Kwanini tunafeli kwenye matangazo ya biashara

Kwanini tunafeli kwenye matangazo ya biashara

MARTIAL20

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2015
Posts
422
Reaction score
1,017
kwanini tunafeli kwenye matangazo ya biashara

tangazo linapiga kelele mpaka unaichukia tv yako mwenyewe [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
ongezeni ubunifu na sio kupiga makelele tu kuna matangazo yakirushwa hewani unatamani lisiishe
 
Gharama ndogo ndio tatizo

Ushaona matangazo ya simu, bia ynavyokua mazuri kuanzia maudhui, rangi, wahusika, sauti, picha....
Kule uwekezaji ni mkubwa sana

Makampuni mengine hayawekezi hela za matangazo
 
Gharama ndogo ndio tatizo

Ushaona matangazo ya simu, bia ynavyokua mazuri kuanzia maudhui, rangi, wahusika, sauti, picha....
Kule uwekezaji ni mkubwa sana

Makampuni mengine hayawekezi hela za matangazo

mkuu hili la voda la watoto linapiga sana walitoe tu wabuni lingine aiseee
 
Ni jinsi tulivyo, kila tufanyacho, twafanya kwa wepesi, bila ubunifu au umakini, bahili wa kugharamia matangazo, bado washamba...
 
Matangazo ya Majuto ni ya hovyo sana

Mungu ni Pendo
 
Lile la "NINA MPANGOOOOO NINA MPANGO" ndio liko ovyo na makelele - utadhani wanatangaza "Madansa wa Muziki" na si Kampuni ya simu.
 
kwanini tunafeli kwenye matangazo ya biashara

tangazo linapiga kelele mpaka unaichukia tv yako mwenyewe [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
ongezeni ubunifu na sio kupiga makelele tu kuna matangazo yakirushwa hewani unatamani lisiishe
Uko sahihi kabisa hasa matangazo ya itv kwanini yanakuwa na sauti kubwa mpka kero kwa anaeangalia tv
 
Kuna tangazo moja sijui ni la tigo sijui ni la voda......linasema "NINA MPANGO". Katika matangazo ya kibwege na ya ajabu lile ni mojawapo, choice mbaya ya mziki, halafu sijui nani kawaandikia script maana nahisi ni mtu kavamia fani si yake, pumbavu.

Yaani natamani niwalipe kampuni husika wasilitumie tena......hivi kwanini wanakuwa na matangazo yenye kero kutazama hivi
 
wanashindwa kujiongeza na kuwaiga cocacola ..yaani coca soda yao wao wala sio soda pendwa lakini jinsi wanavyojikita ktk ubunifu wa matangazo yao ndio wanazidi kuifnya brand yao kuwa ni brand inayokaa vichwani kwa watu mnoo...
kama hili tangazo lao la sasa LA yule demu na Jamaa wanaoendesha Gari maeneo ya nusu jangwa ...NI bonge LA tangazo ...though nakapnda sana kale kademu
 
Lipo la magodoro Channel 10, LA hovyo mno. Hata sauti za kushangilia haziendi pamoja.
 
Back
Top Bottom