Kwanini tulipishwe kwa uzembe wa wengine?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini tulipishwe kwa uzembe wa wengine??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kyachakiche, Jul 2, 2009.

 1. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Kwa wale wadau ambao wamekuwa/wamewahi kutoa mizigo yao through Customs ama iwe kwa njia ya maji au anga, watakubaliana nami kuwa kuna baadhi ya gharama ambazo hulipwa na mwenye mzigo ambazo hazikusababishwa na yeye kwa njia yoyote ile. Mfumo ambao umewekwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), pamoja na wadau wengine kama, Ports, Shipping Lines, Clearing and Forwarding Agents zinawafanya kutokupata hasara yoyote katika biashara zao ikilinganishwa na (Mwajiri wao) mteja anayepitisha mizigo kwao.

  Nasema mwajiri wao kwa maana kuwa kama si huyu mteja, TRA hawana kazi ya kukusanya kodi, Bandari hawana kazi ya kupakia na kupakua mizigo, Shipping lines hawana mizigo katika meli zao na Clearing Agent hawana mzigo wa kutoa. Sasa nije kwenye pointi zenyewe:
  1.Bandari wameweka siku 7 tu tangu meli iingie kuchukua mzigo bila gharama za ziada(storages) bila kujali siku kuu, jpili,nk.
  2.S/Lines wanatoa siku 14 free kuchukua mzigo bila gharama za ziada(demurrages)
  3.TRA, ni siku 21. Zaidi ya hapo ama mizigo ipigwe mnada, au ulipie kinachoitwa Customs warehousing rent kama gharama ya ziada.
  4.C&F Agents wao wanasubiri malipo yao mzigo ukitoka.
  Taratibu hizo hapo juu zinafuatwa kikamilifu bila ya kujali factors nyingine kama ifuatavyo:
  1.Kuna Kitengo cha Cotecna/Tiscan ambamo documents zikiwakilishwa huko zinachukua hata two weeks eti kwa sababu ya price analysis.
  2.Ukitoka huko, upate assessment, kama malipo yanazidi 5million, lazima yapitie BOT ndipo yaende TRA, another 2 or three days,
  3.Baadaye, Customs wafanye sijui documentary checkup, uplifts of value, na baadaye unasikia nenda kakague, hii ni baada ya siku kama tatu baada ya kupokea malipo toka BOT.
  4.Ukifika port, unaambiwa space kwa physical verifications haipo labda baada ya siku mbli ama tatu. Siku ya tatu container inafunguliwa,afisa wa TRA anafanya ukaguzi, taarifa yake anaitoa baada ya siku 2. Hapo omba asirecomend price adjustments kwani inaweza hata kuchukua wiki moja.
  5. Ukienda kulipia bandarini unakuta storage kubwa iliyosabaishwa na mlolongo wote kama nilouweka hapo juu. Ukirudi kwa wenye meli unakutana na demurrage kubwa tu ya kuchelewesha Container lao hadi kuzidisha siku walizojiwekea.
  Jamani nawauliza wanajf wenzangu, mimi kama mwagizaji wa bidhaa, hapa napigwa faini kwa makosa gani? Mfumo wenyewe ndio huo, tufanyeje?
   
 2. Mathias

  Mathias Senior Member

  #2
  Jul 2, 2009
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hii kweli inatia uchungu, nafikiri inabidi wakubwa wafike pahala wafahamishwe mizengwe inayotokana na system yetu! Majuzi niliagiza gari kutoka Japan na limekaa bandarini zaidi ya mwezi, TRA wali uplift charges twice, na baadae katika kulalamika wakasema wali overlift! Na hapo katikati document zikapotea! Mpaka mwisho nimeishia kulipa storage charges pale bandarini 1.2million kwa uzembe wa watu wengine! Kitu ambacho nimekiona system yetu sio open! Taratibu zote za kufuata ni siri ya wafanyakazi! Na hakuna abc za kufuata kurahisisha uchukuaji wa mizigo! Kuanzia sasa ntakuwa naenda bandari ya Mombasa, manake bandari yetu haitusaidii kitu!
   
 3. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Nashangaa ni kwanini mapato ya Serikali yawe yakuunga unga. Mtu anatakiwa kulipa kodi ya halali na si vinginevyo. Hizi uplifts kutoka kwa maofisa wa TRA ndo chanzo cha rushwa kwani mara nyingi ukimfuatilia kwa karibu utasikia, ili tupunguze kidogo uta toa ngapi. Ukiamua kukomaa nao utazungushwa hadi ukute storage port ni kubwa kuliko hiyo uplift. Kwa mfumo wa kufukuzana na faini kwa wananchi kutawajengea hari ya kulipa kodi kwa uhuru?
   
 4. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #4
  Jul 7, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Mpaka hapo tutakapokubali kuachana na rushwa na kufuata taratibu (ambazo tayari zipo), matatizo haya hayatakwisha kamwe.

