Kwanini tunadanganywa kuhusu hali halisi ya uchumi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini tunadanganywa kuhusu hali halisi ya uchumi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Geza Ulole, Feb 13, 2011.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 4,000
  Trophy Points: 280
  Wapendwa wana jamiiforums, imefika wakati tutafakari kuhusu mwenendo wa taasisi zetu mbili yaani Wizara ya Fedha na Benki Kuu zilizo mihimili mikuu ya mustakabali wetu wa kujikimu hapa nchini! Wakati hali halisi ya mfumuko wa bei inaonekana wazi kila kukicha Gavana wetu Mkuu anasema uchumi uko katika hali nzuri yaani katika akiba za kigeni wakati huo huo hafafanui huu mfumuko unatoka wapi!? Vilevile inayofanywa siri kuhusu mapungufu ya bajeti 2010/2011 na Mh Mkulo si siri tena bali ni ufahamu wa kila mtu wafadhili wa bajeti yetu wamekataa kutoa hela kama walivyohaidi haswa kwa sababu ya kuona hali hairidhishi katika utawala wa nchi hii haswa kuhusu swala zima la uwazi, uwajibikaji na mabadiliko kuelekea mfumo bora wa utawala!

  Sasa ni kwanini kama wananchi wa nchi tunafichwa haya? au mpaka wanafunzi waandamane kuhusu fedha za kujikimu zisizotosha tena kutokana na kupanda kwa gharama za maisha kusikodhibitiwa? Au mpaka wafanyakazi waanze nao migomo maana naskia sasa hata mishahara inachelewa kutoka na hata wale walioongezewa wanalipwa mishahara ya zamani! Hivi haki yetu sisi ipo wapi? katika kujua mustakabali wa mambo yanayotuhusu sisi moja kwa moja? Hivi huu uchakachuaji hata wa hali halisi ya uchumi utaendelea hadi lini na kwanini Mh Mkulo anakuwa mtu wa mipasho na si mtu mwenye wajibu kuueleza umma ni nini kinaendelea? Imekuwa tabia ya Mh huyu kuwa mkali pasipo sababu anapoulizwa swala lolote la bajeti na amekuwa akitumia maneno kama "uwongo!?" au "umeskia wapi?" anapoulizwa kuhusu mapungufu makubwa ya bajeti yanayolikabili Taifa kwa sasa! naombeni tutafakari haki yaetu iko wapi katika serikali hii ya usiri isiyo shirikishi katika kueleza yanayojiri kabla mambo hayajafumuka!
   
 2. haibreus

  haibreus JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 296
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Tatizo kubwa watu wengi hawajui kabisa juu ya mambo ya uchumi wa nchi yetu,na wengine sio kosa lao kwani wamenyimwa fursa za kujifunza juu ya mambo ya uchumi na maendelo,kifupi wengi hawajui hata nini maana ya haki!
  so let us wake up and fight the minority who kill our future generation!
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kwa wenye akili hali hii haina haja ya kuambiwa, lakini serikali haiwezi hata siku moja kusema hali ya uchumi ni mbaya kwa kuwa wakisema hivyo ni kama kujitangazia wazi kuwa wameshindwa kazi. Hata kama mimi nigekuwa madarakani ningeendelea kudanganya.
   
 4. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu, kudanganya mpaka lini..hawajatambua waTz wengi siku hizi hawadanganyiki tena?
   
