Kwanini makondakta wa Daladala na Bodaboda wanaongoza kwa stori za uongo na kero?

mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
5,262
12,835
Ni kwasababu ya elimu duni, ukosefu wa ajira au malezi ya hovyo ndio yanafanya dereva wa boda boda na makonda wa dala-dala, kuwa kero.

Hizo Jamii mbili za hao watu wanaongoza kwa kusema stori za uongo na za umbeya, kama unataka kupata za uzushi mtaani kwako nenda karibu na kijiwe cha boda-boda utazipata tu.

Kwa makonda wa dala-dala na wapiga debe ndio wana ongoza kwa kutoa majibu ya kukera ya maudhi na kejeli kama we sio "gentleman" unaweza kujikuta unamtukana au unapigana na konda kwa dharau zao zile duh ndio maana konda akipigwa na askari yoyote raia wengi watakua upande wa askari, kwanini?

Konda atakuambia hoyaa bro ingia gari ni nyeupa nafasi kibao wakati imejaa nawengine wamesimama, ukisita kuingia tu toka mlogani na ubisho wako, kanunue yako.

Jana mama moja alikua mgeni hiyo sehemu akashawishiwa na konda apande dalala yake, kumbe dala dala haifiki kule anapoelekea, yule mama anaenda mbali na daladala inapita njia panda ya hiyo sehemu japo nauli ni ileile 400 lakini nadhani yule mama hakuwa na hela nyingine zaidi ya kupanda gari ya pili, gari ilivyofika njiapanda konda akamwambie 'maza' shuka mama akamjibu mbona sio hapa sijafika bado, konda shuka tu simama hapo njia panda usubiri picha ya pamoja na mgeni rasmi, yule mama alikakasirika kweli kweli, alimwambia kwa hasira ntakuroga wewe konda.

Je, wewe makonda walishawahi kukukera? Walikukera nini? Na nini kifanyike hiyo tabia ikomeshwe?

Screenshot_20210223-071452_Google.jpg
 
Back
Top Bottom