Mkuu kuna ukweli unachokisema ila unaweza ukatumia a small budget na bado movie ikawa bora, alafu pia inabidi kuangalia buying power ya wabongo peke yake na sababu ya piracy ni vigumu kutegemea hili soko ili uweze ku-return investment yako, wenzetu nje hawategemei soko la video tu.., bali matangazo, sponsorship, kuuzia tv networks na kuuzia majumba ya cinema.Lakini lengo la kuigiza ni kufanya biashara na movie itakayotoka hapo iweze kuuzika isiwe hasara, hivyo ndo maana tunaona movies nyingi za 4weeks na 20m budget. Hakuna utaratibu mzuri uliowekwa na serikali wa kusimamia usambazaji wa filamu hivyo si rahisi kuinvest 2years and a big budget for one movie.
Waandishi na waigizaji wa filamu tulio nao sasa ni njaa kali. Hakuta vipaji ujuzi wala kujituma zaidi ya umaarufu wa shilingi mbili. Wazo lako bomba ingawa nina shaka kama watanzania watazipenda kutokana na tabia ya kupenda udaku. Sometimes hawa watunzi wanaangalia upuuzi wanaopenda wateja wao. Leo hii magazeti ya udaku kuanzia wa nyumbani hata kwenye majengo ya ibada vimetawala. Angalia magazeti hayo ya udaku wa kidini na kifamilia yalivyoshamiri.
Ni kweli mkuu usemayo lakini hata kama ni udaku hivi kweli wabongo wanashindwa kujipanga na kutengeneza series kama Isidingo ya kibongo, ambayo itakuwa inacheza kila siku kwenye TV fulani ?, na hapa kama itakuwa ni bora nina uhakika TV (ITV, TBC, n.k.) watagombana ili kuipata sababu na wenyewe watapata matangazo na sponsorship.., kwahio hata kama ni huo udaku utengenezwe realistic na uwe na connection na maisha ya bongo ambayo mtanzania anaweza ku-associate.., kwanini prime time kwenye tv badala ya watu kuangalia isidingo kunakuwa na series ya maana ya kibongo, na sisi maybe tuweze hata ku-export hata Kenya na Uganda (more money for wasanii), watu kama wale Bishanga, Jangala na Kina mzee Jongo (yaani pure utanzania ambao watu wanaweza ku-associate)
Ni kweli mkuu kitabu ni tofauti na movie script.. (sababu movie script inabidi ielezee kila kitu kinachotokea, mazingira dialogue n.k., kwahio inakuwa more elaborative) sasa sababu movie za kibongo haziendi kitaalamu kwanini waandishi ambao nina uhakika wanaweza kuandaa dialogues bora zaidi wasitumike ?Waandishi wa vitabu na waandishi wa movie scripts ni watu wawili tofauti kabisa
Tatizo ni kwamba waandaaji wa films za kibongo hawataki kutumia vitabu vya kibongo kama vyanzo vya stori zao, wamekazana na zakutunga wenyewe