 5. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi nafikiri walioko ndani baada ya kuona mambo hayaendi wameamua kuiweka hiyo iendelee kuwa siri yao, huku wenyewe wakifanya kila njia kuchukua chao mapema ili mambo yakienda kombo wawe na pakuhegemea.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,624
  Likes Received: 82,221
  Trophy Points: 280
  Mkullo kwa kutangaza bajeti ya Serikali ya mwaka 2010/2011 ambayo imemalizika miezi sita kabla ya muda wake ni dalili tosha kabisa kwamba kazi imemshinda. Sasa hivi wanahaha huku na kule kutafuta pesa kwa kuomba kutoka nchi za wafadhili na hata kukata bajeti za baadhi ya Wizara kwa 80% au hata zaidi!!!! Hakuna anayemuuliza kulikoni hadi bajeti ambayo ilikuwa ikidhi matumizi ya Serikali kwa miezi 12 iishe baada miezi sita? wataleta longo longo lao ambao ni uongo mtupu. Ukweli ni kwamba CCM walichota mabilioni ili kufanyia kampeni za uchaguzi wa 2010.

  Hawa BoT nao ni waongo wakubwa sana. Kila mwaka wao takwimu zao huonyesha uchumi wetu umekuwa kati ya 5% na kuendelea kitu ambacho si cha kweli bali ni kutaka kuibeba Serikali ili ionekane inafanya kazi vizuri. Itakuwaje uchumi wa nchi ukuwe kila mwaka kati ya 5% na kuendelea halafu ugumu wa maisha unaongezeka kila mwaka. Hizo takwimu za BoT zimejaa usanii mtupu. Ukiwauliza formula yao inayowawezesha kutoa tamko kwamba uchumi wa nchi unakuwa kila mwaka wanang'aa macho. Hiyo formula wanayotumia ni siri kubwa sana kamwe Wananchi hatutaijua. Natumai nchi za wafadhili hazitawapa hata senti tano ili Serikali hii ambayo inafuja mali sana ianze kupata akili ya kuyaepuka matumizi yaliyojaa matanuzi ambayo hayana tija yoyote kwa Watanzania.

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/109572-government-coffers-are-empty.html
   
 7. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Tunadanganywa kwa sababu tunapenda kudanganywa. Kama hatuwezi kuhoji kitu na kama kila kitu tunachoambiwa na wakubwa tunapiga makofi - tunakikubali - kwa nini tusidanganywe? Serikali inajua bila kutudanganya haiungwi mkono na ujanja ambao pia CCM inautumia. Kwa vile hatuhoji kitu na kwa vile hatufanyi utafiti pia, wakubwa wameyafanya yote haya kuwa mtaji wao na wanafanikiwa kwa hilo!
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  kwa sababu siye ni mabwege
   
 9. dazenp

  dazenp Senior Member

  #9
  Feb 13, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kwahiyo wale mliosema kuwa hatuhoji na sie waTz ni mabwegwe mnasuggest nini maana sioni solution zenu na hivyo ndivyo na nyinyi mnaonwa wajinga....kwakuwa hamtoi solution mnaishia kulalama tuuu tena jamiii forum not even on public
   
 10. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sisi ni Wadanganyika. Tunapenda kudanganywa kama watoto wadogo. Tuko radhi kusikia maneno matamu ya uwongo kuliko ukweli mchungu. Mkwere kaja na "maahadi mapya, usanii mpya na hakuna jipya" na bado tukampa nchi. Tukigundua tumedanganywa wanatupiga na uwongo mwingine tunalainika. Wanajua hiyo formula Tanzania tu inawezekana. Sasa watuambia ukweli halafu pageuke kuwa TUnisia, sidhani kama wao wajinga hivyo.....
   
 11. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  sijui hao wafadhili wenyewe watatoka wapi wakati marekani yenyewe kwenye makadirio ya bajeti yake ya 2012 inatarajia nakisi ya USD 1.48 Trillion,na kuhusu hali ya uchumi wataalamu wetu wachache ambao ni wabinafsi wanaoshirikiana kuudanganya umma kuwa hali ya uchumi ni nzuri huku tukiwa na mfumuko mkubwa wa bei na kuporomoka kwa sarafu yetu kila kukicha na hata siku moja hawazungumzii kuna UNEMPLOYMENT RATE kiasi gani kwa Tanzaniaaa.
   
Loading...