  Wafanyakazi wa TRA na TPA (haswa Dar) wamezoea rushwa, wamelemaa. Rushwa ni silaha kubwa ya Iblis, ukinogewa (si hela ya bureeee) basi utazoea na utaona ni haki yako kulipwa, kumbe umeshikwa na Shetani!

  Sisi tunaotaka kupitia njia ya halali tunalipishwa kwa uzembe wa makusudi, kwa kuwa tu hatukuwapatia "kidogodogo" chao! Wao wako Serikalini, wamepewa "mpini" wa kushika, sisi "makali", tujikate wenyewe.

  Uwajibikaji utakuja lini Tanzania? Rushwa rushwa! Wanasema kwa mdomo wanaipiga vita, kwa vitendo wanaihalalisha kabisa. Hatimaye TRA wanapiga mnada vitu vya watu waliokwamishwa (si walioshindwa) kulipa kodi kwa sababu ya urasimu uliojengwa ili kuhimiza mianya ya rushwa. Kubalini TRA, TPA, mnanuka rushwa, wote pamoja na TISCAN, TICTS na kadhalika! Mkondo mzima!
   
 5. Rabin

  Rabin Senior Member

  #5
  Jul 7, 2009
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Jamani mazingira na location ya ofisi zenyewe ndio hivyo mnavyoziona, huko kumeoza, document inatoka ofice moja kwenda nyingine umbali wa nusu km!! hii itapunguza rushwa na urasimu kweli?wafanyakazi wa bandarini na airport kwanza wao wanajifanya wanajua kila kitu hata kama mteja umeagiza mizigo yako zaidi ya mara mia kwao bado ***** tu, nasikia sasa hivi wanajifanya system mpya iliyowekwa haifanyi vizuri ili warudishiwe utaratibu wao wa zamani unaoruhusu mianya ya rushwa na ndiyo maana "system iko down" ndiyo imekuwa lugha yao hata kama siyo.
   
 6. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hapa ni simple ili kuwajibisha hawa jamaa wanaohusika katika hii red rape ni kutengeneza regulations kuwa kwa kuwa mwenye mali hatachelewesha na hawezi kuchewesha procedures zao. Muda ule wote utakaozidi idara husika ilipe fedha hizo na si kumfanya mwananchi kitu mbaya namna hii. Mbona malandcruiser yao yasicheleweshwe. Huu ni upumbaf mwingine. Kwani mtanzania anayeagiza gari hana pa kuliegesha? Mwachie mwananchi aende na gari lake na ndio hiyo kuchelewesha itakuwa valid. Hawa jamaa unajua wamesoma halafu shule ikajifuta kichwani mwao. Ni wajinga kabisa. Hasa idara zote zinazohusika na kodi. Ni wajinga sana. Why? Because wanamgeuza mwananchi maskini na kumwadhibu kwa kodi, kwa maan ya kwamba hamna return ya kodi yake katika maendeleo, badala yake ni ushenzi tu; ufisadi na ufirauni. Nachukia sana. Sasa ni wapi pana usalama katika nchi hii. Kila unapogusa pananuka utoko. Nchi ni afadhali iuzwe na kila mtu apate share yake akafie mbali.
   
 7. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Unajua dawa ni nini wakuu...sheria. Kama wanasheria wa bongo wangekuwa na moyo wa kutenda haki, bila woga, hapa kungekuwa kesi kibao. Yani hii process ingefanywa nyeupe kama hivi vitengo vingepelekwa mahakamani kwa uzembe.
  Sheria katika nchi ni kitu cha kuzingatia sana. Bila sheria hatuwezi kuwa na maendeleo. Vitu vitaendeshwa kwa mabavu na ubabe. Na hichi ndicho kinachofanya developed countries kuendelea kuwa juu...Utawala wa Sheria.
   
 8. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu, hapo umesema na niko na wewe, ila punguza ukali wa maneno(joke!!)
   
 9. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Lakushangaza na kusikitisha zaidi ni usiri wa watu wa TRA. Kwa mfano ukitaka kuagiza gari let say ya mwaka 2003, ukawa na proforma invoice na ukaamua kwenda nayo ofisi ya TRA(Customs) ili kutaka kujua ni kiasi gani cha kodi utakacho kuja kulipa pindi gari likifika, utazungushwa katika idara mbalimbali lakini hawatakuwa tayari kukupa tax estmates. Mwisho wa siku gari ikija utaambiwa gharama ni mara mbili ya ile ya kwenye proforma invoice. Ukiuliza ni kwanini, unaambiwa hiyo ndiyo bei waliyonayo kwenye data base yao. Swali hapa ni kwanini wasingetoa hiyo bei mwanzo ili mtu ajiridhishe kwamba yako tayari kwa malipo husika? Huu ni uonevu na tena ni wizi. Kama huna hicho kiasi, basi jiandaye kwa maumivu zaidi huko bandarini(storages)!!!
   
Loading...