Kwanini trafiki akisimamisha daladala, lori au basi anateremka konda/utingo na si dereva?

Penye udhia penyeza rupia.
Kazi ya dereva ni kuombwa leseni na kadi ya gari.
Kazi ya tingo au konda ni kuelezea wana kias gan cha fedha ya kubrashia viatu.
Traffic by necha akiamua kukutaftia kosa hawezi kulikosa kwenye gari yako.
Mimi hua najua kbsa gari haikosi kosa, kwaio naangalia ukubwa wa makosa yangu, mambo sijui ya kufunga mkanda, mara wiper haifanyi kazi, sijui taa imezima, nmepita kwenye nyekundu n.k hapo ni buku 2 kavu.
Kosa kubwa kama tairi kipara, mara bima imeisha, hapo ni dasi lililonyooka.
Na hua sirembi mwandiko, nnapotoa leseni mkono mmoja unakua umeshkilia noti iliokunjwa vzur mwingine una leseni, chaguo ni lake achukue kipi kati ya hivyo. Na mara zote hua hawaioni leseni ukishika noti.
 
Back
Top Bottom