard, piga picha Tz ya miaka 50 ijayo, itakuwa kwenye direct colonialism, sad
 
Sasa tupewe trillion mia kwa mwaka dah bajeti ya miaka 2 hiyo hatakuwe na ufisadi gani lazima maisha ya watu yabadilike na taswira ya nchi lazima ibadilike hata rank ya nchi lazima ipae sio tena ya kipato cha chini bado tunahitaji fedha ili tuendelee bila fedha hatuwezi ndio maana akina Deng Xiaoping walifungua China mpaka kutengeza free coastal city ambazo zilikuwa rafiki kwa wawekezaji wa kigenina zile special economic zone za Shenzen na Guangdong sasa ndio export zone hizo na sasa leo hii mchina anatukopesha waliona na wakajua thamani ya fedha katika maendeleo wakaachana na zile stori za chairman zilizowapelekea great famine walipomuona mke wa Mao anawarudisha nyuma anawaletea stori za Mao kama zako fedha sio kitu wakampotezea kule , na kuleta reforms leo hii China is rich na ina mabilionea zaidi ya 200 endelea tu kusema fedha sio kitu.
 
Africa Africa Africa, ni nani aliyetuloga. Hatujifunzi kutokana na makosa yaliyofanyika huko nyuma?. Historia yetu inatuhukumu mpaka sasa, ni mikataba mingapi mibovu serikali hii na bunge hilihili limeshaipitisha na inatutesa?. Serikali ifute huu mkataba maramoja na kuanza mchakato upya wenye uwazi ili kuleta umoja wa kitaifa ambao sasa umetoweka katika muda mfupi. Kutumia mabavu hakutasaidia. Hakuna asiyetaka maendeleo, na uwekezaji ni sehemu ya kuleta maendeleo, ila sio kwa mkataba huu wa kifisadi na unyonyaji mkubwa. Hii itakuwa laana kwa wote ambao wataendelea kushupaza shingo. Mungu wetu hatanyamaza, ni swala la muda tu. Mengi yameshasemwa, kinachotakiwa ni kuufuta mkataba huu na kuanza mchakato mpya wenye transparency and kufuata sheria za nchi yetu.
 
Broda hiv umewah kukaa hizo nchi au unajisemea tu. Milango ya nchi inafunguliwa kwa mikataba hii ya kishenz. Hiv unajua Dubai hata uwe na hela kiasi gan huwez kupewa leseni ya kufungua biashara yoyote bila kuwa shea na mwenyeji!? Mbona mnakuwa malimbuken hivyo. Waarabu pamoja na kwamba wazungu ndio wachimbaji wa mafuta lakin mashirika yanamilikiwa na serIkali mzee. Nakutolea mfano mdogo. Kama utatafuta hela na zikawa nyingi kama hutaandaa wanao kwa maana ya kusoma hujafanya lolote. Ni utajir wa msimu na watakuja wagen kujichukulia huo utajiri tu. Tunahtaji wawekezaji ila kwa mikataba ipi. Na tangu tumeanza kuwekeza tumefanikiwa kias gan na tumefeli wapi? We unamzungumzia huyo rais wa china hiv unajua utaratibu wa kuwekeza soko la hisa la Shanghai wewe. Achen ubwege bana kama hujui kitu kaa kimya.
 
Dubai hata uwe na hela kiasi gan huwez kupewa leseni ya kufungua biashara yoyote bila kuwa shea na mwenyeji!? Mbona mnakuwa malimbuken hivyo.

NB: Sio Dubai tu huko nje ndio wenzetu wanavyofanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hivi kwa akili zako hizi za kucharuka kwa masoko hayo ya hisa ya shanghai etc sheria zake leo 2023 ndio hizo hizo zilitawala mwaka 1979 wakati wa mageuzi ya kiuchumi halafu umekaa nchi za watu kwa hiyo sisi hata tukitaka kujikwamua tufuate sera za mageuzi ya wakati ule wa kujikwamua au unataka tufuate sera za sasa za modern rich china iliyojitosheleza kila kitu tatizo sio kuwa na fikra je fikra zako zitakukwamua hapo ulipo kimkakati mwenzio alishapanda sasa anavuna wewe ndio kwanza unapanda halafu unajiweka kwenye same position ndugu yangu mbona ushafeli acha mhemko mambo yanataka fikra kuu na strategy usione vyaelea lazima ukae chini uviunde kwa utulivu
 
Dubai hata uwe na hela kiasi gan huwez kupewa leseni ya kufungua biashara yoyote bila kuwa shea na mwenyeji!? Mbona mnakuwa malimbuken hivyo.

NB: Sio Dubai tu huko nje ndio wenzetu wanavyofanya

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo hatuangalii walifikaje na sie tufike hapo sisi tunaangalia hapa walipofika wanafanya nini sasa nasi tufanye tuonekane kama wao .
 
Kwa mikataba hii ya hovyo tunayoingia kufika walikofika wao ni ndoto za kufikirika

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati wa dubai wenyewe pale kwao wanayo mahakama maalumu ndani ya zile free economic zone yaani DIFC COURT ambayo haitumii sheria za serikali ya dubai yenyewe inatumia common english law kusolve dispute zote kwa kampuni zote zilizomo au zinazofanya shughuli zake ndani ya dubai financial international centre na zile free economic zone sisi unadhani hayo tunayaweza halafu sisi wapiga kelele huku tunataka investor na fdi hapo unapata jibu kwa nini wawekezaji wakubwa wanakimbilia huko na wao pia sheria zao zinaruhusu mtu kupata land for 99 years au private ownership ktk zile special economic zone zao nadhani na wao walishauza nchi yao ama vipi ???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…